Nape: Wapinzani wachukue watuhumiwa ufisadi CCM

fangfangjt

JF-Expert Member
Apr 25, 2008
571
139
SOURCE : Nape: Wapinzani wachukue watuhumiwa ufisadi CCM


Ramadhan Semtawa
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, amesema chama hicho hakitishwi na uwezekano wa vyama vya upinzani kuwachukua makada wake inaotaka kuwatema kwa tuhuma za ufisadi.Msimamo wa Nnauye unakuja kipindi ambacho mpango mkakati huo wa CCM kujivua gamba, ukiwa umeibua mjadala mzito ndani na nje ya chama hicho tawala.

Akizungumza katika kipindi maalumu kilichorushwa na TBC Taifa jana, Nnauye alisema anatangaza zabuni ya bure kwa wapinzani kuwachukua watuhumiwa hao wa ufisadi.

Nnauye ambaye alikuwa akijibu swali kwamba, haoni uamuzi huo wa chama kutema makada wake hao unaweza kuwafanya wakimbilie upinzani, huku akisisitiza: "Tena wakifanya hivyo watakuwa wametusaidia."

Mwanasiasa huyo machachari alifafanua kwamba, CCM ni chama kitukufu kilichojengwa juu ya misingi ya maadili na Baba wa Taifa, marehemu Mwalimu Julius Nyerere, hivyo hakitakumbatia watu wasiokuwa na maadili.

"Ndio maana leo hii kanisa linataka kumfanya Mwalimu Nyerere kuwa mwenye heri, linajua amefanya mambo mengi mazuri. Mwalimu alijenga misingi ya uadilifu ndani ya chama, sasa leo hii watu wasio waadilifu hawawezi kuwa na nafasi,” alisema Nnauye.

Alionyesha tambo akisema: "samaki ana nguvu akiwa ndani ya maji, lakini akishatoka nje hana nguvu. Kwa hiyo hata hawa wanadhani wana nguvu kwa sababu wako ndani ya chama, tukishawatoa mtaona."

Kujivua gamba kwenye jumuiya
Nnauye mwana wa kada maarufu wa CCM marehemu Brigedia Jenerali Moses Nnnauye, alisema mchakato wa kujivua gamba hautaishia hapo, kwani ni sawa na kuoga mtu anapaswa kuoga mwili mzima.

Aliweka bayana kwamba, mtu anapooga hugusa viungo mbalimbali ikiwamo mikono na kichwa na kusisitiza: "yapo maamuzi mengi tu tutachukua ikiwamo kugusa jumuiya."

Akitoa mfano, alisema vijana ambao ni karibu asilimia 75 ya wapiga kura wanapaswa kuwekewa mikakati ili waweze kuvutiwa na chama na kama hali ni tofauti, itapaswa kuangaliwa sababu za msingi.

Aliongeza kwamba katika mchakato huo wa kujivua gamba, chama kitashuka ngazi kwa ngazi na hatua kwa hatua hadi kuhakikisha kinarejea katika misingi yake iliyoachwa na waasisi wake.

Kuhusu ukuu wa wilaya
Nnauye ambaye amefanya kazi hiyo kwa miezi minane tangu kuteuliwa, alisema anatarajia kukabidhi ofisi wiki ijayo ili aweze kukijenga chama na kukitumikia vizuri.

Alisema hivi sasa watu waliopo kwenye sekretarieti wanapaswa kukitumikia chama peke yake, hata wengine wenye nyadhifa zao watapaswa kuziachia.
 
Kina nani hao mafisadi mbona huwataji ndugu yangu Nape au una maana ya Chiligati maana na yeye ametajwa kuwa ni fisadi, wataje tuwajue mwisho unakuwa kama tarumbeta tu.
 
Nape anaongea sana, too much too much......... too much

Nape umekua domokaya sasa, tulia ufanye kazi unatia aibu na kero sasa
 
Mara nyingi Wanaosema sana huwa si watendaji wazuri inonekana Nape ni mmoja wao kama kweli anajua alisemalo basi atoe orodha kamili ya hao Mafisadi ambao wanatakiwa kuondoka ili kesho tuseme walitajwa na hawakuondoka sio kubwabwaja tu..
 
Unajua nape anafurahisha.......he is a comedian,wenzie wanataja yeye hawataj,sasa anaemvulagiza nani,mi nimechoka kunsikia kwenye media ,sasa amekua msemaj wa rais na si mweneza itikad za chama,maana leo amezungumzia mali za jk,kazi ya vizabizabina akina salva ndo anaifanya yeye
 
Nape nafanya kazi aliyopewa na JK! Hajafanya kosa, sifa ya mwanasiasa ni kuongea sana! CCM imepata msemaji anaenda na wakati huu
 
Tuishi kwa matumaini kama wale wagonjwa wa ........tumpe muda kijana inawezekana ana jambo mfukoni mwako. Mbona akina Zitto, Mnyika na wengineo wanaongea lakini hatujawachoka? Matokeo ya kauli za Nape hatuwezi kuyaona kwa wiki moja, inawezeka hivi sasa Nape anaongea sana ili kutuma ujumbe kwa mafisadi wajiondoe wenyewe kisha wasipofanya hivyo vitafuata vitendo.

Kwa baadhi ya watendaji baada ya maneno ni vitendo.
 
Mara nyingi Wanaosema sana huwa si watendaji wazuri inonekana Nape ni mmoja wao kama kweli anajua alisemalo basi atoe orodha kamili ya hao Mafisadi ambao wanatakiwa kuondoka ili kesho tuseme walitajwa na hawakuondoka sio kubwabwaja tu..
Hajawataja kwa majina kwa vile ameweka akiba............... Kwa yeyote atakayehamia upinzani atakuwa ndiye FISADI
 
watahamiaje upinzani hao mafisadi wkt ni mashareholder kwa NNJI HII YA WADANGANYIKA? SIGNATURE ZAO MTAZIONA KWENYE MIKATABA FEKI NA MAMBO YOOTE YA MAGUMASHI MAKUBWAMAKUBWA,TAHETEHETEHEEE
 
Nape nafanya kazi aliyopewa na JK! Hajafanya kosa, sifa ya mwanasiasa ni kuongea sana! CCM imepata msemaji anaenda na wakati huu


Hakika umenena, bwana mdogo Nape yuko kwenye siasa za kisasa, Jamii ikimuuliza swali linajibiwa papo hapo sio mpaka kikao cha chama kitakapokaa. Wengi tumeshuhudia madhara ya kukumbatia taarifa kwa upande wa CCM huku wenzao wa Chadema wakizunguka kuzungumza kila siku.

Media zimejaa Chadema kila pembe pengine Nape atasaidia CCM ikasikika kwa upande wa pili na kisha sisi wananchi tukalinganisha uzito na mantiki ya taarifa za vyama vyote viwili.
 
Siasa za ushindani zimerudi..anafanya kazi ya siasa, cdm imeongea muda mrefu sasa kada kawekwa kuzungumza full time for ccm..its just politics as usual...ukimya umeumiza chama cha baba wa taifa ccm..
Good job nape, endelea na kazi aliyofanya baba yako brig. Nnauye
 
hapa CCM lazima imeguke makundimakundi hv kujivua gamba kunaongeza kumeguka kwa chama!
 
CDM sidhani kama wana shida ya rasilimali watu,wazalendo waliomo na wanaoendelea kujiunga wanatosha,hakuna haja ya kuingiza watu wenye kutilia shaka,ambao wataongeza kazi ya kuchunguza mienendo yao siku hadi siku.hao mafisadi wapumzike tu hawana nafasi tena
 
CDM Ingepunguza kunyooshea vidole Mafisadi kama Agenda na kuanza kujenga Matawi Hadi Vijijini, Katani kuingiza Wanachama..Kutegemea Magazeti katika miji hakuwezi kukuza Wigo la wapiga kura Uchaguzi Ujao..Agenda ya Mafisadi ikiisha usishangae wakipata kura chache na Majimbo Machache 2015..SERA ZA UCHUMI, KUJENGA CHAMA KUTOKA NGAZI YA KAYA/NYUMBA KUMI NDIO NJIA PEKEE KUINGOA CCM OTHERWISE, NIMETOKA KIJIJINI NAPE ANAZUNGUMZWA VIZURI HATA NA MADIWANI WA CDM KANDA YA ZIWA..RUZUKU IFIKE CHINI OTHERWISE UKOMBOZI USIWE MBIO ZA SAKAFUNI
 
dalili za mtu mwenye I/Q ndogo ni kama za Nape ,si mtu wa kufikiri ila ni mropokaji ,hawa ndio wanatakiwa na CCM ya kisasa .
Itikadi sio kuwatoa mafisadi ,maana hao ndio wamekifikisha chama kilipo kwa wizi wa kura na mambo kama hayo ...Bila lowasa na siasa za maji taka leo JK angekua raisi ???acheni unafiki nyie ...Bila rostam team ya kampeni ingekamilika 2005 ,Jk alikua na hela za kuhonga azitoe wapi?? bila ya organizasheni ya Mamvi ...tuache huu ni unafiki na sie wajuvi tunajua ..kua ni unafiki !eti wananchi wanaona kua chama kinakumbatia mafisadi ,kwani Jk hana utashi ???huu ni ujinga mtupu ...Ndio kawaida ya nchi maskini lakini ...watu ambao
 
Sidhani kama Rostam, Lowasa, Chenge, na Karamagi wanaweza pokelewa Chadema. Sidhani kama wanaweza kuwa na ''GUTS'' za kuomba uanachama Chadema, ni kitu ambacho hakiwezekani.
So Mr Nape usiogope Chedema kupata nguvu ya mafisadi kuchukua Dola, Ninajua huo ndio uoga wako, Si unajua tena Tanzania ukiwa na Pesa za Kofia na T-shirts unajichukulia Nch kilainiii!!
 
nape anachefua kuliko makamba acheni aendelee kuropoka maana ataimalizia ccm iliyo vipandevipande
 
Nape asisahau kuwa siasa is a matter of mass manipulation..
Hivyo hao anaowatuhumu kuwa mafisadi, wakipata Ma-lobbyist wazuri wanaweza kurudi kwenye chati nzuri kumshinda yeyote pale..
Wakumbuke chezo lililowahi kuchezwa kati ya Zuma na Mbeki labda kuna watakalojifunza pale...

Shauri yao!
 
Back
Top Bottom