Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,753
7,844
Wajemeni eeh

Kuuliza si ujinga na kuuliza njia ndio kujua njia!

Nahitaji bastola, kwa self defence tu, si vinginevyo! Sababu; najiona vulnerable mno huko 'uswekeni' ninakoishi. Hamna umeme, na majirani wanahesabika, BTW, practicing targets zipo za kutosha huko!

Najua humu kuna wengi tu wanaomiliki silaha kikazi, na wanaomiliki silaha kwa sababu kama zangu mie,..tatizo sijui "a" wala "be" nianzie wapi, meaning sheria na taratibu zikoje Bongo kumiliki silaha, hivi kuna duka la silaha Bongo?

Wapi?

Mfano; nikipata semi auto M92 Beretta yenye uwezo wa rounds 12 au 15 inatosha, au kuna 'limit' ya silaha ya aina gani naruhusiwa kuwa nayo? natamani kuagiza nje lakini nahofia nisijebanwa na sheria za uingizaji silaha...

Maduka ya kununua bastola dar yapo kama 2 ninayoyafahamu moja lipo pale mitaa ya stesheni, nyuma ya jengo la TRA, linaitwa Tanganyika Arms. Hili ni private(meaning price pia ni kubwa). Pia unaweza Wenda kununua pale Makao Makuu ya Jeshi Upanga kuna duka la Mzinga(bei fresh sana pale ila nyingi ni za kutoka nchi za kisoviet).

Vile vile unaweza kuagiza ulaya kama unataka quality like Colt 45 na ikifika unaiclear halafu inahifadhiwa pale Tanganyika Arms mpaka upate kibali(Ila kuwa makini sana hapo maana inabidi jamaa wakutumie serial number ya bastola, wakiiuza na kuleta ingine kazi utakuwa nayo kwenye kuprocess kibali)

Kupata kibali cha kumiliki ndo kimbembe maana procudure inaanzia kwa mtendaji wa kata ambaye anaitisha kikao cha usalama na wanaclear.

Ukitoka hapo unaenda polisi wilayani, for clearance, then wilayani, baada ya hapo ni kwa mkuu wa mkoa ambapo unakuwa endorsed na kikao cha usalama cha mkoa. Kwa Dar nasikia kinafanyika mara chache sana.

Ukimaliza hapo ndo unaenda Polisi Mkoa then Makao Makuu ya Polisi(Registry, na figure prints department) na finaly kibali kinatoka kwa DCI.KIbali kikitoka unaenda kuchukua "Ngoma yako".

Kuna watu imewachukua zaidi ya mwaka kwa hii process, lakini wengine inachukua miezi 2, depending on your connection.

Goodluck

Miaka 3 iliyopita niliwahi kwenda kwenye lile duka la silaha pale Samora (Behind TRA) ili kujionea Silaha zenyewe. Walinipokea vizuri tu na walikua cooperative sana kunionyesha silaha za aina mbalimbali, kunitajia bei zake na hata kunipa nizishike na kuzikagua endapo ningeipenda.

Waliniambia kama kuna niliyoipenda utaratibu ni kwamba ningetakiwa kulipia Full amount (ilikua ina Rage from 700,000 to 1,500,000 depending on features) Lakini huchukui Silaha.

Baada ya hapo wangenipa Fomu 1 in 4 copies, ambayo ningeenda nayo Serikali za Mitaa, Kamati ya usalama ya Mtaa ingekaa na kunijadili na kuziforward hizo Form katika Kamati ya Usalama ya Wilaya ambapo wangezipitia na Kuziforward Katika Kamati ya usalama ya Mkoani na hatimaye mwishoni zingepelekwa Central Police Station.

Kila Stage itakapopitia copy moja ya hizo fomu hubaki huko kwa kumbukumbu. Vilevile walisema the main uzito mkubwa uko katika mapendekezo ya kamati ya usalama ya mtaa na Wilaya, Zikipita stage hiyo Mkoani na taifani hakuna shida kwa sababu hawakufahamu.

Baada ya Fomu kufika Central Policy Station, wao watakuita na kama wameridhika na recommendation za ngazi zote watatoa idhini ya wewe kwenda kuchukua hiyo silaha yako uliyolipia, Pamoja na Kitabu cha Silaha hiyo ambacho kitatumika wakati wa ukaguzi wa Silaha unaofanyika kila mwaka.

Unless wewe ni mwanajeshi au Polisi, Utatakiwa kulipia gharama za mtu kukupeleka Range kwa ajili ya kujifunza kutumia Silaha.

Process nzima kuanzia ulipolipia hadi kukabidhiwa silaha yako inaweza chukua miezi mitatu

Baada ya hapo unakua Mmiliki halali wa Silaha.

KUHUSU UTARATIBU WA KUMILIKI SILAHA KISHERIA

Mimi ninavyofahamu kama unataka kumiliki kwa mara ya kwanza utaratibu ni huu:

1. Utanunua silaha kutoka maduka ya Mzinga Corporation au Tanganyika Arms Ltd au kutoka kwa mmiliki halali ambapo utakuwa na mkataba wa mauziano na pia kitabu cha umiliki wake (kama umenunua kwa mtu). Hiyo silaha hautapewa ila itabaki mikononi mwa uhifadhi wa Mzinga Corporation, Tanganyika Arms au central police station na wewe kupewa nakala ya Receiving Note kuonyesha kwamba silaha imebaki mikononi mwao kwa utunzaji. Kama ni silaha ya urithi basi kuwepo na muhtasari wa kikao cha wanandugu kilichoridhia wewe kumilikishwa silaha hiyo (wakati huo silaha inayotakiwa kurithiwa ikiwa mikononi mwa moja ya hizo sehemu nilizotaja hapo juu).

2. Utaenda polisi (mfano ofisi ya kamanda wa polisi wa wilaya) na kupewa fomu utakayotakiwa kuijaza maelezo yako kama jina, unapoishi, sababu za kuhitaji silaha, maelezo ya silaha uliyonunua.

3. Fomu yako itatakiwa ipate maoni ya serikali yako ya mtaa, kamati ya ulinzi na usalama ya kata yako (hawa watatakiwa pia kuandika muhtasari kuonyesha kuwa wamekujadili na kukukubalia). Hapa inaweza kuchukua siku chache tu au muda mrefu. Itategemea na UCHESHI wako.

4. Utatakiwa kupitisha fomu yako kwa hakimu au mwanasheria. Hapa ni suala la dakika chache tu na uchakavu kidogo.

5. Utatakiwa uende polisi forensic department kuchukuliwa alama za vidole kupata clearance certificate kuonyesha kuwa hauna kosa lolote la jinai. Kuchukua alama na kupata majibu ni ndani ya kama siku tatu hivi japo kuna uwezekano pia wa kupata majibu siku hiyo hiyo. Na kwa ujumla hapa hapana usumbufu wowote. Kuna malipo kidogo utalipia. Kama sikosei ni Tshs. 3,000/= au 5,000/=.

6. Ukiwa na muhtasari huo wa kamati ya kata, barua yako ya maombi (covering letter), clearance certificate ya Forensic department, fomu yako iliyokwisha sainiwa na ofisi ya serikali ya mtaa, kamati ya ulinzi na usalama ya kata, hakimu au mwanasheria utavipeleka ofisi ya kamanda wa polisi wa wilaya ili nae akusainie covering letter yako na ile fomu yenye maelezo yako na silaha. Hapa ndipo uchukua muda kwani lazima kuwe na kikao cha kamati ya ulinzi na usalama cha wilaya kitakachokaa na kujadili maombi ya watu wengi na wewe kutakiwa kuhojiwa mbele ya hiyo kamati ambayo vikao vyake ufanyika mara moja moja. Ukikubaliwa muhtasari wa kikao utaandaliwa na nakala yake kuambatanishwa kwenye maombi yako. Kama nilivyokwishasema hapa ndipo nyaraka zinaweza kukaa muda mrefu zaidi nadhani kuliko kwingine pote (hata miezi kadhaa) kwa sababu vikao vya kamati ufanyika mara moja moja.

7. Kamanda wa polisi wa wilaya ambaye ndiye katibu wa kamati ata forward hizo nyaraka zako ili zikapitishwe pia na kamanda wa polisi wa mkoa, kamanda wa polisi wa kanda maalumu, na hatimae kwa Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai ambaye ndiye anaetoa kibali cha umiliki wa silaha husika. Huku kwa kamanda wa polisi wa mkoa, kamanda wa polisi wa kanda maalumu na pia kwa Mkurugenzi nyaraka hazikai sana.

8. Kibali hicho uwa valid kwa muda wa miezi mitatu na usipokilipia ndani ya muda huo utalazimika kwenda ofisi ya Mkurugenzi ili kuongezewa muda wa kulipia kibali hicho.

9. Ukishalipia hicho kibali utaenda wizara ya mambo ya ndani makao makuu (kwa watu wa Dsm) ili ukaandikiwe kitabu cha kumiliki silaha kwa jina lako na pia chenye picha yako (Firearm Licence). Zoezi hili linahitaji muda mfupi tu siku hiyo hiyo.

10. Utachukua kitabu chako na kwenda ofisi ya kamanda wa polisi wa mkoa ili uandikiwe kibali cha kukuruhusu kununua risasi (haichukui muda-dakika chache).

11. Utaenda ulipohifadhi silaha yako (Mzinga, Tanganyika Arms au central police station) ukiwa na leseni yako na pia kibali cha kununulia risasi na hivyo kukabidhiwa silaha yako na pia kuuziwa risasi kwa idadi iliyokubaliwa kwenye kibali. Hapa utatakiwa kulipia storage charges za hiyo silaha tangu ulipoiacha hapo hadi siku hiyo unapotaka kuichukua.

12. Baada ya kupata leseni ya umiliki wa silaha kila mwaka (kuanzia Julai hadi Septemba) unatakiwa kulipia leseni yako. Baada ya Septemba utatakiwa kulipa na faini.

Kwa mtu anaebadilisha kunakuwa hakuna mlolongo mrefu kama hapo juu. Ataandika covering letter kwenda kwa kamanda wa wilaya anayoishi akiwa na vielelezo vyote vya silaha mpya na ya zamani. Lakini hakutakuwa na haja ya muhtasari wa vikao vya kamati za ulinzi na usalama vya ngazi ya kata na pia wilaya ambavyo ndivyo vinavyosababisha zoezi zima kuchukua muda mrefu na pia usumbufu usio wa lazima (hasa huku ngazi ya mtaa na kata kwani kama mjuavyo kila mtu anataka nafasi yake imwezeshe kupata mboga ya nyumbani na pia jioni kujenda heshima baa).

Angalizo: Mimi siyo polisi na wala siko ofisi zinazohusika kutoa leseni za umiliki wa silaha. Nilichoandika ndicho ninachofahamu kwa upande wangu kama mdau wa kawaida. Hivyo kunaweza kukawa na masahihisho fulani kwenye maelezo yangu kutoka kwa wenye ufahamu zaidi. Hata hivyo naamini kama masahihisho yapo basi yatakuwa si makubwa sana.

Sheria ya umiliki wa Bunduki Tanzania
Tanzania tuna matatizo mawili makubwa:
(a) tunapenda sana kuiga mambo ya nchi za nje hasa marekani,
(b) tunawaogopa sana viongozi wetu kiasi kuwa wakitoa tamko hata kama ni wazo lao binafsi tunalichukulia kama ni sheria.

Swala la umiliki wa silaha za moto (bunduki) ni jambo ambalo siamini kuwa liliwahi kujadiliwa kwa kina na bunge letu bali lilitolewa kama agizo kutoka kwa Waziri mkuu (Sumaye) wakati ule. Matokeo ya umiliki hovyo wa bunduki, na hasa bastola, umesababisha mambo mengi ya ukiukwaji wa amani kwa raia wa kawaida, hasa yakiwahusisha watu wa ngazi za juu katika jamii: viongozi na wafanya biashara.

Marehemu Mzuzuri anakumbukuwa sana kwa hili, ila kuna watu wengi sana kama watoto wa wanasiasa wakongwe Kingunge na Mungai, na viongozi wengine mbalimbali pamoja na wafanya biashara wa viwango tofauti kama vile Mbilinyi Hartmann na steven Kanumba.

Umiliki wa silaha za moto kwa nchi kama Marekani ni swala tete sana ambapo makampuni ya utengenezaji wa bunduki yanatumia nguvu kujihakikishia soko la bidhaa zao hizo. Hata hivyo, Marekani bado wamegawanyika kuhusu umiliki wa silaha hizo ingawa vile vile wana sheria ngumu sana kuhusu utumiaji wa silaha za moto. Kuna mlolongo wa background check kabla mtu hajaruhusiwa kununua bastola, na state nyingine , kwa mfano Florida, wana sheria inaitwa 10-20-life kama inavyoelezwa hapa. Chini ya sheria hiyo, kutoa vitisho kwa kutumia silaha ya moto kunampeleka mtu jela miaka kumi na zaidi. Halafu kama ataua basi ajue naye atanyongwa bila cha swaleh mtume. Florida ni state ya pili kwa unnyongaji huko Marekani. Pamoja na kuwepo kwa hatua hizo, Marekani wamekuwa wansumbuliwa sana na mauaji ya hovyo ya utumiaji wa bunduki zinazonunuliwa mitaani, kwa mfano yale mauajia ya Virginia Tech na yale yaliyofanywa na Major Nidal Malik Hasan huko Texas hivi majuzi.

Kinachonifanya nianzishe thread hii, ni ukuaji wa vitisho na matumizi ya silaha za moto nchini kwetu kwa ubishi mdogo tu kama eti kugombea "demu."
Jana niliongea na ndugu yangu mmoja kule Tabora akaniambia kuwa mtoto wa Profesa Kapuya aliua kijana mwenzie kwa kumpiga risasi kwa bastola eti wakigombea DEMU: sijapata data zaidi kuhusu tukio hilo, ila hiyo ni trendi inayoonekana kuwa ya kawaida kwani wiki chache zilizopita kulikuwa na uvumi wa mwana sinema Hartmann kuwatishia mahasimu wake kwa bastola kwa vile eti walimnyang'anya DEMU.

Swali langu ni kuwa je Tanzania tulinogewa wapi na uzuri wa bunduki hadi kuwa na sheria za kuwaruhusu watu kumiliki bundukuki kiholela? Kwa utaratibu wa sasa tuna mwanya mdogo sana wa kujua tofauti kati ya jambazi na raia mwema tukiwaona wakiwa na bunduki.

Tulizoea bunduki kubwa (shortgun+ rifle) kama silaha za kuwindia tu. Bastola ni silaha ya kuua mtu, siyo silaha ya kuacha kila mtu ajibebee mfukoni na kwenda nayo kwanye vilabu.

Naomba Bunge letu liangalie tena sheria yoyote inayohusu umiliki holela wa silaha za moto kama bastola. Ningefurahi kama wataweka sheria ya kusimamia matumizi ya silaha hizo kama ile ya 10-20-life inayotumika Florida

Mfano; nikipata semi auto M92 Beretta yenye uwezo wa rounds 12 au 15 inatosha, au kuna 'limit' ya silaha ya aina gani naruhusiwa kuwa nayo? natamani kuagiza nje lakini nahofia nisijebanwa na sheria za uingizaji silaha.

Good reliable gun. Ila stopping power yake sio kubwa, risasi za 9mm zinapenya, stopping power yake sio kubwa sana unless umelenga sehemu nyeti. Silaha ya kujilinda ningeshauri kuwa na bastola inayotumia risasi .45 ACP, k.m. Heckler & Koch USP.
 
wajemeni eeh

kuuliza si ujinga na kuuliza njia ndio kujua njia!

... nahitaji bastola, kwa self defence tu, si vinginevyo! Sababu; najiona vulnerable mno huko 'uswekeni' ninakoishi. Hamna umeme, na majirani wanahesabika, BTW, practicing targets zipo za kutosha huko!

Najua humu kuna wengi tu wanaomiliki silaha kikazi, na wanaomiliki silaha kwa sababu kama zangu mie,..tatizo sijui "a" wala "be" nianzie wapi, meaning sheria na taratibu zikoje Bongo kumiliki silaha, hivi kuna duka la silaha Bongo?

wapi?

mfano; nikipata semi auto M92 Beretta yenye uwezo wa rounds 12 au 15 inatosha, au kuna 'limit' ya silaha ya aina gani naruhusiwa kuwa nayo? natamani kuagiza nje lakini nahofia nisijebanwa na sheria za uingizaji silaha...

Maduka ya kununua bastola dar yapo kama 2 ninayoyafahamu moja lipo pale mitaa ya stesheni, nyuma ya jengo la TRA, linaitwa Tanganyika Arms. Hili ni private(meaning price pia ni kubwa). Pia unaweza kwenda kununua pale Makao Makuu ya Jeshi Upanga kuna duka la Mzinga(bei fresh sana pale ila nyingi ni za kutoka nchi za kisoviet). Vile vile unaweza kuagiza ulaya kama unataka quality like Colt 45 na ikifika unaiclear halafu inahifadhiwa pale Tanganyika Arms mpaka upate kibali(Ila kuwa makini sana hapo maana inabidi jamaa wakutumie serial number ya bastola, wakiiuza na kuleta ingine kazi utakuwa nayo kwenye kuprocess kibali)

Kupata kibali cha kumiliki ndo kimbembe maana procudure inaanzia kwa mtendaji wa kata ambaye anaitisha kikao cha usalama na wanaclear. Ukitoka hapo unaenda polisi wilayani, for clearance, then wilayani, baada ya hapo ni kwa mkuu wa mkoa ambapo unakuwa endorsed na kikao cha usalama cha mkoa. Kwa Dar nasikia kinafanyika mara chache sana. Ukimaliza hapo ndo unaenda Polisi Mkoa then Makao Makuu ya Polisi(Registry, na figure prints department) na finaly kibali kinatoka kwa DCI.KIbali kikitoka unaenda kuchukua "Ngoma yako".

Kuna watu imewachukua zaidi ya mwaka kwa hii process, lakini wengine inachukua miezi 2, depending on your connection.

Goodluck
 
ya kupigia wanyama au watu?

:D ...acha maskhara yakhe! Bastola ya kuulia wanyama? ...kwa self defence, wala sio kusudio langu kuua mtu, huko 'porini' nikivamiwa na majambazi ya Kibongo atleast nijue wapi pa kutokea.

si nunua panga au .. uhame tu hapo unapokaa ....mtu mwenyewe kasema hajui lolote kuhusu mtutu sasa mnampeleka tu .. tutampoteza oho .... we haya

No naimaomari, ni taratibu tu za kumiliki silaha bongo. MajambaZI wa Bongo wanapokuja na AK-47 na kufunga mtaa hilo panga wala hutoliona... labda unipe mbinu za 'kinjeketile Ngwale' za kugeuza risasi kuwa maji!
 
Good reliable gun. Ila stopping power yake sio kubwa, risasi za 9mm zinapenya, stopping power yake sio kubwa sana unless umelenga sehemu nyeti. Silaha ya kujilinda ningeshauri kuwa na bastola inayotumia risasi .45 ACP, k.m. Heckler & Koch USP.

Na kweli M42 pia uwe umeshiba wakati unafyatua. Hiyo .45 ACP H&K USP inakitako kikubwa, handling yake mgogoro, sitaki dubwana linalo 'bulge' kwenye nguo.

Nini ushauri wako kuhusu Sig sauer P250 9para, au TAURUS slim 9para? ...all in all ni silaha ya self defence tu... not less than 12 rounds, ukivamiwa na mwenye AK-47 si unajua tena yeye 'ananyeshea mvua' tu mpaka magazine yake iishe.
 
...unaweza kuagiza ulaya kama unataka quality like Colt 45 na ikifika unaiclear halafu inahifadhiwa pale Tanganyika Arms mpaka upate kibali(Ila kuwa makini sana hapo maana inabidi jamaa wakutumie serial number ya bastola, wakiiuza na kuleta ingine kazi utakuwa nayo kwenye kuprocess kibali)

Kupata kibali cha kumiliki ndo kimbembe maana procudure inaanzia kwa mtendaji wa kata ambaye anaitisha kikao cha usalama na wanaclear. Ukitoka hapo unaenda polisi wilayani, for clearance, then wilayani, baada ya hapo ni kwa mkuu wa mkoa ambapo unakuwa endorsed na kikao cha usalama cha mkoa. Kwa Dar nasikia kinafanyika mara chache sana. Ukimaliza hapo ndo unaenda Polisi Mkoa then Makao Makuu ya Polisi(Registry, na figure prints department) na finaly kibali kinatoka kwa DCI.KIbali kikitoka unaenda kuchukua "Ngoma yako".

Kuna watu imewachukua zaidi ya mwaka kwa hii process, lakini wengine inachukua miezi 2, depending on your connection.

Goodluck

...na kweli ni mtiririko mrefu... unatoa mianya mingi ya rushwa humo 'njiani', anyway,

mtaka cha uvunguni...

...hiyo silaha, nitaruhusiwa kwenda nayo Zanzibar? nasikia huko huruhusiwi mtu yeyote kumiliki silaha?

Thanks for your very useful info.
 
Mimi ya kwangu nimeitoa hivi majuzi tuu baada ya process ndeefu. Mane, I feel like bustin' a cap in some nigga's ass! (teh-teh-teh).

...Lucky you!,

...tatizo unaweza ukajiona kama John Wayne wakati dereva wa dalafala anakupa 'mid-finger salute' nawe upo full loaded!

:D

hizo process ndeeeeefu ndio mimi zinaniacha hoi...
 
...na kweli ni mtiririko mrefu... unatoa mianya mingi ya rushwa humo 'njiani', anyway,

mtaka cha uvunguni...

...hiyo silaha, nitaruhusiwa kwenda nayo Zanzibar? nasikia huko huruhusiwi mtu yeyote kumiliki silaha?

Thanks for your very useful info.

Zanzibar hawaruhusiwi kumiliki silaha.

Ukiwa unamiliki bastola lazima ujue kuitumia vizuri, isije ikakudhuru mwenyewe kwa kujipiga risasi, au kuingia katika hali ya kuhatarisha maisha yako. Unapomiliki silaha, hasa ya kujilinda inabidi ujue sheria vizuri, na ni yepi yatakayokusibu ukiwa umejeruhi/kuua mtu.

Hivyo ni vizuri kuifahamu silaha yako vizuri, kwenda range mara kwa mara, na ikiwezekena kujiunga na club za kufanya mazoezi ya kujilinda.

Huko utafundishwa namna ya kufanya pindi utakapojikuta katika hali ambayo itabidi uchomoe bastola yako.
 
Ndugu yangu, mshale wa kisasa ni more effective na efficent kuliko bastola. Na hauna matata kisheria unaweza kumiliki bila kibali, na ni mzuri sana kwa kupambana na majambazi na wezi, very silence! Ukikaa mahali na mishale yako ukifyautua hawezi kujua uko wapi, tofauti na bastola( Labda iwe na silencer) Lakini unatakiwa kujua namna ya kuutumia, Ushauri tu.
 
...na kweli M42 pia uwe umeshiba wakati unafyatua. Hiyo .45 ACP H&K USP inakitako kikubwa, handling yake mgogoro, sitaki dubwana linalo 'bulge' kwenye nguo,

...nini ushauri wako kuhusu Sig sauer P250 9para, au TAURUS slim 9para? ...all in all ni silaha ya self defence tu... not less than 12 rounds, ukivamiwa na mwenye AK-47 si unajua tena yeye 'ananyeshea mvua' tu mpaka magazine yake iishe.

Hizo bastola ulizotaja ni nzuri, na zinafaa kwa carry conceal, lakini ushauri wangu utafute bastoa inayotumia caliber kubwa ya risasi k.m. .45 ACP. Hii ina stopping power kubwa ambapo ukimpiga adui lazima itamuangusha mara moja. Caliber ya 9mm sio mbaya, ila stopping power yake sio kubwa kama .45 na inaweza kupenya isifanye madhara sana ya kumsimamisha adui mara moja. Ningeshauri bastola ya aina hiyo hiyo kama sig p220 .45 compact
 
na smell smell mtu anataka kudito watu....kijana angaliaaaa!!!!mie ushauri wangu ingia gym kula nondo la nguvu ukitoka kachukue tizi la karate self defense tosha kabsaaaa tuone ka kuna mtu atakusumbua wala kukugusa!!
 
...Risasi inapofyatuliwa kuna mawili, moja ukiusikia mlio wa bastola/bunduki jua imemkukosa hiyo! PILI kwa mlio huo huo, utalala chini mwenyewe bila kuambiwa, nilikuwa mahala zikafyatuliwa toka kwenye AK-47, ...palifuatia ukimya kuanzia Binadamu, mbwa mpaka Mbu...!
 
Hizo bastola ulizotaja ni nzuri, na zinafaa kwa carry conceal, lakini ushauri wangu utafute bastoa inayotumia caliber kubwa ya risasi k.m. .45 ACP. Hii ina stopping power kubwa ambapo ukimpiga adui lazima itamuangusha mara moja. Caliber ya 9mm sio mbaya, ila stopping power yake sio kubwa kama .45 na inaweza kupenya isifanye madhara sana ya kumsimamisha adui mara moja. Ningeshauri bastola ya aina hiyo hiyo kama sig p220 .45 compact

Kitia, ahsante sana kwa ushauri, darasa nimelielewa. Shukran.
 
Ukiona urasimu bongo mkubwa kama ilivyo jadi,sema nikupe bastola ya kijadi.Haina usajili,leseni haina wala hakuna atakayejua kama unayo.Bastola hiyo ni kwa ajili ya kuzuia wezi tu si kuua wala kwenda kuibia.

Ni kimti fulani unaweka home kwako basi,wezi wakija nyumba hawaioni basi,kama una mshiko mkubwa,basi unanusa kijiti chako,vibaka/wezi hawakuoni.Hizo za kisasa balaa.
 
wajemeni eeh

kuuliza si ujinga na kuuliza njia ndio kujua njia!

... nahitaji bastola, kwa self defence tu, si vinginevyo! Sababu; najiona vulnerable mno huko 'uswekeni' ninakoishi. Hamna umeme, na majirani wanahesabika, BTW, practicing targets zipo za kutosha huko!

Najua humu kuna wengi tu wanaomiliki silaha kikazi, na wanaomiliki silaha kwa sababu kama zangu mie,..tatizo sijui "a" wala "be" nianzie wapi, meaning sheria na taratibu zikoje Bongo kumiliki silaha, hivi kuna duka la silaha Bongo?

wapi?

mfano; nikipata semi auto M92 Beretta yenye uwezo wa rounds 12 au 15 inatosha, au kuna 'limit' ya silaha ya aina gani naruhusiwa kuwa nayo? natamani kuagiza nje lakini nahofia nisijebanwa na sheria za uingizaji silaha...

Kila la heri katika jitihada zako za kulijinda wewe na familia yako pia na mali zako. Ombi moja tu ukiipata basi uwe makini sana mahali unapoiweka ili isije ikasababisha madhara makubwa ndani ya familia yako.
 
Maduka ya kununua bastola dar yapo kama 2 ninayoyafahamu moja lipo pale mitaa ya stesheni, nyuma ya jengo la TRA, linaitwa Tanganyika Arms. Hili ni private(meaning price pia ni kubwa). Pia unaweza kwenda kununua pale Makao Makuu ya Jeshi Upanga kuna duka la Mzinga(bei fresh sana pale ila nyingi ni za kutoka nchi za kisoviet). Vile vile unaweza kuagiza ulaya kama unataka quality like Colt 45 na ikifika unaiclear halafu inahifadhiwa pale Tanganyika Arms mpaka upate kibali (Ila kuwa makini sana hapo maana inabidi jamaa wakutumie serial number ya bastola, wakiiuza na kuleta ingine kazi utakuwa nayo kwenye kuprocess kibali)

Kupata kibali cha kumiliki ndo kimbembe maana procudure inaanzia kwa mtendaji wa kata ambaye anaitisha kikao cha usalama na wanaclear. Ukitoka hapo unaenda polisi wilayani, for clearance, then wilayani, baada ya hapo ni kwa mkuu wa mkoa ambapo unakuwa endorsed na kikao cha usalama cha mkoa. Kwa Dar nasikia kinafanyika mara chache sana. Ukimaliza hapo ndo unaenda Polisi Mkoa then Makao Makuu ya Polisi(Registry, na figure prints department) na finaly kibali kinatoka kwa DCI.KIbali kikitoka unaenda kuchukua "Ngoma yako".

Kuna watu imewachukua zaidi ya mwaka kwa hii process, lakini wengine inachukua miezi 2, depending on your connection.

Goodluck

(Ila kuwa makini sana hapo maana inabidi jamaa wakutumie serial number ya bastola, wakiiuza na kuleta ingine kazi utakuwa nayo kwenye kuprocess kibali)

Je taabu yote hii.

Kupata kibali cha kumiliki ndo kimbembe maana procudure inaanzia kwa mtendaji wa kata ambaye anaitisha kikao cha usalama na wanaclear. Ukitoka hapo unaenda polisi wilayani, for clearance, then wilayani, baada ya hapo ni kwa mkuu wa mkoa ambapo unakuwa endorsed na kikao cha usalama cha mkoa. Kwa Dar nasikia kinafanyika mara chache sana. Ukimaliza hapo ndo unaenda Polisi Mkoa then Makao Makuu ya Polisi(Registry, na figure prints department) na finaly kibali kinatoka kwa DCI.KIbali kikitoka unaenda kuchukua "Ngoma yako".

Ni kwasababu ya kupata serial number nyingine ama ndiyo kawaida ya process hata kama serial number ni sahihi?
 
Back
Top Bottom