Nape: Tutaanza kuwatumia vijana wetu kulinda viongozi

Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,550
5,688
Namtakia kila la kheri ktk mkakati aliouanza. Ajue kuwa nguvu ya umma ni zaidi ya vijana wake.
 

Tetere Enjiwa

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
217
65
Hivi waTz wote tumekosa akili na busara kiasi hiki, kweli kama ni watu wenye akili timamu tunakaa tunaongozwa na viongozi kama hawa, hawa ndio viongozi wetu kweli. sisi tumekaa tunasubiri watuvuruge tuuane kweli, nchi hii inaongozwa kisultani na sisi tumerizika kabisa tumekaa tunaangalia tu, jamani tumeingiwa na nini?

Yaani wote sisi tumekuwa mazezeta kiasi hiki, wote hawa ni watoto wa viongozi ndio wanakuja kuongea pumba mbele yetu tunawaangalia tu. Wamemtoa RA ghafla wamerudi kumpigia magoti, sisi tumekaa tu hawa watupe uongozi kwenye nchi yetu tufikie pahala tuseme hapa imetosha, hivi kweli waTz tumekuwa wajinga kiasi hiki, hivi kweli siamini.
 

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,876
6,836
Kwa nini vijana hao Nape hakuwaelekeza kuwalinda wake za watu wasinajisiwe na viongozi wa CCM hasa Mwigulu?
 

Tundapori

JF-Expert Member
Aug 12, 2007
585
181
Kwanza huyu katoa wapi ruhusa ya kubwabwaja hovyo bila kufikiri kwanza ndo aseme? Je, karuhusiwa kweli na wakubwa/mabosi wake kubwabwaja au anaiba tu rukhusa ili mradi aonekane na yeye yupo kwenye msitu wa matunda pori mengi? Awe mwangalifu asije kula "tunda bangi" ataharisha sana, tunda hatari sana hilo lina tabia ya kuifanya sehemu ya haja kubwa itoke nje (Rectal prolapse).
 

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
nape asema sasa wataanza kuwatumia vijana wao kuwalinda viongozi wao.ameongeza kusema haiwezekani watu wa arusha na mwanza waende igunga kubaka watu,kudhalilisha wakina mama na kupigana mapanga.anasema wao hawatakubali.ameongea na waandishi akiwa dar.
my take;
ccm maji yamewafika shingoni na wanashindwa wafanyeje.sasa waameanza siasa za maji taka na ubaguzi wa kusema watu wa arusha hawatakiwi kwenda kwenye kampeni igunga.anafikili ccm ndo ina vijana tu.nape mwaka huu mnalo na limewaganda.
chanzo ch10.mia

Nadhani ningemuona Nape wa maana kama angesema wana mpango wa kuwatumia vijana kulinda mali ya umma inayoibiwa kwenye migodi ya madini na wanyama wetu wanaochotwa mbugani....Kuwalinda viongozi wahuni kama yule mkuu wa wilaya sidhani kama ni big deal.
 

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,882
Mimi Lunyungu huko nyuma nilisha waonya kwamna acheni kuleta mda zozote zinazo mhusu huyu kula kulala .Huyu ni mtupu lakini hamkunisikia .Leo CCM wanahubiri fujo kwa uwazi baada ya kuzifanya kwa ndani ndani na kushindwa. Haya yetu macho na masikio huko Igunga .
 

lyimoc

Senior Member
Feb 20, 2011
140
9
Akitaka kuona vijana wa cdm ajaribu aone moto wa gesi yeye anategemea mateja cdm vijana tuko fiti muda wowote iwe usiku au mchana gusa unase Nape
 

BASHADA

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
513
147
Nilishahisi kuna kituko kitafuata baada ya yaliyojiri siku mbili tatu hizi Igunga. Unajua Nape presha imepanda kote kote sasa hata uwezo wa kufikiri umeswitch off. Haya lets wait and see. Hivi bado hajajijua kuwa yeye ni gamba vuvuzela naye aatakiwa akajivue kwanza.
 

UmkhontoweSizwe

Platinum Member
Dec 19, 2008
7,018
5,545
Kama ni kweli Nape kasema hayo maneno basi yeye ni hopeless, na hastahili kuwa kwenye nafasi hiyo ya uenezi na itikadi ya chama chake. Kiongozi wa ngazi yake kwenye chama TAWALA hawezi kuhamasisha na kutishia kutumia MAJAMBAZI kwenye shughuli yoyote inayohusu jamii. Ni upuuzi na ujinga uliopindukia!

Yeye ndo anapaswa kuhamasisha watu kuheshimu sheria na vyombo vya ulinzi. Polisi wanafanya kazi gani mpaka chama tawala kiamue kutumia vibaka kulinda viongozi wake? Sikio la kufa ..................!
 

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,296
I wish ningekuwa na database ya kutunza kauli za huyu jamaa zote....
 

Mkulima wa Kuku

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
1,271
532
Hii ni aibu! Jeshi la polisi lenu na linawalinda kwa gharama zetu, bado hamuaminiani mnapeleka wengine porini kwa mafunzo maalum ya ugaidi... Hivi wangekuwa CUF au CDM wamepeleka vijana wao porini kama ninyi leo si kungekuwa na vita ikijumuisha mpaka JWTZ? Nepi ameishiwa hoja, ccm imeishiwa hoja sasa wanataka kuvuruga amani ya nchi ili uchaguzi usiwe wa haki wajitangazie ushindi kama huko nyuma... Vijana wa cdm aluta continua...mpaka kieleweke
 

mashikolomageni

JF-Expert Member
Jan 5, 2010
1,569
185
Nape kumbe ni kilaza sasa kama ametangaza kuwa wao watajiamulia la kufanya kwa sababu polisi imeshindwa hajui maana yake ni kuwa serikali ya ccm imeshindwa kutoa ulinzi kwa raia na viongozi wake!!!!!!!!!
 

Feedback

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
7,990
4,506
Alichokifanya ni kuzidi kumuaibisha kampeni meneja wake Mwigullu na issue ya kufumaniwa. Yeye hajioni kuwa hatakiwi CCM utakuwaje katibu mwenezi usifike kwenye kampeni uanze kubwekea mbali?
 

mwanapolo

Senior Member
Mar 29, 2011
193
55
Wanasema DC mwanamke kadhalilishwa tena na vijana! Mbona hawasemi DC kafanya kosa gani?
Kwani kuwa mwanamke kunamtolea kinga ya kufanya makosa? Nafikiri ifike wakati tuheshimu sheria zetu, DC huwezi vuruga aman watu wakuchekee tu.
Huyo DC mwenyewe ana uzoefu gani kama sio vyeo vya kupewa?
Nilidhani DC angeonywa kwa kitendo cha kuingilia ratiba ya CDM wananchi wa Igunga wangeweza kuielewa serikali yao. Lakini kwa hili naona kama wanazidi kujiharibia. Hata hiyo kesi waliofunguliwa wabunge sijui kama ina nguvu sana.
 

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
12,738
22,085
Episode ONE

Shaban: ( mpambe wa Rostamu) Nape unatafuta nini hapa?

Nape: (vuvuzela la CCM) Wewe unafahamu unaongea na nani?

Shaban: (kwa dharau) Ndiyo. Nafahamu kwamba wewe ni Nape Nnauye.

Nape: (kwa unyonge)…Nimekuja kikazi. Tupishe tunamazungumzo yetu.

Shaban: (kwa ukali)…Ondoka hapa, vinginevyo tutakuonyesha. Umekuja kutuharibia uchaguzi siyo ?
Mara baada ya kauli hiyo, taarifa zinasema Nape aliondoka katika eneo hilo na kuingia kwenye gari lake haraka kuelekea Singida.

Episode TWO

JF: (ikitoa breaking news)) Nape kapigwa marufuku asikanyage Igunga.

Mukama: (wakiwa Dodoma) Nimeambiwa unajiandaa kwenda Igunga? Mbona wewe kijana husikii ? …hutakiwi kukanyaga Igunga.

Nape: (akitamba kenye Facebook) Mlisema chama kimempiga marufuku Nape kukanyaga Igunga, nikasema tusubiri. Leo, mmeona nilivyotinga Igunga..

Mukama: (akifoka) Nape, nimeambiwa umekwenda Igunga, wakati Kamati Kuu ya chama imekuzuia kwenda huko. Unataka nini? Mbona umekwenda ?

Nape: (akijitetea) Nilikwenda kuhani kutoa pole kwa familia ya wazazi wa mtoto Peter Ezekiel, aliyefariki dunia papohapo baada ya kugongwa na gari la mizigo, wakati mgombea wa CCM, Dk. Peter Kafumu akichukua fomu.

Mukama: Nani amekutuma? Nani amekuruhusu? Kijana, tafadhali usituharibie uchaguzi. Wewe, Samwel Sitta, Christopher ole Sendeka na Dk. Harrison Mwakyembe hakuna kukanyaga Igunga, Rostamu Aziz hataki kuona sura zenu huko
!

Sasa tusubiri Episode THREE.
 

Izack Mwanahapa

JF-Expert Member
Apr 21, 2011
497
235
Viongozi wa vyama mnatakiwa kutulia, kutafakari na kuchagua maneno ya kuongea mnapotaka kuzungumzia mustakabali wa chaguzi ndogo zinazoendelea nchini. Msitumie matatizo makubwa haya yanayojitokeza na kuwaathiri wananchi kama mtaji wa kisiasa. Kumbukeni mwisho wa maneno haya ya uchochezi Madhara ni kwa wananchi wa kawaida.
 

Arafat

JF-Expert Member
Nov 17, 2009
2,582
755
Vijana wao! Vijana wa CCM! Green Guard!

Kumbe DC ni kiongozi wa CCM? na anapaswa kulindwa na Green Guard na siyo Polisi? Haya Polisi nadhani mmesikia hayo maneno, DC alikuwa anafanya kazi za CCM na siyo za Umma.

Nape ametupa ushahidi wakutosha kuwa DC alikuwa anafanya kazi za CCM na siyo Umma na kuwa sasa ataendelea kuzifanya chini ya ulinzi wa Green Guard.
 

jigoku

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
2,413
731
Huyo dogo hana hata mshipa wa aibu au kwa vile CCM yote wamekuwa viziwi na vipofu,au dhambi ya ufisadi imegeuka kuwa laana juu yao,,hivi kweli haka ka Nape hakaoni hata aibu kuwa ka vuvuzela ka chama huku kakiwa hakakubaliki?na ndio maana kanaanza kuleta lugha za uchochezi,wameona jeshi la polisi halitoshi,usalama wa Taifa hautoshi na saa huyu Nape anatangaza kupeleka vijana,apeleke aone,asidahani tunayafurahia yale wanayotufanyia.

Kwanza wewe Nape niliwahi kukuuliza kwa nini hukanyagi Igunga kipindi hiki cha Kampeni? Hiki ni kipimo tosha kuona kama unafaa au hufai,kwa nini ulipigwa stop Igunga,kwanza umeniudhi nijibu hata kuhusu siku 90 za magamba hazijaisha tu? Wewe si ilikuwa unapiga kelele magamba utayashughulikia? We dogo we we huo ni mziki mzito sana wala huna uwezo wa kuyavua magamba,kmwe Nape hapo unaota ndoto,CCM wote hamuwezi kumtoa Chenge na Lowasa hata kwa kupigana bado Nape hutaweza.

Acha kuropoka bwana
 
2 Reactions
Reply
Top Bottom