leonaldo
JF-Expert Member
- Oct 26, 2014
- 2,583
- 3,181
Hatimae leo mchawi halisi wa watanzania, asiyetaka wananchi wasiangalie bunge live abainika kuwa ni chama cha mapinduzi CCM. Baada ya jambo hili kuzunguka kwa mda mrefu imebainika kuwa baada ya uchaguzi kamati kuu ya halimashauri kuu ya CCM iliagiza serikali kuhakikisha matangazo ya moja kwa moja ya tv na radio yanakomeshwa. Kama ni kweli CCM hii ndio shukurani yenu kwa watanzania? ombi langu kwenu jitokezeni hadharani mlikubali msitutende huku mkiwa mafichoni kama sio lenu jitokezeni mkanushe na muwaambie watu wenu waache kubaka haki zetu. Kama lengo lenu lilikuwa kuwanyamazisha wapinzani mmekosea sana jambo hili limewaudhi watanzania wote bila kujali vyama hasala mtakayoipata ni kubwa kuliko faida. wa salaam