MBUTAIYO
JF-Expert Member
- Nov 15, 2010
- 683
- 393
Hongera mkuu kwa ufafanuzi, hapa inatosha.U-wenye heri wa Mzee Nyerere ndugu Nape siyo mambo ya siasa ,ili apete hilo daraja inabidi factsheet ijae mambo ya kumpendeza mungu kiukristo siyo hayo uliyoyataja eti ya uadirifu ndani ya chama.Kwa hili wewe kwa mjibi wa kanisa katoliki umeonyesha ni mbumbu kabisa kabisa. Katika huu mchakato wa kupelekea Mzee Nyerere atangazwe ni mwenye heri (bado hajatangazwa) kanisa katoriki (papacy) huko kwa papa wanasubiri sasa mashuhuda washuhudie muujiza mmoja ambao candidate ameufanya , na muujiza huo utatangazwa dunia nzima wajue na wauhakikishe. Nachopenda kukufahamisha Ndugu Nape ni kwamba suala la kumtangaza Mzee Nyerere mwenye heri siyo la chama cha CCM au Kardrinari pengo bali ni la Baba mtakatifu baada ya kupata ushuhuda wa muujiza toka hapa tz au kwingineko.
Hata hivyo Ndugu NAPE Mzee Nyerere anakabiliwa na vikwazo vikubwa vitatu ambavyo kwa mjibu wa canon law vinaweza kumkwamisha kufikia daraja hilo:-
1. Katika wadhifa wake wa urais aliidhinisha kisheria death sentence mbili, ya yule mhindi na ya Mwamwindi yule mhehe aliyemmua Dr, Kreruu.( hii ni kinyume na sheria no 6 ya Mussa alizopewa na mungu).
2. Pia katika maisha yake aliidhinisha vita kati ya tz na uganda, mambo haya huwa hayampendezi mungu,
3. Kumwachia Cassim Hanga kwenda Zanzibar pia inaweza kuwa ni kikwazo,alichotakiwa kufanya ni kumbakiza
hukuhuku bara, kwa kweri huyu jamaa yaliyoenda kumkuta kula zenj Mzee Nyerere hawezi kukosa kuwajibika
mbele ya mungu.
Ninakuambia haya kama Mroma niliyebobea, tutakufa wote hata wale waliozariwa leo Nyerere hajapata daraja la uwenyeheri, Pia ninakukanya Nape usiseme mambo usiyoyajua vizuri;
Huwa tunamalizia na TUMSIFU YESU KRISTO.
Nape analeta propaganda kwenye mambo ya dini!