Elections 2010 Napenda Kuwapongeza Watanzania kwa Kuiadhibu CCM tarehe 30 October, 2010

Tanzania

Senior Member
Jun 6, 2008
115
195
Mimi binafsi, NEC na wengine walio wengi tunaamini kabisa CCM imeshindwa kwa kiasi kikubwa ktk Uchaguzi ulifanyika pamoja na kwamba wanaoneka kuongoza. Nakumbuka kabla ya Uchaguzi tuliwasikia viongozi na watu wengi wazalenda wakiwaasa watanzania kutumia kura yao vizuri na ndivho kilichofanyika. Hivyo napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza watanzania kwa kazi nzuri. Nawatia moyo msikate tamaa, yuko Mungu wa Isaka na Yakobo anaweza yote, yeye hufanya kwa wakati wake. Nawatakia amani na faraja na mtashuhudia jinsi gani Mungu anafanya kazi.
Mbarikiwe.
 

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,473
2,000
Naona msemo wa makamba kuwa slaa ni santuri mpya umemtokea puani
 

Ruge Opinion

JF-Expert Member
Mar 22, 2006
1,829
2,000
AMEEENNNN! kuna part ana play mungu ma part anaplay mwana adam:nono:
Kweli kabisa. Kuna wengine tuliotoa angalizo kabla ya uchaguzi kuwa vyama vya mageuzi vilikuwa havijajipanga vema kukabiliana na mbinu za CCM pamoja na vyombo vyake vya dola (kwa sasa) za kuiba kura. Lakini tulichokuwa tunasikia katika majukwaa ni uhakika kuwa kura hazitaibwa. Wansiasa wanapaswa kujua kwamba kura haziibwi siku ya kupiga na kuhesabu kura. Mipango inaanza mapema kabisa. Mfano, Ingawa kila mtu sasa amekazana kuwa watu hawakujitokeza kupiga kura wanasahau kuwa daftari lenyewe la wapiga kura limejaa majina feki ambayo yamewekwa kwa nia ya kuwezesha uibaji wa kura. Maana yake ni kwamba sababu wanayotoa ni ile ambayo wameelekezwa na Tume ya CCM badala ya kuangalia hali halisi. Haiwezekani watu wasijitokeze nchi nzima. Haiwezekani watu wampe mbunge wa upinzani kura za kishindi halafu za uraisi wampe Kikwete. Kwa hiyo, bila kujiweka sawa kitaalam pamoja na kufanya utafiti kabla ya kupanga mikakati ya ushindi hadithi itakuwa hii hii kila uchaguzi. Naomba niongeze kuwa katika majimbo ambayo uchaguzi umeahirishwa vyama vya mageuzi havitapata hata kiti kimoja kwa sababu sasa CCM na dola wataelekeza nguvu zote kule. Tuambizane baada ya uchaguzi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom