Napenda kuifahamu Tanganyika Law Society(TLS)

Ofcoz inaonekana haina nguvu coz waliokuwa wakiongoza huenda walimezwa na system wakamezeka. Ila kwa sasa waliona wanashindwa kumeza wakataka wateme ili wapate wa saiz yao. Ikashindikana, jiulize ngosha aliongea kwa ukali sana alivyoona TL anagombea na dalili za kushinda zikiwa ni kubwa.
By the way impact ulimboka serikali ilihaha sana
 
Nianze kwa kusema Tuu kuwa Mimi si Mwanachama Wa Chama Chochote hapa Tanzania! Lakini ni mfuatiliaji wa karibu wa mambo yanayo husu siasa na Jamii kwa Ujumla!

TLS ni kitu ambacho hakisikiki sanaa na Labda kwa mwaka huu kimeweza kusikika kwa Ajili ya Uchaguzi huu na ni vile tuu Mpinzani kagombea na upinzani kazi yao ni kukuza mambo!

Mimi najiuliza Faida za TLS kwa Watanzania ni zipi? TLS imefanya makubwa yapi ambayo watanzania wanaweza Kujivunia? TLS ina Impact gani katika Serikali zaidi ya Bunge? Najiuliza hivi kwasababu nashangaa kuona ni uchaguzi unao ongelewa vibaya Mno kama Vile kuna kitu kipya kinakuja Tanzania

Oky Lissu kashinda lakini najiuliza katika TLS Lissu kawa Mwanachama Tokea lini na Kipi alikifanya Katika TLS?

Nielewesheni Faida za TLS katika Jamii......
 
Nmebaki najiuliza kuhusu powers za Rais wa TLS katika Nchi yetu hii pendwa, sipati jibu, pamoja na majukumu mbali mbali ya TLS na pamoja na influence ya Rais wa TLS katika masuala ya kisheria hapa nchini lakini bado sijawahi kuona wala kusikia uchaguzi wa TLS uliofuatiliwa na watanania wengi kiaasi hiki!!!
Nilichokiona Serikali yenyewe imefanya kosa ambalo hawakulijua la kumpaisha Lisu both kisiasa na as a person. Maana zile kauli za kutaka kufuta TLS mara kuwa Fulani asichaguliwe zilichochea wengi kutaka huyo mtu achaguliwe, and in the other hand kumpaisha jamaa. Hivyo Serikali bila kujua ilifanya kumpigia kampeni jamaa na akapeta kiulaini.
Hongera Lissu.
Lets call a spade a spade, not a big spoon.
sisi wanasheria huyo ndiye rais wetu. hao wengine...hahahahaha, vichekesho tu.
 
Hongera Lissu kwa ushindi mnono, I wish TLS ingekua na uwezo wa kufanya mabadiliko kwenye katiba ya TZ.
 
Kwenye muhimili wa mahakama TLS ndio stop engine kama hujui.
Bunge likitunga sheria za hovyo zinazokandamiza haki za raia, utu wa binadam n.k hawa jamaa ndio kwa kushirikiana na mahakama huichambua sheria husika na kuisaidia mahakama kutoa maelekezo ya ama uhalali au ubatili wa sheria husika (kwenye kesi)

Serikali nayo hupewa maelekezo mahakamani (nadhani wajua mawakili wa serikali walivyofokewa na jaji wa mahakama ya rufaa kanda ya AR kwa mizengwe yao)

Kumekucha sasa.
 
Hakina faida yoyote ile zaidi ya kupiga tararila tu.

Isingekuwa kubugi kwa Magu na Mwaky wake wala kisingepata hii kiki ya muda mfupi kiliyopata.
 
Hakina faida yoyote! Kinadai kipo kwa ajili ya kumtetea mtanzania kwa issue za kisheria. Cha ajabu kuna wakili anasota Kisongo kwa kesi ya kutakatisha pesa (ambayo ina dhamana).na kesi nyingi tu za watanzania zenye dhamana au kuhitaji msaada wa kisheria..sasa hapo pata picha mwanachama katelekezwa je wewe mwananchi wa kijijini Gezaulole kitakusaidia nini
Jambo lingine la aibu halikuweza hata peleka muwakilishi ktk bunge la katiba kujadili rasimu ya katiba...walishindwa na chama cha waganga wa kienyeji walipeleka muwakilishi.
Kwa mtazamo wangu naona akina manufaaa kipo kunufaisha viongozi kwa ada wanazokusanya toka kwa wanachama wote Tz(ofisi za uwakili)...na kula posho za makongamano na semina basii!
 
TLS moja kati ya faida yake - Ni kiboko ya SIZONJE au SHILAWADU au mkurupuko au mwakiwembe au Bashite baby!
 
Back
Top Bottom