Nape: "uking’ang’ana na oil chafu injini yako itanoki"

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,477
15,320


Baada ya kimya cha muda mrefu, hatimaye Chama Cha Mapinduzi kilizungumzia uamuzi wa Edward Lowassa na wanachama wengine wa chama hicho kuhamia kambi ya upinzani. Akiongea na waandishi wa habari enzi hizo kuhusiana na Edward Lowassa na wanachama wengine wa CCM kuhamia kambi ya upinzani, aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM, Nape alitumia mifano mbalimbali ya kejeli katika kuhalisha mtazamo wake kuwa waliokihama chama hicho walikuwa hawafai kuendelea kuwepo.

Alisema kuwa kitendo cha watu hao kuhama kinaipa unafuu CCM kwa kuwa ni kama mtu anaebadilisha oil chafu kwenye injini yake ili kuiokoa, “uking’ang’ana na oil chafu injini yako itanoki.” Pia, Nape alidai kuwa kuondoka kwa wanasiasa hao kwenye chama hicho kwa sababu hawakutimiziwa kile walichotaka na kujiabisha kwa kujivua nguo mbele ya wananchi.

“Kwamba CCM ilikuwa njema kwa miaka yote ambapo wewe ulikuwa na fursa, ikifika mahali unaambiwa wewe hauna fursa kwa jambo unalolitaka moja basi unaona CCM haifai kwa kila kitu. Bila shaka wamejivua nguo mbele za watu na watanzania watawaadhibu,” alisema Nape.

Hata hivyo, Nape alisisitiza kuwa ni kawaida katika siasa watu kuhama chama kimoja kimoja kwenda chama kingine na kwamba wapo ambao wataendelea kuhama kutoka CCM kuingia upinzani na wapo watakaotoka upinzani kurudi CCM. Nape aliweka mkazo kuwa pamoja na mambo mengine yote, CCM lazima itaibuka na ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu mwezi Oktoba 2015.

Chanzo: http://dar24.com/nape-awafananisha-akina-lowassa-na-oil-chafu/
 
....
.....Mshukuruni.MUNGU kwa kila Jambo

Kwa kweli maana ......

hqdefault.jpg
 
Kwa kweli maana ......

hqdefault.jpg
Hahahah, kweli mkuu... Niliwahi sema kilichotokea Dodoma 2015 kitaitafuna CCM na walioshiriki kukifanya!!

Yetu macho na masikio.... Ikiwa tuna Bahati... Mungu atatupa fursaa ya kuona
 
Lowassa bwana
ukianza kuangalia wale wote walio kuwa wanamsema vibaya,
yanayo wapata sasa hivi ni balaa huyu huyu Nape ndio alimkejeli Lowassa kwa sababu ya Magufuri,
Sasa inayotumika ni law of KARMA.

AHAMIE TU CHADEMA ASIONE AIBU.
mbona kina fulani walikuwa wanamsema vibaya lakini alivyo hamia CHADEMA wametulia wakati kila siku walikesha kutuaminishi Lowassa ni fisadi...!?
 
Lowassa bwana
ukianza kuangalia wale wote walio kuwa wanamsema vibaya,
yanayo wapata sasa hivi ni balaa huyu huyu Nape ndio alimkejeli Lowassa kwa sababu ya Magufuri,
Sasa inayotumika ni law of KARMA.

AHAMIE TU CHADEMA ASIONE AIBU.
mbona kina fulani walikuwa wanamsema vibaya lakini alivyo hamia CHADEMA wametulia wakati kila siku walikesha kutuaminishi Lowassa ni fisadi...!?
Sofia simba madabida nao walimsema Lowassa?
 
Back
Top Bottom