NAPE: Tumetuma Vijana wapeleke mashambulizi mitandao ya kijamii

kapotolo

JF-Expert Member
Sep 19, 2010
3,727
2,214
Nilimsikiliza Nape Juzi akihojiwa Mlimani TV, moja kati ya mikakati yao ni kuwafikia vijana wengi popote walipo. Kati ya njia wanazozitumia ni kutuma vijana waingie kwenye mitandao ya kijamii ambako wanaamini kuna vijana wengi na hii itawasaidia kuwapata.

Hili wimbi la wanachama wapya kwenye hii mitandao, hususani jamiiforums, ambao wana itikadi za kimagamba limenifanya niamini kauli hii ya Nape. Lakini waje wakitambua vijana wa kileo wanajitambua na propaganda za magamba haziwezi tena kuwashawishi.

Hongera Nape lakini hii strategy, kama zilivyo nyingine, naamini haitafanya kazi kwa kuwa mfumo wa uendeshaji wa chama chenu cha magamba ni mbovu na ndio tatizo.
 
Kwanini wasitume vijana kuhamasisha shughuli za maendeleo. Kweli priorities zetu zinatofautiana sana. Akishatuma vijana then what nchi itapata maendeleo???
 
Mfikishieni ujumbe, kuwa vijana wake wamefeli, badala ya kujenga, wao wanabomoa.
 
Haya maneno mkuu huenda yana ukweli mkubwa sana ndo maana hapa Jamvini kuna watu wanajibu kila post na ukisoma majibu yao yanafanana ni kutetea ccm na serikali yake. Ingawa hii ni kazi ngumu sana kufanya manake unaandika usichokiamini ili mradi mkono uende kinywani na mwisho wa siku watu wanakuelewa na kukuponda vilevile.

Njia hii ya kutuma watu mitandao haitakijenga chama kama wanavyofikiri na pia ni muhimu wajue kuwa watu wengi wanaoonyesha machungu yao na kutaka mabadiliko hawakutumwa na chama chochote bali dhamira zao za ndani na hali halisi ya maisha ya Mtanzania wa leo.

Njia ya pekee ya kusaidia kuinusuru ccm ni kufanya kazi tu, kujenga matumaini mapya kwa watu kwa vitendo, kupunguza makali ya maisha na kubalance mgao wa keki ya taifa Vinginevyo hizo pesa wanazowalipa hawa watu ambao wengine wao wako hapa JF zinapotea tu bure na bado wataanguka tu
 
Waambie hata waje 1000,kijana mmoja wa jf anawatosha kabisa .Magamba kitu gani bwana
 
Huyu bado yupo kuleee mwaka 47, anaota mchana kweupee....ivi kweli hao vijana watafanya nini wanadhani wanavua perege kwenye mto ruvu hapa JF ? OK makada karibuni mje mmwage sera za magamba.
 
Hata watume vijana mia na maelfu haitaweza kushawishi lolote zaidi ya kuleta malumbano yasiyo na miguu wala kichwa kama ya MS na wengine. CCM itapaswa iongee kwa vitendo kutushawishi humu ndani na hilo ndilo tatizo. Nape mwenyewe yumo humu ndani na mara zote ameonekana hoja nyingi anazozitoa humu ndani ni umbea au taarabu za kishabiki zisizo na mashiko yoyote sasa vijana wao ndo itakuwaje?

Chema chajiuza kibaya chajitembeza. Waje wajitembeze sisi tunashawishika na hoja za mashiko sio blahblah za kidumu chama cha Magamba.

Kwanza kukuta kijana yuko CCM ujue ana mashaka na taaluma na uwezo wake kuweza kupambana na mazingira baada ya chuo. Wengi wanasukumwa na maslahi badala ya uwezo wao na kujiamini hivo wakija humu na pumba zao hatushawishiki. Waje na hoja si ushabiki ili mradi mkon uende kinywani.
 
Huyu kijana Nepi hajui alichokiandaa juu ya ccm! Kitendo cha kutuma vijana baadala ya yeye na wenzake kuingia huku nakuuza sera za chama chake ametuma vijana wahuni kama MS,Faiza,Ritz,Tumaini na wengine kukiua chama!!
 
Mfa maji haachi kutapatapa.
Chamsingi hao vijana wangetumwa kuzunguka nchi nzima kuwaaga wananchi kwa niaba ya chama chao.
Waende wakiimba"Saaasa saa ya kwenda kwetu kwaheri ikulu kwaheri hatuonani kesho".
 
Nilimsikiliza Nape Juzi akihojiwa Mlimani TV, moja kati ya mikakati yao ni kuwafikia vijana wengi popote walipo. Kati ya njia wanazozitumia ni kutuma vijana waingie kwenye mitandao ya kijamii ambako wanaamini kuna vijana wengi na hii itawasaidia kuwapata.

Hili wimbi la wanachama wapya kwenye hii mitandao, hususani jamiiforums, ambao wana itikadi za kimagamba limenifanya niamini kauli hii ya Nape. Lakini waje wakitambua vijana wa kileo wanajitambua na propaganda za magamba haziwezi tena kuwashawishi.

Hongera Nape lakini hii strategy, kama zilivyo nyingine, naamini haitafanya kazi kwa kuwa mfumo wa uendeshaji wa chama chenu cha magamba ni mbovu na ndio tatizo.

Sasa watu wenyewe ndio akina MS na FaizaFox? Watz sasa hivi hawadanganyiki, Nape akaendelee kugawa kanga za magamba!
 
.....Vijana wa miaka hii si analog wa kupelekwa kama upepo...nimeona baadhi ya mikutano ya Nape kwenye vyombo vyetu vya habari..anatumia nguvu mno kutujengea imani kwa chama chao.

CCM kwa vijana wa sasa ni kama malaria..haikubaliki na Tanzania bila CCM inawezekana kila mmoja atimize wajibu wake,tutawang'oa...
 
Wapo ila tatizo hawajajiandaa,wakishapata mgao pale Lumumba na kupewa desktop wanakimbilia ku login jf bila hata kufikiria wanachoongelea. Mfano ni jamaa mmoja kaleta hoja anasifia bajeti ya jk ya mwaka 2011/12 eti ni kubwa kwa kuwa ni nzuri ,kataja amount eti ni kama bil14.

Nimemjibu kuwa aliyemtuma kamdanganya bil14 hata nusu wizara haitasimama. Nkamweleza aende kuchukua maelezo upya kwani iyo aliyotumwa ni 10% tu ya wizara ya ujenzi. Next time waambiwe kuwa kwa sasa bajeti imeshaingia kwenye trilioni na si bil. Wapo wengi ila tutaenda nao sawa tu,si ugomvi ni mwendo wa kuwaelimisha tu!
 
Kama hizo ndizo fikra zake bado hajaelewa mitandao ya kijamii. Members wa social networkings like Jamii ni watu wenye uelewa mkubwa miongoni mwa watanzania. Wanaweza kupima na kuchagua!

Ushauri wangu kwake, CCM watatue kero za jamii zinazopigiwa kelele na wananchi. Bila hivyo hata wangetuma vijana laki 2 ili wameze members wote kitakachotokea ni Great thinkers kuamia kwenye mitandao mingine pale JF itakapogeuzwa sehemu ya porojo!
 
Nilimsikia jana kwenye kipindi cha KEKI YA TAIFA,AKAJINASIBU KUWA WANA BENKI YA VIJANA AMBAO NI MAKADA PALE UVCCM TAIFA,ALIZUNGUMZIA SUALA LA MITANDAO YA KIJAMII
 
Huyu kijana Nepi hajui alichokiandaa juu ya ccm! Kitendo cha kutuma vijana baadala ya yeye na wenzake kuingia huku nakuuza sera za chama chake ametuma vijana wahuni kama MS,Faiza,Ritz,Tumaini na wengine kukiua chama!!

Vijana wengi wa CCM ni bendera fuata upepo na hata akiwatuma wengi hawataweza kuingia humu kutokana na kuwa na uwezo finyu hata wa kutumia mtandao. Wengi ni njaa kali na hawajitumi bila kupata ka- alawansi.

Tulioko humu tumeamua kuipigania nchi yetu kwa damu zetu wenyewe bila kutumwa na mtu bali tukisukumwa na stimulus kama viongozi wezi na wabinafsi pamoja na nchi kukosa dira na hivy hali ya uchumi kuwa mbay. Kwetu hii ni coping strategy ya kujikwamua wakati wao vijana wa CCM ni kutafuta kula au mradi.
 
Nape una ujasiri gani wakati wewe mwenyewe unaikimbia mitandao hiyo? Huna ubavu wowote wewe na vijana wako. Muulize malaria sugu atakwambia hadanganyiki mtu hapa. Sana sana wataishia kupewa BAN. Kama wanakuja hapa waje na hoja lakini wakija na vioja wataipata fresh.
Mimi niko kwenye sites zote hizo na mashambulizi yenu nayaona lakini hakuna hoja ya kuvutia zaidi ya kujaza matusi tu.
Kwa kuanzia kaa wewe mwenyewe tukudadavue
:madgrin:
 
Back
Top Bottom