Nape unasemaje sasa kuhusu falsafa mufilisi ya kujivua gamba? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape unasemaje sasa kuhusu falsafa mufilisi ya kujivua gamba?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Crashwise, Jun 15, 2012.

 1. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Wapo watanzania wanaoamini kuwa itawachukua muda sana kumsahau mwanasiasa Nape Nauye kut View attachment 56473 okana na kile kinachoweza kutafsiriwa kuwa jinsi mwanasiasa huyo kijana alivyojigeuza kichekesho kila anapopata wasaa wa kuzungumza na wanahabari naam!

  Huyo ndiyo Nape Moses Nauye yule katibu wa itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi ambaye amejipachika jukumu la kuitikia kiitikio cha wimbo maarufu wa Jakaya Kikwete wa ``CCM lazima ijivue gamba``.

  Sifahamu mara ngapi huwa Nape anazisoma makala zangu lakini nina uhakika kila anapopata wasaa wa kufanya hivyo huwa hakosi kuzisoma hivyo niweke wazi kuwa nina uhakika makala hii itamfikia iwe kwa kuisoma yeye mwenyewe au kwa kusikia kutoka kwa wapambe wake.

  Ni Nape Moses Nauye huyu ambaye sasa ameamua kupunguza ``uvuvuzela`` baada ya kumaizi kuwa alichodhani ni mapambano kumbe ni fitna za makundi ya ndani ya chama chake.

  Huyu aliwahi kujitapa kuwa CCM sharti ijivue gamba tena ndani ya siku tisini tu!, wenye akili tulishabaini kuwa hizi ni kelele za mlevi aliyenyimwa pombe, sasa Nape ni shahidi kuwa hivi sasa ni takribani miezi tisa sasa lakini hakuna gamba lililovuliwa au hata hiko chama chake kukiri uzito wa gamba hilo.

  Nape ni aina ya wanasiasa wanaopenda kubebwa kwa mbeleko , hii ndiyo sababu hata alipokuwa anajitokeza na kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu dhana ya kujivua gamba kila mwenye akili timamu alijua pasi na shaka kuwa ametumwa na wanaomtumia, alahaula!

  Lakini Nape kwa kutojua amefuta jina lake kwenye orodha ya wanasiasa wakubwa wa Tanzania wa miaka ijayo, hakuna ubishi naposema kuwa amejifuta mwenyewe naweza nisieleweke, bilashaka hii ni mantiki dhaifu lakini naomba wasomaji wangu muikubali kwasasa licha ya udhaifu wake kwa kuwa pasipo kukubali mantiki hii ya Nape kujimaliza itakuwa vigumu sana kwenu kuuelewa mwelekeo mbovu wa CCM na watendaji wake wa aina ya Nape.

  Labda nitoe mfano wa mwanaharakati na mwanamapinduzi aliyetutoka hivi karibuni hayati Regia Mtema ambaye aliwahi kufanya tendo la ujasiri la kuomba msamaha mara Baada ya matamshi yake makali dhidi ya wale aliowaita ``wafugaji wavamizi`` huko katika wilaya ya kilombero, nachotaka kukisema hapa in ule ujasiri wa Regia kujitokeza hadharani na kuomba msamaha ndiyo maana namuuliza Nape anangoja nini kuomba msamaha kwa kuwaghilibu watanzania? Si Nape aliyejifanya mafisadi watang`oka ndani ya siku tisini?

  Si Nape aliyewapotezea muda wananchi masikini wa nchi hii kwa kuwadanganya kila uchao? Anataka mpaka Kikwete amtume kuomba msamaha?

  Ni dhahiri pasipo shaka yoyote kuwa falsafa yaw kujivua gamba imefeli hata mwasisi wake Luteni Kanali Jakaya Mrisho Kikwete anafahamu ukweli huo, tatizo lililopo ambalo linazidi kuimaliza CCM ni kuwa si Kikwete wala huyo Nape aliyetayari kukiri hadharani kushindwa huko, ndiyo maana kwa kutambua hilo nataka kumuuliza Nape kuwa baada ya kushindwa kutimiza alichowaahidi watanzania, sasa anasema nini kuhusu falsafa mufilisi ya kujivua gamba? Tafakari!, A luta continua!

  Nova Kambota ni mchambuzi wa maswala ya kisiasa , Mwanaharakati na Mwandishi wa kujitegemea, anapatikana kwa anwani ya barua pepe novakambota@gmail.com, au tembelea tovuti yake www.novakambota.com
   
 2. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2013
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  iNA ZAIDI YA MWAKA LAKINI NAPE HUJAJIBU...
   
 3. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2013
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Maswali magumu haya utamuua bure..
   
 4. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2013
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  hivi alisema ni miaka 90 au siku 90.
   
 5. bulama

  bulama JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2013
  Joined: Dec 13, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kama alitumwa kuongea hayo anasubiri kutumwa ili ayakane au kukiri udhaifu wake na mwenyekigoda wake. Chama kizima kina akina mh. Pinda watupu.
   
 6. F

  FUSO JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2013
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,860
  Likes Received: 2,338
  Trophy Points: 280
  huku ni kutoneshana madonda!! wana JF tuoneane huruma.
   
 7. f

  fast jet JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2013
  Joined: Jun 29, 2013
  Messages: 202
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nape akionaga uzi kama huu huwa anafungaga macho..
   
 8. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2013
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Haiwezi kuwa siku 90 maana zishapita tusubiri miezi 90 isipokuwa hivyo basi tusubiri miaka 90 kama ccm itakuwa hai bado
   
 9. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2013
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hizo huwa naziita siasa za kukurupuka na huwa siku zote nape anakurupuka ndo maana anashindwa
   
 10. k

  kisimani JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2013
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 553
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Ha ha ha dah...JF burudani
   
Loading...