Sijui kipindi kile Nape uliishwa vitu gani. Ulikuwa mtu wa hovyo sana katika aridhi ya Tanzania. Yaani leo hii tunapiga kelele za Bashite na kulaani baadhi ya upuuzi anaoufanya; Mh Nape wewe kipindi kile ulifanya zaidi ya haya ya Bashite. Unavyoona humu ndani habari nyingi ni za Bashite/Makonda, kipindi hicho sehemu kubwa ya habari jf ilikuwa ni Nape.
Wengine tunaamini kabisa hata hiyo nafasi uliipata baada ya yote uliyoyasema na kuyatenda.
Mh hongera sana kwa kubadilika na kukubali kuwa 'mtu'. Yawezekana hata Makonda ipo siku atajirudi tu. Ni suala la muda. Lakini tukumbuke kuwa maneno na matendo yetu yanaweza kusamehewa lakini hayawezi kusahaulika.
Endelea kuonesha msimamo na uongozi wako ndani ya utawala huu usioeleweka vizuri. Kila binadamu anayo tabia ya asili ya kuchoshwa na kukelwa na jambo au kitu fulani.