Wakikujibu ni shutue mkuu kwa nadikao lako lililoenda shuleBaada ya kusikiliza na kusoma hoja za viongozi wanaotetea na kuunga mkono ujenzi wa bandari ya bagamoyo kuwa ujenzi huo una maslahi na faida kwa watanzania naona ni wakati muafaka viongozi hao wanielimishe ni kwa namna gani wachina watafaidiaka na bandari hiyo na watapata faida gani ili twende sawa.
Ikumbukwe mpaka kufikia january, 2021 china wamejipatia bandari 20 za deep water na viwanja vya ndege. Zambia kwa mfano wameshindwa kulipa uwekezaji uliogharimu $8B kwenye miundombinu ya barabara na kupelekea kupoteza kiwanjancha ndege, shirika la umeme na shirika la utangazaji. Zambia imekuwa nchi ya wachina wanafanya watakalo.
Mfano mwingine ni pakistani, kenya, na sri lanka. Fedha za china zina moto mfano deni la kenya ni SGR yao ambayo mpaka sasa haijaweza kutimiza malengo yaliyo kusudiwa. Kenya waliweka bondi bandari yao ya nchi kavu ya nairobi.
Vp kama kiongozi akikubali mradi huu alafu baadae ukawa floppy atakumbukwa na vizazi vya mbele kama mtu wa namna gani? Miradi ya ufadhili wa china ni kama ina gundu. Mfano ni nchi kama ecuador nao waliingia kwenye mtego wa dola milioni 19 china wamechukua umiliki wa mafuta yao. Djibout wao wanadaiwa dola 590 milioni wameshindwa kulipa road na belt infrastructure.
Ieleweke kwamba Huo uwelezaji ni deni sio bure vp kama tukishindwa kulipa hilo deni? Kuna Ulazima wa bandari hiyo kujengwa?. Je bandari hiyo itapelekea kupungukiwa uwezo wa bandari yetu ya asili ( sisi watanzania mali yetu ni bandari ya dar es salaam) vp bandari nyingine zitakufa kama tanga na mtwara. Je hakuna suluhisho lingine badala ya ujenzi wa bandari ya bagamoyo labda tuingie ubia kupanua bandari ya mtwara yani mchina na mtanzania waingie partership kukuza bandari moja kati ya hizo tatu kubwa.
Kwanini kuna wasiwasi kuwa ujenzi wa bandari hiyo kubwa sana utafanya bandari zingine zife kwa kukosa mizigo na kutokana kuwa na teknolojia ndogo manake wachina wataweka mikazo kuwa mizigo yote inayotoka china ipitie bandari yao ya bagamoyo. Ni wangapi watakao kosa kazi baada ya bandari hizo kufa.
Je kuna viongizi wenye tamaa wanao harakisha ujenzi wa bandari hii ya bagamoyo?
Asante.