Nape ulipigania chama kwa msukumo wa posho nene uliyolipwa na si kutokana na mahaba ya dhati kwa CCM

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,375
Kwako Comrade Nape.

Nakusalimu kiongozi, pole na hongera majukumu ya kulitumikia Taifa.

Kiongozi ninakuandikia waraka huu lengo ni kutaka kujua kweli inayosambaa mitandaoni kuwa mnamo tarehe 8 Aprili, 2017 utakwenda jimboni kwako, na moja ya shughuli utakayoifanya ni kuongea na wapiga kura wako. Mimi sina shaka na wewe kuongea na wapiga kura wako hata kidogo, kwani ni kawaida kwa mbunge kuongea na wapiga kura wako. Kama ni kweli umepanga kufanya hivyo naomba uzingatie yafuatayo:

i. Naomba nikusihi sana tumia busara katika kuongea, kama busara itakushinda usiongee. Kuna tetesi kuwa endapo utafanya hivyo, ama ni wewe mwenyewe au jirani zetu, wameandaa kikundi cha kushangilia na kikiwa na mabango ambayo sio mema sana kwa chama chetu. Kama ni wewe jiulize mara mbili mbili.

ii. Umesema unakwenda kusema kweli, hakikisha kweli iwe kweli, kweli kweli, hata upande wako useme kweli yako, yaani udhaifu wako, usiseme udhaifu wa watu wengine tu, ukidhani wewe huna mawaa.

iii. Siku unaongea na waandishi wa habari uliowaandaa, ulisema umekipigania Chama, hili mimi sina shaka nalo hata chembe. Naomba nikukumbushe tu, ukirudia kusema hili, pia waambie hiyo ndio ilikuwa ajira yako katika Chama, na ulikuwa unalipwa ili ukipiganie Chama chetu. Kukipigania chama kwako wewe kunatofautiana sana na mabalozi ambao walipigana kufa na kupona ili chama kishinde, pasi malipo yoyote, lakini wewe ulikuwa unalipwa mshahara na stahiki zingine. Ingelikuwa ajabu kweli kweli kama Katibu wa Itikadi na Uenezi asikipiganie chama chake.

iv. Comrade, nakukumbusha tu wakati kulikuwa na dalili za wewe kuanza kupishana na Mwenyekiti wetu, kuna kundi la watu lilitokea likawa “linakutia hasira” kundi hili lilidiriki hata kukuambia ujiuzulu. Kundi hilo hilo ulipotolewa katika nafasi ya uwaziri, lilianza kukuzomea, likikuambia kwamba wewe ulikuwa mtesi wa wengine sasa nawe yamekukuta. Lilishadadia kusema Bunge live, sheria ya mtandao, mafisadi kukatwa 2015 ni wewe ulisababisha hivyo, ngoja uonje joto la jiwe. Kundi hili hili tena ndilo linaloeneza hiki unachotaka kufanya, nadhani hapa uwe mbayuwayu.

v. Nakusihi sana, mimi bado naona kuna nafasi ya kuwekana sawa, kama ulivyosema siku ile wakati unatolewa, kwamba hukuulizwa wakati wa kupewa Uwaziri, ni sawa. Lakini ulipopewa hukuitwa waandishi wa habari wala hukufanya maandamano jimboni kwako. Tumia busara Comrade, sasa kama kila kiongozi akitolewa katika nafasi yake akaitisha vyombo vya habari, itakuwaje? Kumbuka ulipokuwa mwenezi, ambapo ulipowatambua mawaziri mizigo, wengine walitolewa, lakini hawakuitisha vyombo vya habari.

Sina mengi Comrade, ni mimi mmoja wa watu waliokipigania chama na bado nasonga mbele kukipigania Chama pasi malipo yoyote kaka, tofauti na wewe uliyepigania chama wakati unalipwa mshahara mzuri tu na marupurupu.

Wasalaamu

Kisena Mabuba
Mwanamtaa
 
Too late...ulitakiwa uyaandike kabla ya uchaguzi hapo ningekuelewa.
 
Mnashindwa kuelewa huu uoga mlio nao dhidi ya nape unatoka wapi? Kama CCM ilishindwa kumsaidia alipokuwa ofisini basi na aachwe na wapiga kura wake. Na mtambue kuwa nape nyuma yake wapo wana CCM Wengi waliochoshwa na utawala huu wa kiimla na kulazimishama. Basi na kama unasema alilipwa posho ili awe kwenye chama basi na aachwe aongee si mmeshamfukuza kazini woga unataka wapi?
 
Kwako Comrade Nape.

Nakusalimu kiongozi, pole na hongera majukumu ya kulitumikia Taifa.

Kiongozi ninakuandikia waraka huu lengo ni kutaka kujua kweli inayosambaa mitandaoni kuwa mnamo tarehe 8 Aprili, 2017 utakwenda jimboni kwako, na moja ya shughuli utakayoifanya ni kuongea na wapiga kura wako. Mimi sina shaka na wewe kuongea na wapiga kura wako hata kidogo, kwani ni kawaida kwa mbunge kuongea na wapiga kura wako. Kama ni kweli umepanga kufanya hivyo naomba uzingatie yafuatayo:

i. Naomba nikusihi sana tumia busara katika kuongea, kama busara itakushinda usiongee. Kuna tetesi kuwa endapo utafanya hivyo, ama ni wewe mwenyewe au jirani zetu, wameandaa kikundi cha kushangilia na kikiwa na mabango ambayo sio mema sana kwa chama chetu. Kama ni wewe jiulize mara mbili mbili.

ii. Umesema unakwenda kusema kweli, hakikisha kweli iwe kweli, kweli kweli, hata upande wako useme kweli yako, yaani udhaifu wako, usiseme udhaifu wa watu wengine tu, ukidhani wewe huna mawaa.

iii. Siku unaongea na waandishi wa habari uliowaandaa, ulisema umekipigania Chama, hili mimi sina shaka nalo hata chembe. Naomba nikukumbushe tu, ukirudia kusema hili, pia waambie hiyo ndio ilikuwa ajira yako katika Chama, na ulikuwa unalipwa ili ukipiganie Chama chetu. Kukipigania chama kwako wewe kunatofautiana sana na mabalozi ambao walipigana kufa na kupona ili chama kishinde, pasi malipo yoyote, lakini wewe ulikuwa unalipwa mshahara na stahiki zingine. Ingelikuwa ajabu kweli kweli kama Katibu wa Itikadi na Uenezi asikipiganie chama chake.

iv. Comrade, nakukumbusha tu wakati kulikuwa na dalili za wewe kuanza kupishana na Mwenyekiti wetu, kuna kundi la watu lilitokea likawa “linakutia hasira” kundi hili lilidiriki hata kukuambia ujiuzulu. Kundi hilo hilo ulipotolewa katika nafasi ya uwaziri, lilianza kukuzomea, likikuambia kwamba wewe ulikuwa mtesi wa wengine sasa nawe yamekukuta. Lilishadadia kusema Bunge live, sheria ya mtandao, mafisadi kukatwa 2015 ni wewe ulisababisha hivyo, ngoja uonje joto la jiwe. Kundi hili hili tena ndilo linaloeneza hiki unachotaka kufanya, nadhani hapa uwe mbayuwayu.

v. Nakusihi sana, mimi bado naona kuna nafasi ya kuwekana sawa, kama ulivyosema siku ile wakati unatolewa, kwamba hukuulizwa wakati wa kupewa Uwaziri, ni sawa. Lakini ulipopewa hukuitwa waandishi wa habari wala hukufanya maandamano jimboni kwako. Tumia busara Comrade, sasa kama kila kiongozi akitolewa katika nafasi yake akaitisha vyombo vya habari, itakuwaje? Kumbuka ulipokuwa mwenezi, ambapo ulipowatambua mawaziri mizigo, wengine walitolewa, lakini hawakuitisha vyombo vya habari.

Sina mengi Comrade, ni mimi mmoja wa watu waliokipigania chama na bado nasonga mbele kukipigania Chama pasi malipo yoyote kaka, tofauti na wewe uliyepigania chama wakati unalipwa mshahara mzuri tu na marupurupu.

Wasalaamu

Kisena Mabuba
Mwanamtaa
Jazba apunguze bila hivyo atapotea kwenye uchaguz ujao maana ccm hawashindwi kumkata kwenye kula za maoni na kunyimwa uongozi WA aina yeyote ndani ya chama halafu ndo atajua ccm halisi ni IPI amabayo kwa sasa haifahamu ila akamuulize lowasa na sumaye wanaijua.
 
Back
Top Bottom