Nape waache wazee na viongozi wastaafu waikosoe serikali hata kama wao hawakutenda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape waache wazee na viongozi wastaafu waikosoe serikali hata kama wao hawakutenda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gosbertgoodluck, Mar 24, 2012.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu,

  Kuna tabia imeanza kujengeka miongoni mwa wanasiasa hususan wa aina ya Nape kutaka kuwazuia wazee na viongozi wastaafu kutoa maoni yao kuhusui mwenendo wa serikali katika kushughulikia masuala mbalimbali ya kisiasa, kijamii na kiuchumi. Hivi karibuni, Nape ameamua kumjibu Mhe. Lowassa kuhusu kauli yake ya mara kwa mara ya kuikumbusha Serikali kuhusu umuhimu wa kuwa na mkakati maalum wa kushughulikia ajira kwa vijana na kwamba kadri Serikali inavyozidi kuwaacha vijana wamezagaa mitaani bila kazi au ajira, ndivyo Serikali inavyozidi kutengeneza bomu litakalokuja kulipuka baadaye. Hali hii pia imewahi kumkumba Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Frederick Sumaye. Kuna maoni fulani alitoa lakini alijibiwa na kiongozi mmoja wa umoja wa vijana wa ccm kuwa yeye wakati wa uongozi wake alifanya nini.

  Kwa nchi inayoheshimu uhuru wa kutoa mawazo, sioni kama hilo ni tatizo. Hata kama Lowassa alikuwa Serikalini na hakushughulikia suala la ajira kwa vijana kwa namna anavyoongea sasa, je, hiyo immnyime uhuru wa kusema ili Serikali au viongozi waliopo sasa nao wasisahau! Je, kama Mzee Mkapa kuna jambo ambalo kwa masusudi au bahati mbaya hakushughulikia wakati wa utawala wake na sasa analiona kwa ukaribu zaidi na umuhimu wake kwa ustawi wa nchi, je akae kimya asiishauri Serikali!!! Upuuzi gani huu!!

  Tabia hii ya kuwashona mdomo viongozi wasiongee na kuikosoa Serikali yao ni udikteta wa hali ya juu uliopitiliza. Viongozi wastaafu ni hazina muhimu na haswa nchi inapokumbana na changamoto mbalimbali za kiuongozi kama wakati huu wa uongozi uliopwaya wa kikwete. Ndiyo maana wengi wao bado wanaendela kulipwa mafao au marupurupu manono yanayotokana na kodi ya wananchi.

  Kwa mantiki hiyo, namshauri Nape aache siasa zake za majitaka kuwazuia viongozi wetu wastaafu watamke wanachoona kinafaa kwa ustawi wa nchi yake. Anachotakiwa Nape ni kuishauri Serikali ya chama chake kueleza hali halisi na kutoa takwimu zinazojibu hoja iliyotolewa na Mhe. Lowassa na siyo kuwaita waandishi wa habari na kuanza kubwabwaja maneno yasiyo na mbele wala nyuma.
   
 2. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  nakubaliana na wewe 100%
   
 3. k

  kaka miye Senior Member

  #3
  Mar 24, 2012
  Joined: Sep 25, 2011
  Messages: 157
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  ukweli mtupu mwambie ajue kuwa wao nao ni raia wana uhuru wa kutoa maoni yao
   
 4. Keen

  Keen JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 620
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Imetulia!!!
   
 5. H

  Honey K JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Gosbert,
  Kwanza haya ni mawazo yako na tafisiri yako binafsi! Sijawahi kuwaza wala kutamani kuwanyamazisha wazee au wastaafu na hata vijana, kwani mie ni muumini wa uhuru wa kutoa mawazo!

  Katika majibu yangu kwa mwandishi wa Mwananchi ambae alitaka kujua msimamo wangu baada ya majibu ya serikali kwa swala la ajira nilisema yafuatayo.....
  Sasa inawezekana kabisa kwa tafisiri yako haya maneno yanaziba midomo ya wazee wastaafu....

  SINA NIA HIYO, SIO MUUMINI WA HILO.
   
 6. H

  Honey K JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hasa kwenye red,

  HIVI NI WAPI NIMEITA WAANDISHI NA KUBWABWAJA KAMA UNAVYODAI?? UNAPOKARIRI KUMTUKANA TU NAPE POPOTE UNAPOTEZA MWELEKEO! SIJAWAHI KUITA WAANDISHI WA HABARI KWA HILO, ACHA KUDANGANYA WATU HAPA NI AIBU KUSEMA UONGO MTU MZIMA.....
   
 7. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Nape sasa umekuwa mwanasiasa zaidi na huongei hali halisi ya watanzania hasa vijana waliopo mitaani. Lowassa hajasema vijana wasio na ajira ni mabomu bali kuwepo na vijana wengi wasio na ajira ni bomu ambalo litakuja lipuka baadae. Tofautisha hii, hakuwaita wao bomu (noun) bali tendo la kuwa unemployed youth ni bomu (verb) na hilo ni ukweli.

  Unataka takwimu kujua hili!!? Siamini kama akili yako ni MGANDO kiasi hiki kama ya yule mama Kabaka... Anaelinganisha sijui 75% ya Singida na 25% ya Dsm!!

  Oneni ukweli na muufanyie kazi ndio mtaweza washawishi watu na wataamini chama chenu, lakini kudanganya danganya mnazidi poteza credibility mbele ya watanzania vijana ambao angalau mmewapa uwezo wa kuelewa baada ya kuwaanzishia shule za kata.
   
 8. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #8
  Mar 24, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Gwanda gamba!!

  [​IMG]
   
 9. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Nape, natambua uzito wa nafasi uliyonayo na umuhimu wake katika maendeleo ya jamii yetu. Maswali yangu ni JE? Ni namna gani unashauriwa Kabla ya kukabiliana na Changamoto za wadhifa wako? Washauri wako wanapatikanaje? Maswali yangu yanatokana na ukweli kwamba wewe binafsi huna uwezo wa kutathmini na hatimae kuwa na mwelekeo wa kimawazo wa jibu la Changamoto nyingi ziananazo kukabili katika kazi yako.
   
 10. P

  Pius Kafefa Member

  #10
  Mar 24, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Ndugu Nape,

  Nafahamu kwamba wewe ni mjamaa kwa matendo na kauli zako. Naomba usisite kusema ukweli pale unatapotakiwa kutokana na nafasi yako. Tunajua kwamba matatizo ya nchi yetu yanafungamana na namna viongozi wetu wanavyofanya maamuzi katika kutekeleza majukumu yao. Mfano ni kashfa ya Richmond/Dowans iliyopelekea taifa kukumbwa na aibu pamoja na hasara ya mabilioni. Hivi leo tungekuwa na umeme wa kutosheleza mahitaji yetuni Watanzania na wageni wangapi wangewekeza kwenye viwanda? Uwekezaji huo ungeibua ajira ngapi?

  Tuache malumbano, binafsi sikubaliani na hoja za Waziri kabaka, ukosefu wa ajira ni tatizo. Kasi ya kulishulikia ni ndogo zaidi kwa sababu ya matatizo ya kimfumo yalichangiwa na viongozi watangulizi, hasa walipoamua kuhalalisha rushwa na ujanja ujanja katika kutekeleza miradi ya serikali. Kama tumeshindwa kuwavua gamba kwa njia ya moja kwa moja lazima tutumie mtindo wa kuwakumbusha makosa yao. Sisi watoto wa wakulima tunaelewa maana ya ukosefu wa ajira. Sidhani kama watoto wa wakubwa wanachagua kuwa watumishi wa serikali! Wanafanya kazi kwenye taasisi zenye mishahara mizuri na pengine wamewezeshwa kujiajiri wenyewe.
   
 11. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,397
  Trophy Points: 280
  nape unakubali kuna tatizo la ajira tanzania au hapana?au ajira ni vijana kuuza vocha na line,bidhaa za mchina barabara
   
 12. H

  Honey K JF-Expert Member

  #12
  Mar 24, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sasa unakuja mahali penyewe penye mzizi wa tatizo. Sasa jiulize leo ikitokea analiyeongeza tatizo la umeme nchini kwa kushindwa kusimamia upatikanaji wa umeme wa uhakika basi hata huo mdogo tukaingia kwenye tatizo la malipo ya Richmond na baadae Dowans, pamoja na athari tulizozipata za uwekezaji, analaumu tatizo la ajira!!!!!!!!!

   
 13. H

  Honey K JF-Expert Member

  #13
  Mar 24, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Bahati mbaya au nzuri kipimo cha uwezo wa akili yangu ulichotumia hakitumiwi na wenye akili zao....kwahiyo litabaki dua la kuku tu   
 14. H

  Honey K JF-Expert Member

  #14
  Mar 24, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tatizo la ajira lipo na si dogo na wala halipo Tanzania pekeake, lipo dunia nzima. Lakini si la kiliita bomu na wanaolalamikia.....mwalimu alitwambia ukikataa rushwa kwa maneno basi hata sura ifanane na kukerwa na jambo lenyewe!!!
   
 15. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #15
  Mar 24, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Nape mimi sio mwanasiasa wala huwa si mchangiaji sana kwenye issue za siasa.
  Napenda tuu unapoongea swala la ajira Tanzania ongelea kama Tanzania na swala la kusema kuwa lipo dunia nzima sidhani kama ni kipimo
  Jiulize wewe na sera za chama chako mnafanya nini kupunguza tatizo la ajira kwa vijana ambao kila mwaka wanamwagwa kutoka vyuoni na sekondari ambao hawana uhakika wa nafasi yoyote ya ajira kwenye private sector au kwenye serikali
  Mmetengeneza nafasi ngapi mpya za ajira toka mlipoingia madarakani maana rate ya viwanda kufa imeongezeka sana toka hii awamu iingie madarakani
  Viwanda vingi vilivyobinafsishwa vimegeuka magodown ya kuhifadhia bidhaa kutoka china na korea
  Je mlalishughulikiaje hilo au mna sera gani kuhusu hilo
  Hizi takwimu za waziri wenu hazina lolote maana ukweli watu wanauoana wanaoishi huku mtaani vijana wengi waliomaliza vyuo na sekondary hawana tegemeo lolote la maisha
   
 16. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #16
  Mar 24, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  penye nyekundu hayo nimaneno ya mtu mvivu huwa sipendi kuyasikia nappe ikiwezekana wewe kijana mwenzangu yatoe na UELEZEEE JINSI SERIKALI YAKO INAVYOFANYA JUHUDI KULIONDOA, unaposema dunia nzima wenzetu litatoka libaki kwetu tu, dunia nzima wanafanya juhudi lakuliondoa tunataka sehemu yenu ni ip??
   
 17. rifwima

  rifwima JF-Expert Member

  #17
  Mar 24, 2012
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Yaani hata wewe ni kiongozi ndani ya nchi hii!? Kama tatizo la ajira lipo jawabu ni kulitatua, siyo kulinganisha kizembezembe kwamba lipo duniani kote. Pamoja na hayo, kama lipo duniani kote, lets say "tatizo lipo Tanzania na UK". UK the government pay Unemployment benefits to her people. Nyie mnafanya nini kama siyo kupiga mavuvuzela tu kujinufaisha peke yenu? Thinking yako kwa mjibu wa maelezo yako hapo juu...tatizo la ajira lipo na lipo Duniani kote, the inference from your slight cheap premise ni kwamba, kama lipo Tanzania na Duniani kote, therefore its not an issue in Tanzania, liendelee kuwepo tu. Inaonekena hata hujui uko Duniani ulokutaja wao wanadeal vipi na tatizo hilo.
  Swali, Je Tanzania inakosa nini mpaka tatizo la ajira hasa kwa vijana liwepo? Wakati unajibu fanya ulinganifu wa resources zilizopo nchini (the vast fertile land, Geological resources, water, vegetation, animals, wind, sun including human resources...Vijana) just few to mention. Kama ni muungwana utasema "Leadership is missing".
  NAPE, CCM and all its associates ni Janga la kitaifa. CCM italipeleka Taifa hili pabaya.
   
 18. M

  Mpanzi JF-Expert Member

  #18
  Mar 24, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 767
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Nape unahitaji kujifunza kutoka kwa viongozi wenzio vijana kama Makamba na Zitto, huwa hawakurupuki, their minds run faster than their mouths! Kupambana na Lowassa hakutakusaidia, you are digging your own grave!
   
 19. NdasheneMbandu

  NdasheneMbandu JF-Expert Member

  #19
  Mar 24, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 940
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nape,

  Katika jambo ambalo binafsi huwa silipendi ni kutaka kuhalalisha mapungufu yetu kwa kulinganisha au kutoa mfano wa mapungufu hayo hayo yanayotokea katika nchi zingine au maeneo mengine. Inawezekana wenzetu hali ya ajira ni mbaya kwa sababu ya uchache wa rasilimali au fursa nzuri za kiuchumi. Sisi kama Tanzania ni nini tusicho nacho? Tuna ardhi nzuri ya kilimo, mito mingi, tumezubgukwa na maziwa pande zote na mengine ndani kabisa ya nchi, tuna madini ya kila aina na mengine yanapatikana hapa kwetu tu, tuna mbuga za wanyama nyingi, tuna bandari Tanga, Dar na Mtwara bila kutaja za maziwani, tuna misitu, n.k na zaidi ya yote nchi yetu ni tulivu. Kwa fursa hizi, Bw. Nape kweli ni halali vijana wetu wakose ajira!!!! Nape, ni vizuri kukiri kwamba mipango ya serikali ya chama chako cha ccm ni mibovu na hii yote ni kwa sababu ya rais wetu kuendekeza utegemezi kwa wazungu. Wakati mwingine huwa najiuliza hivi kikwete huwa haoni aibu kuzunguka na bakuli la misaada wakati anaowaomba hawana hata robo ya rasilimali ilizonazo nchi yake!! Kijana kama wewe ulipaswa kulisimamia ipasavyo tatizo hili vijana kukosa ajira badala ya kupoteza muda kushindana kwa kauli na Mhe. Lowassa. Hata kama nae ana mapungufu yake, lakini kauli ya Lowassa kuhusu vijana ni sensible na msipoifanyia kazi haki ya nani Mungu shahidi bomu hilo litawalipukia.
   
 20. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #20
  Mar 24, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Anachosema mwandishi wa thread ni kweli. Kuna mtindo mbaya umeanza kujengwa na ccm wa kuponda kila kinachosemwa na viongozi wastaafu hata kama kina mantiki. Njia inayotumika ni kutaja mapungufu ya kiongozi husika ili aogope na kukaa kimya. Tabia hiyo ni ya kipuuzi na ninamwonya Nape aache mara moja. Wenye nchi watakapoichukua nchi yao sijui atakimbilia wapi.
   
Loading...