NAPE: Watu wameshindwa kujitokeza kupiga kura wakiohofia kumwagiwa Tindikali

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,768
894
Katibu wa Itikatdi na Uenezi wa CCM.
Nape, kaongea kwenye taarifa ya habari TBC1, anasema sababu iliofanya watu wachache kujitokeza kupiga kura kwenye jimbo la Igunga, watu walihofiwa kumwagiwa Tindikali.

SOURCE: TBC1 HABARI
 
Wengi Niliwahiji Wameogopa kupiga kura sababu hakukuwa na Mwislamu wa kuchagua kuwa Mbunge

Nape hakuwa Igunga alikuwa anaranda randa Singida, Mwanza, Arusha na kwingineko
 
Nani wa kuwamwagia tindikali na kuwapiga mapanga zaidi ya kikosi cha green guards? Nape anaji- contradict mwenyewe.
 
Japo HITLER alikua ni racist lakini ninauhakika angempa Nape nafasi kwny kitengo cha propaganda....
 
Nadhani kuna ukweli kwenye madai yake. Unajua watu wa vijijini ni waoga sana. Kitendo cha Magwanda kwenda na mapanga kiliwafanya wanyong'onyee na waogope sana.
 
Chuki binafsi hazijengi...wana cdm tukae tujipange na tuje na majibu, huyo nape mnaemzozoa anaeza kuamua kujiunga cdm siku moja mkaumbuka
 
Wengi Niliwahiji Wameogopa kupiga kura sababu hakukuwa na Mwislamu wa kuchagua kuwa Mbunge

Nape hakuwa Igunga alikuwa anaranda randa Singida, Mwanza, Arusha na kwingineko

Arusha hawezi kanyaga masaburi huyo. Akithubutu watampenda fastafasta.
Nimemsikia akitamka maneno hayo nikabaki mdomo wazi.
 
ninakubaliana na wewe kwa asilimia 90 mkuu,huenda ile sumu ya masheikh imewaathiri wana igunga na kuona bora wasipige kura...
 
Yaani huyu bwana mdogo siku za hivi karibuni amekuwa na kiherehere kibaya. Anaropoka hovyo hovyo, hajui maadili ya uongozi, Sijui anatafuta sifa?
JF ituruhusu kutumia lugha kali kidogo tutoe hasira zetu!
 
Nchi hii ukitaka kuwa msemaji wa ccm lazima uwe bingwa wa kutuma ujumbe wa kuudhi.
 
Kafanya utafiti?

Huyo kijana mbona hajajiuliza kwanini uchaguzi mkuu uliopita wapiga kura walikuwa kidogo au kulikuwapo na Tindikali?

Je mwandishi aliyekuwa anamuhoji ameridhika na jibu hilo? Lakini hata waandishi wetu saa nyingine unaweza kusema bora watoto wa shule!

Je kaongelea shahada zao kukusanywa na watu flani?
 
Nadhani kuna ukweli kwenye madai yake. Unajua watu wa vijijini ni waoga sana. Kitendo cha Magwanda kwenda na mapanga kiliwafanya wanyong'onyee na waogope sana.

Una uhakika?! Mbona huko kwenu Mara mapanga ni jambo la kawaida tu!? Husipende kugeneralise mambo kilayman!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom