Nape: Sijaiona sababu ya Serikali kuchukua fedha zake kuwekeza kwenye miradi mikubwa

Hivi kweli mkosaji haishi kulalama:-

Nape alikuwa ndiye Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM...na ndiye aliongoza kupiga UFISADI vita..nini maana yangu kuanza hivyo ,wao ndiyo walioandaa ILANI ya Uchaguzi ya miaka 5(2015-2020) ambapo karibu hayo yote aliyoyasema yapo MLE kwa maana kama Ilani iliandaliwa basi ilijumuisha watu wa Kada mbalimbali.

Unapoandaa Ilani ya Uchaguzi na ispotekelezwa basi unajionyesha mbele ya Wapiga kura wako kwamba HUKUWA na UWEZO je,kwenye kuandaa hiyo ILANI iliwekwa kwamba Serikali ije kutumia Sekta binafsi katika kuendeleza MIRADI?Lakini katika UOZO wa FIKRA anaouongea Nape ni UWANJA WA NDEGE ambapo anajitia UPOFU kwa kujifanya hili jambo limeletwa na JPM anasahau lilianza na Mkapa na kumaliziwa na JK ambapo kama kulikuwa na haja ya kutumia watu binafsi kuuendesha ilikuwa ni huko NYUMA na si sasa,isipokuwa alichokifanya JPM ni kusawazisha hilo maana alikuta Wakandarasi WANADAI na Ujenzi ulisuasua,sasa yeye KAWAMALIZIA MALIPO na HAWADAI ila sote twakumbuka alipokwenda pale ALIKOSOA GHARAMA ILIYOTUMIKA kuwa ni KUBWA kwa UWANJA ULE kwqmba kuna HELA ILIPIGWA.Hili nalo lawama ANABEBESHWA JPM kuwa anatumia pesa ya Serikali kwa Miradi mikubwa,ndani ya Miaka mitano UANZE kuita sekta binafsi kisha uwape MIRADI waiendeshe MSIPOKUBALIANA?Mtawajibu nini Wapiga Kura?

Hiyo Reli tunaona hapa ilipewa sekta Binafsi lakini kilichotokea tulikishuhudia,mpaka BUNGE wakaingilia kulalamika na kuliua lile shirika na Mkataba wake wa Awamu ya 4,Nape akiwa Mwenezi wa Chama maboresho ya Waganyakazi anayotaka Nape yaboreshwe ni yepi kuliko kuongezwa mishahara na kuondolewa kodi asilimia 2 kwa Wafanyakazi na Wakulima kusimamiwa mauzo ya Mazao yao na kuondolewa kodi takriban 80?

Mradi wa umeme vijijini na miradi ya maji iliyokuwa kero nayo inatatuliwa kwa nguvu wakati huu.
Itikadi ya CCM ni UJAMA NA KUJITEGEMEA ...Mwenyekiti Magufuli katumia Uwezo wa ziada KUKUSANYA KODI na KUONGEZA KARIBU BIL. 400 kuwa 1.2-1.3TRL kutoka BIL.8OO-900 za JK ambapo tulishudia mikwamo mingi ya MIRADI hasa WIZARA zinapopewa kiasi chini ya Walichoomba kwenye BAJETI.

Juzi akihojiwa Dodoma alisema yeye ndiye kwa kiasi kikubwa na Mzee Kinana walizunguka miezi 36 na wakafanikiwa kuingiza waliyoyaona ktk Ilani hii ambayo JPM anaitekeleza labda alitaka tumuone kuwa JPM si lolote ila yeye kwa hiyo ILANI anayoigeuka LEO.

Ni vyema TUJENGE WENYEWE kuliko KUJENGEWA hao SEKTA BINAFSI.Maana huna HAKIKA ni LINI UTAKUBALIWA .

Nape amejaribu kuonyesha kuwa WABUNGE wa CCM wana uwezo wa KUJENGA HOJA ila mtindo alioingia nao ndiyo kaukosea ni ULE wa WANAOPINGA pasina FIKRA.

JPM kwa kwa kuisimamia MIRADI kwa PESA za NDANI yuko SAHIHI mno NAPE na WENZIO RUDINI KWENYE ILANI. Mtapata majibu.
 
ni utaratibu wa kazi, ukiwa waziri huwezi kusema hivi sio Nape wala Bashe wala Serukamba so msipotoshe
Wamesahau yaliyompata Lyatonga Mrema awamu ya pili!! Kuna huyu mdudu anaitwa collective responsibility kwa mawaziri. Huwezi kuikosoa serikali ukiwa waziri ukabaki salama. Labda uamue kujiuzulu ndio unaweza kuikosoa serikali, lakini ukiwa ndani ni kutetea tu hata ya hovyo hovyo!! Nape sasa hivi ana uwezo wa kusema anachotaka, hawajibiki tena serikalini na hawawezi kumfanya chochote, yuko huru.
 
Leo hii mheshimiwa Nape Nauye ameeleza kwa kina jinsi ambavyo serikali inakosea katika mambo mengi sana, nape anasema Serikali imevaa viatu ambavyo sio saizi yetu. Nimependa sana Uzalendo wa Nape Nauye ... Hebu mtazame hapo chini alivyofunguka kisha toa maoni yako.

Tunashangilia bila analysis!! Naamini michango yake bungeni ni kazi ya kusimuliwa. La maana angeweza kuiambia serikali isiwe overambitious. Lakini huwezi kunishawishi kwamba eti miradi ifanyike kwa kutumia private sekta. Private sekta ipi?? Iko wapi. PPP kwenye nchi hii kwa tawala zilizopita mbona imeishia kuwa ni kamba shingoni mwetu? IPTL imekuwa ni mfano wa kushindwa kwa nchi za Kusini mwa sahara, leo hii tena eti kuna mbunge anashauri tutumie PPP. Mbunge huyu anashangiliwa na JF tunatoa likes.

Kweli tunauwezo wa alayses? Tujiongeze.
 
shida ni pale tu mpaka mttu akikosa benefit ndio anakuwa na guts za kuyasema.otherwise mmmh!! Ila hongera zake kwa kusema haya.
 
You can't operate without sharing the national worth. Stable private sector will be instrumental in spearheading the industrial development we are looking for.
Tuache kubaguana na kuchaguliana....kama contractor wa uwanja wa ndege ni mzawa na rafiki...wote ni wazawa na marafiki. Tuwaendeleze wote. Vinginevyo naungana na Serukamba...tuamue moja ujamaa au ubepari.
 
Kaongea point sana, ila sasa shida inakuja kwa KOCHA!

Kocha kapanga 4-4-2
Wewe mchezaji unataka 5-4-1,
Kuna Mpira hapo?

Refer kauli hizi;

"Mimi huwa sipangiwi"

"Atakayeleta fyokofyoko kukiona"

"Serikali Yangu"

"Mawaziri wapumbavu"

"Mimi ni dereva wa Lori sisikilizi kelele za watu waliokwenye bodi"

NB; Huwezi Kujiokoa ukianza kuzama, tulia waje wengine wakuokoe, na ukineng'eneka zaidi utameza vikombe vya kutosha.
Kwa hiyo kujiokoa ni kuhamia chagadema?

Je manywele amejiokoa?

He nyala ndu amejiokoa au kajimaliza?
 
Anasahau kuwa ndege zetu tuliingia ubia na watu binafsi tukapigwa ATC iliyokuwa walau inapumua ikazimia kabisa .Nape alikuwa akibebwa tu kwa sababu ya jina LA babaake sidhani kama hata anajua ilani ya CCM inaongelea nini au anaijua hata inafananaje
Ni kweli tulipigwa mkuu, but sababu sio kwa kuwa ilikuwa chini ya sekta binafsi ( watu binafsi )ni sababu ya mikataba na usumamizi mbovu wa serikali yetu. Nafikiri hujamwelewa vema hoja yake anashauri kama serikali iweke mazingira mazuri ya sekta binafsi kufanya shughuli za uwekezaji wa miradi ambayo inaweza kujiendesha kibiashara. Nape ana hoja ya msingi sana kwa kwl na katimiza wajibu wake kama mbunge kuishauri serikali na sio kujifanya sehemu ya serikali kama wapuuzi wengine wanavofanya. Hakika ccm bado kuna watu wanaojitambua sana ....viva Nape!
 
Tunashangilia bila analysis!! Naamini michango yake bungeni ni kazi ya kusimuliwa. La maana angeweza kuiambia serikali isiwe overambitious. Lakini huwezi kunishawishi kwamba eti miradi ifanyike kwa kutumia private sekta. Private sekta ipi?? Iko wapi. PPP kwenye nchi hii kwa tawala zilizopita mbona imeishia kuwa ni kamba shingoni mwetu? IPTL imekuwa ni mfano wa kushindwa kwa nchi za Kusini mwa sahara, leo hii tena eti kuna mbunge anashauri tutumie PPP. Mbunge huyu anashangiliwa na JF tunatoa likes.

Kweli tunauwezo wa alayses? Tujiongeze.
Huyu mbunge anapayuka tu hana lolote , tumejaribu kuwapa hao private reli wahindi , umeme Iptl , ndege south africa wote walituingiza hasara tupu
 
Kaongea point sana, ila sasa shida inakuja kwa KOCHA!

Kocha kapanga 4-4-2
Wewe mchezaji unataka 5-4-1,
Kuna Mpira hapo?

Refer kauli hizi;

"Mimi huwa sipangiwi"

"Atakayeleta fyokofyoko kukiona"

"Serikali Yangu"

"Mawaziri wapumbavu"

"Mimi ni dereva wa Lori sisikilizi kelele za watu waliokwenye bodi"

NB; Huwezi Kujiokoa ukianza kuzama, tulia waje wengine wakuokoe, na ukineng'eneka zaidi utameza vikombe vya kutosha.
Miradi anayoifanya magufuli ni kukamilisha miradi iliyoshindikana kutekelezwa kipindi kilichopita kwa sababu hakuna wawekezaji waliojotokeza kufanya kwa sababu ya visingizio mbalimbali sioni ubaya kwa magufuli kutumia fedha za serikali kukamilisha iradi hiyo.hivyo nape anaota ndoto ya kushindwa
 
Leo hii mheshimiwa Nape Nauye ameeleza kwa kina jinsi ambavyo serikali inakosea katika mambo mengi sana, nape anasema Serikali imevaa viatu ambavyo sio saizi yetu. Nimependa sana Uzalendo wa Nape Nauye ... Hebu mtazame hapo chini alivyofunguka kisha toa maoni yako.

Rubbish!, Nape na masuala ya uchumi wapi na wapi!, analeta propaganda kwenye suala nyeti la uchumi!, Anafikiri yupo kwenye kampeni, nonsense!
 
Miradi anayoifanya magufuli ni kukamilisha miradi iliyoshindikana kutekelezwa kipindi kilichopita kwa sababu hakuna wawekezaji waliojotokeza kufanya kwa sababu ya visingizio mbalimbali sioni ubaya kwa magufuli kutumia fedha za serikali kukamilisha iradi hiyo.hivyo nape anaota ndoto ya kushindwa
Sawa. Wewe ni genius Mkuu kumzidi Nape.
 
Huyu mbunge anapayuka tu hana lolote , tumejaribu kuwapa hao private reli wahindi , umeme Iptl , ndege south africa wote walituingiza hasara tupu
yaani nape anajitoa ufahamu kifupi aelewe tu kuwa enzi za kubebwa kwa jina LA mzazi zimepita Ndani ya CCM it is either you are capable or not
 
Back
Top Bottom