Nape, wewe ni mbunge tu wa Mtama. Sio yule Nape msemaji wa CCM, wala Waziri wa habari, utamaduni na michezo

Dec 4, 2018
15
28
Nakusalimu Nape, salaam. Pole kwa misukosuko ya kwenye Chama chenu. Pole kamanda maana mpaka wakati huu wewe ni mbunge tu wa Mtama. Sio yule Nape msemaji wa CCM, wala Waziri wa habari, utamaduni na michezo.

Wenye kumbukumbu tunakumbuka ukiwa Waziri wa habari ulivyofungia magazeti tuliyoyapenda. Tunakumbuka ulivyokuwa msemaji wa CCM ulivyokuwa unawakejeli wapinzani kwa mbwembwe. Tunakumbuka juu ya goli lako la mkono juu ya maamuzi ya watanzania. Ulijisifia kufunga kwa mkono. Mwanzoni refa aliweka katikati, sasa kaenda kuangalia VAR karudisha mpira. Ni wa adhabu baada ya kugundua wahuni wachache mlishika mpira. Mnalalamika nini?

Huko nyuma mlikuwa untouchables. Leo mnavuna mlichopanda, mnataka tuvune wote kweli? Mlikula mkiwa kivulini, sisi tukiwa juani. Leo nanyi mnaonja jua eti mnataka tuwe wote, kweli? Oteni jua wenyewe sisi tulishazoea! Yaani mnaona mianya yenu ya kupata nafasi za uongozi inazibwa ndo mnajifanya wazalendo. Acheni mambo hayo bwana!

Mlitutahadharisha kubatizwa kwa moto, leo tuliotarajiwa kubatizwa tumeshaokoka, mmegeukiwa nyie baada ya mbatizaji kuwajua mlikuwa wapagani! Batizweni mjue ubatizo wa moto jinsi ulivyo. Ama kweli mwosha huoshwa!
 
Bwana Nape kipindi anatumbuliwa alipost Instagram hasa ile ishu ya kushikiwa Bastola.. nikamchana Pale.. kwamba wakati unafunga goli la mkono hukuwa unasikia raha na maneno kadha wa kadha pale.. mwamba akanifuata inbox.. anasema Hata Biblia inatuambia sameheni 7 mara 70.. kwahio tusameheeni!

Binafsi nadhani Nape na wenzie wanastahili dawa zaidi ya hii!

Power is not Permenent!
 
Nakusalimu Nape, salaam. Pole kwa misukosuko ya kwenye Chama chenu. Pole kamanda maana mpaka wakati huu wewe ni mbunge tu wa Mtama. Sio yule Nape msemaji wa CCM, wala Waziri wa habari, utamaduni na michezo.

Wenye kumbukumbu tunakumbuka ukiwa Waziri wa habari ulivyofungia magazeti tuliyoyapenda. Tunakumbuka ulivyokuwa msemaji wa CCM ulivyokuwa unawakejeli wapinzani kwa mbwembwe. Tunakumbuka juu ya goli lako la mkono juu ya maamuzi ya watanzania. Ulijisifia kufunga kwa mkono. Mwanzoni refa aliweka katikati, sasa kaenda kuangalia VAR karudisha mpira. Ni wa adhabu baada ya kugundua wahuni wachache mlishika mpira. Mnalalamika nini?

Huko nyuma mlikuwa untouchables. Leo mnavuna mlichopanda, mnataka tuvune wote kweli? Mlikula mkiwa kivulini, sisi tukiwa juani. Leo nanyi mnaonja jua eti mnataka tuwe wote, kweli? Oteni jua wenyewe sisi tulishazoea! Yaani mnaona mianya yenu ya kupata nafasi za uongozi inazibwa ndo mnajifanya wazalendo. Acheni mambo hayo bwana!

Mlitutahadharisha kubatizwa kwa moto, leo tuliotarajiwa kubatizwa tumeshaokoka, mmegeukiwa nyie baada ya mbatizaji kuwajua mlikuwa wapagani! Batizweni mjue ubatizo wa moto jinsi ulivyo. Ama kweli mwosha huoshwa!
na nyinyi zamu yenu ya kulia juani ni lini
 
Karma ikimaliza chini itahamia juu,hadi wote wakili Ubaya haulipi.
 
Nasubiri kuona atakaye mbatiza Magufuli kwa Moto. Eeh Mungu naomba maisha marefu niione siku ambayo Magufuli atabatizwa kwa moto. Amen
 
Nakusalimu Nape, salaam. Pole kwa misukosuko ya kwenye Chama chenu. Pole kamanda maana mpaka wakati huu wewe ni mbunge tu wa Mtama. Sio yule Nape msemaji wa CCM, wala Waziri wa habari, utamaduni na michezo.

Wenye kumbukumbu tunakumbuka ukiwa Waziri wa habari ulivyofungia magazeti tuliyoyapenda. Tunakumbuka ulivyokuwa msemaji wa CCM ulivyokuwa unawakejeli wapinzani kwa mbwembwe. Tunakumbuka juu ya goli lako la mkono juu ya maamuzi ya watanzania. Ulijisifia kufunga kwa mkono. Mwanzoni refa aliweka katikati, sasa kaenda kuangalia VAR karudisha mpira. Ni wa adhabu baada ya kugundua wahuni wachache mlishika mpira. Mnalalamika nini?

Huko nyuma mlikuwa untouchables. Leo mnavuna mlichopanda, mnataka tuvune wote kweli? Mlikula mkiwa kivulini, sisi tukiwa juani. Leo nanyi mnaonja jua eti mnataka tuwe wote, kweli? Oteni jua wenyewe sisi tulishazoea! Yaani mnaona mianya yenu ya kupata nafasi za uongozi inazibwa ndo mnajifanya wazalendo. Acheni mambo hayo bwana!

Mlitutahadharisha kubatizwa kwa moto, leo tuliotarajiwa kubatizwa tumeshaokoka, mmegeukiwa nyie baada ya mbatizaji kuwajua mlikuwa wapagani! Batizweni mjue ubatizo wa moto jinsi ulivyo. Ama kweli mwosha huoshwa!
Nakumbuka huyu jamaa alivyokua ana mkejeli Dr.Slaa na kumuita Babu😀 leo Slaa yuko zake ng'ambo anakula mema ya dunia,Nape kabaki Mtama anapauka kwa vumbi la ufuta na korosho😀😀😀
 
Back
Top Bottom