Nape: Wapinzani wachukue watuhumiwa ufisadi CCM

Chiume

Member
Apr 8, 2012
48
18
Nimeipenda hiii

Nape: Wapinzani wachukue watuhumiwa ufisadi CCM
Send to a friend
Tuesday, 26 April 2011 21:02
0diggsdigg

Ramadhan Semtawa
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, amesema chama hicho hakitishwi na uwezekano wa vyama vya upinzani kuwachukua makada wake inaotaka kuwatema kwa tuhuma za ufisadi.Msimamo wa Nnauye unakuja kipindi ambacho mpango mkakati huo wa CCM kujivua gamba, ukiwa umeibua mjadala mzito ndani na nje ya chama hicho tawala.

Akizungumza katika kipindi maalumu kilichorushwa na TBC Taifa jana, Nnauye alisema anatangaza zabuni ya bure kwa wapinzani kuwachukua watuhumiwa hao wa ufisadi.

Nnauye ambaye alikuwa akijibu swali kwamba, haoni uamuzi huo wa chama kutema makada wake hao unaweza kuwafanya wakimbilie upinzani, huku akisisitiza: "Tena wakifanya hivyo watakuwa wametusaidia."

Mwanasiasa huyo machachari alifafanua kwamba, CCM ni chama kitukufu kilichojengwa juu ya misingi ya maadili na Baba wa Taifa, marehemu Mwalimu Julius Nyerere, hivyo hakitakumbatia watu wasiokuwa na maadili.

"Ndio maana leo hii kanisa linataka kumfanya Mwalimu Nyerere kuwa mwenye heri, linajua amefanya mambo mengi mazuri. Mwalimu alijenga misingi ya uadilifu ndani ya chama, sasa leo hii watu wasio waadilifu hawawezi kuwa na nafasi,” alisema Nnauye.

Alionyesha tambo akisema: "samaki ana nguvu akiwa ndani ya maji, lakini akishatoka nje hana nguvu. Kwa hiyo hata hawa wanadhani wana nguvu kwa sababu wako ndani ya chama, tukishawatoa mtaona."

Kujivua gamba kwenye jumuiya
Nnauye mwana wa kada maarufu wa CCM marehemu Brigedia Jenerali Moses Nnnauye, alisema mchakato wa kujivua gamba hautaishia hapo, kwani ni sawa na kuoga mtu anapaswa kuoga mwili mzima.

Aliweka bayana kwamba, mtu anapooga hugusa viungo mbalimbali ikiwamo mikono na kichwa na kusisitiza: "yapo maamuzi mengi tu tutachukua ikiwamo kugusa jumuiya."

Akitoa mfano, alisema vijana ambao ni karibu asilimia 75 ya wapiga kura wanapaswa kuwekewa mikakati ili waweze kuvutiwa na chama na kama hali ni tofauti, itapaswa kuangaliwa sababu za msingi.

Aliongeza kwamba katika mchakato huo wa kujivua gamba, chama kitashuka ngazi kwa ngazi na hatua kwa hatua hadi kuhakikisha kinarejea katika misingi yake iliyoachwa na waasisi wake.

Kuhusu ukuu wa wilaya
Nnauye ambaye amefanya kazi hiyo kwa miezi minane tangu kuteuliwa, alisema anatarajia kukabidhi ofisi wiki ijayo ili aweze kukijenga chama na kukitumikia vizuri.

Alisema hivi sasa watu waliopo kwenye sekretarieti wanapaswa kukitumikia chama peke yake, hata wengine wenye nyadhifa zao watapaswa kuziachia.
 
kUNA UJUMBE MZITO PALE

ITAKUWA NGUMU SANA KUPIGA VITA UFISADI HUKU UMEKUBALI EL KUWA MWANACHAMA WAKO
 
kUNA UJUMBE MZITO PALE

ITAKUWA NGUMU SANA KUPIGA VITA UFISADI HUKU UMEKUBALI EL KUWA MWANACHAMA WAKO

Mkuu mi nadhani hao wanakuja CDM ili kuwakomoa CCM na wanajua kabisa hawatapewa kipao mbele,wao ni kama wanachama wa kawaida tu
 
Nape,

Kama hao jamaa wanaoondoka CCM unawaona ni mafisadi,ya nini kuendelea kuwazungumzia?
Halafu kwa mtazamo wa chama chako, ufisadi nini hasa?Elewa tu kila mmoja ana tafsiri ya hii dhana.Usishangae wapo watu wanakuona nawe ni mmoja wa mafisadi.

Utawala wa sheria unaelekeza mahakama pekee ndiyo ina jukumu la kushughulikia watu wenye matatazo ya kimaadili...Nanyi kama kweli mnadhani hawa wanaowakimbia ni mafisadi kwa nini msiwapeleke mahakamani?
Kila mara unahangaika na CHADEMA,kwani wao ndio walio kuajiri?

Kazi yako kuu ni kueneza itikadi ya chama chako.
Dalili zinaonyesha huifanyi vyema hiyo kazi...sasa kwa nini unajiongezea kazi kueneza masuala ya CDM tena kwa namna ya kupotosha?
 
U-wenye heri wa Mzee Nyerere ndugu Nape siyo mambo ya siasa ,ili apete hilo daraja inabidi factsheet ijae mambo ya kumpendeza mungu kiukristo siyo hayo uliyoyataja eti ya uadirifu ndani ya chama.Kwa hili wewe kwa mjibi wa kanisa katoliki umeonyesha ni mbumbu kabisa kabisa.

Katika huu mchakato wa kupelekea Mzee Nyerere atangazwe ni mwenye heri (bado hajatangazwa) kanisa katoriki (papacy) huko kwa papa wanasubiri sasa mashuhuda washuhudie muujiza mmoja ambao candidate ameufanya , na muujiza huo utatangazwa dunia nzima wajue na wauhakikishe.

Nachopenda kukufahamisha Ndugu Nape ni kwamba suala la kumtangaza Mzee Nyerere mwenye heri siyo la chama cha CCM au Kardrinari pengo bali ni la Baba mtakatifu baada ya kupata ushuhuda wa muujiza toka hapa tz au kwingineko.

Hata hivyo Ndugu NAPE Mzee Nyerere anakabiliwa na vikwazo vikubwa vitatu ambavyo kwa mjibu wa canon law vinaweza kumkwamisha kufikia daraja hilo:-

1. Katika wadhifa wake wa urais aliidhinisha kisheria death sentence mbili, ya yule mhindi na ya Mwamwindi yule mhehe aliyemmua Dr, Kreruu.( hii ni kinyume na sheria no 6 ya Mussa alizopewa na mungu).

2. Pia katika maisha yake aliidhinisha vita kati ya tz na uganda, mambo haya huwa hayampendezi mungu,

3. Kumwachia Cassim Hanga kwenda Zanzibar pia inaweza kuwa ni kikwazo,alichotakiwa kufanya ni kumbakiza
hukuhuku bara, kwa kweri huyu jamaa yaliyoenda kumkuta kula zenj Mzee Nyerere hawezi kukosa kuwajibika
mbele ya mungu.

Ninakuambia haya kama Mroma niliyebobea, tutakufa wote hata wale waliozariwa leo Nyerere hajapata daraja la uwenyeheri, Pia ninakukanya Nape usiseme mambo usiyoyajua vizuri;

Huwa tunamalizia na TUMSIFU YESU KRISTO.
 
Mnachokifanya Nape ni kulainisha magamba kwa maji ya moto na magamba kujinyonyoa yenyewe. Hilo ni tofauti kabisa na dhana nzima ya kuvua magamba kitendo ambacho kinatakiwa kuashiria damu. Hata hivyo wakimbilie wapi kama sio kule ambako bakuli la Matonya liko wazi masaa 24?
 
Nape,
iUtawala wa sheria unaelekeza mahakama pekee ndiyo ina jukumu la kushughulikia watu wenye matatazo ya kimaadili...Nanyi kama kweli mnadhani hawa wanaowakimbia ni mafisadi kwa nini msiwapeleke mahakamani?
Kila mara unahangaika na CHADEMA,kwani wao ndio walio kuajiri?
Kazi yako kuu ni kueneza itikadi ya chama chako.
Dalili zinaonyesha huifanyi vyema hiyo kazi...sasa kwa nini unajiongezea kazi kueneza masuala ya CDM tena kwa namna ya kupotosha?
Fisadi manake ni mtu anaesema uongo, malaya mwizi, mla rushwa, mbinafsi, mwenye wifu anaejipatia mali kwa njoa ya uongo n.k je nape anavyo mwita mellya ni gamba? mbona ss wtz hatuoni gamba lake? nape kweli ni vuvuzela hana jipya la kusema. maneno ya mkosaji hayoooo!!!
 
hata wewe mpayukaji mbayuwayu iko siku utakimbia uliko.mbona ulianzisha ccj,nani hakujui fedhuli wee
 
Huyu Vuvuzela la magamba na wenzake wanajua tafsiri halisi ya fisadi? au ndiyo kusema wame pindua/kugeuza maana manake kwao kweli ni hapana, na hapana ndiyo kweli. Anapo taka kutuaminisha kuwa Millya ni gamba tumueleweje? mbona mpaka sasa hana kashfa iliyowazi? Kumbe mtu akihama kutoka magamba vyovyote vile ana qualify kuwa gamba kwa mujibu wao eh?

Kesho Mh.Filikujombe akihama wataanza kumuita gamba. Huyu jamaa amekuwa na fikra tofauti kabisa na magamba wengine. Je naye ana kashfa? lakini akihama tu utasikia "amejivua gamba" Labda kama itakuwa ni kwa kuachana na chama kilijcho jaa uovu.

Jambo jingine kuhusu Filikujombe ni kwamba amekuwa mbunge wa kwanza wa magamba jasiri aliyeweza kukosoa ziara za vasco da gama nje ya nchi. Sasa mtu huyu akihama mkaanza kumuita gamba itabidi turejee tafsiri halisi ya "gamba"
 
The same old stories, too many words too little action. Kila atakayeondoka watamwita fisadi. CCM ingekuwa meli, tungeita MAY DAY.
 
Back
Top Bottom