Nape: Serikali ya awamu ya tano iheshimu sheria zinazopitishwa na bunge

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Dodoma. Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amemtaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuisaidia Serikali kujenga utamaduni wa kuheshimu sheria zinazopitishwa na Bunge.

Akizungumza bungeni leo Mei 22, 2018 katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii mwaka 2018/19, Nape amesema wakati wakikamilisha kuandaa taarifa ya kamati kuhusu bajeti hiyo, Wakala Huduma za Misitu Tanzania (TFS) walitangaza zabuni ya kukata miti katika pori la Selous.

Amesema ukubwa waliotangaza miti itakapokatwa ni kama ukubwa wa Jiji la Dar es Salaam na wapo wanaosema ukubwa huo unalingana na kisiwa cha Unguja, Zanzibar.

Amesema hifadhi hiyo ni kubwa nchini na kutangazwa kwa tenda hiyo kumeshtua.

Hata hivyo, amesema sheria ya usimamizi wa mazingira sehemu ya saba inatamka kuwa maeneo yatakayogundulika kuwa na madini na maji kufanyiwa tathmini ya mazingira kabla ya mradi kufanyika, lakini TFS imetangaza zabuni hiyo wakati tathmini haijakamilika.

Amesema tathmini hiyo ni muhimu kwa utambuzi wa hali halisi ya mazingira na jamii inayozunguka eneo husika: “Mwanasheria Mkuu wa Serikali aisaidie Serikali kujenga utamaduni wa kuheshimu na kwa unyenyekevu mkubwa naomba isitishe zoezi isubiri kwanza tathmini ya kimkakati ya kimazingira.”

Amesema msitu huo unazunguka na mikoa mitano ya Morogoro, Pwani, Lindi, Mtwara na Ruvuma na kwamba haiwezekani kupuuza jambo hilo.

Chanzo: Mwanachi
 
Nape na kundi lake wanapinga mradi wa umeme kwa manufaa ya nani?
 
Kutokuheshimu sheria huwa ni kaugonjwa kagumu sana kukaacha, na bahati mbaya awamu ya tano walikaanza mapema sana
 
Kuwa na akili kidogo basi hata uelewe alichozungumza nape.hii ndio shida ya kutumwa na akili zako ni zero.
ndo ccm walivyo kilsa wabunge wa ccm wakijitahidi kuishauri serikali wanawaita wasakliti wanataka waseme mazuri tu sasa serikali itajirekebishaje kama haitaambiwa matatizo ?
 
Sababu hizi zimekuwepo tangu enzi za Baba wa Taifa, kinachotakiwa hapa ni audacity
 
Nape na kundi lake wanapinga mradi wa umeme kwa manufaa ya nani?
Manufaa ya taifa kwa ujumla.

Kiukweli kwa sasa installed capacity ya TANESCO na vyanzo vingine mbali na Stigler gouge vinatosha nchi kwa zaidi ya miaka saba au kumi ijayo with no issue.
Ona matumizi ya TANESCO katika Gridi ya Taifa hayafiki hata Gigawati moja kwa sasa. Huwezi ukaamini baada ya saa tano usiku matumizi yanakuwa kama 0.5 ya Gigawati (500MW)
Tusije tukafanya tena mambo ya bomba la gesi tumekopa hela nyingi sana tukajenga bomba kubwa sana 36" la uwezo wa 750mmscfd na two gas plants (Songo Songo na Mtwara) lakini hadi saa hii matumizi yake ni kama 60mmscfd ambayo ni 8% ya kusudio lake. Pamoja na hayo haizuii wa TZ kulipa mkopo wa China EXIM Bank, mishahara kwa wazawa na wachina na gharama za uendeshaji. As such tunatoa hela hazina kuendesha mradi huu wa gesi badala ya kujiendesha na kupelaka hela hazina.
Wako wapi ma economists wa nchi hii hasa wa Ministry of Energy???????????
 
Nimekuelewa mkuu ila umeme wa gesi ni ghali sana kuliko maji. Pia mradi wa gesi ulikuwa white elephant, je unashauri tuendelee na gesi au stiegler gorge?
 
Maandamu tayari una miundo mbinu ya gesi (Already invested heavily in gas to power) hakuna haja ya kutumia hela nyingine nyingi kwa kitu ambacho unacho tayari!!!! 750mmscfd ni sawa na 3.75 GW (3750MW). Why should you spend money and destroying the nature of Serous and other livelihood for the sake of 2.1GW while you have 3.75GW at your figure tips?????????
 
Manufaa ya taifa kwa ujumla.

Kiukweli kwa sasa installed capacity ya TANESCO na vyanzo vingine mbali na Stigler gouge vinatosha nchi kwa zaidi ya miaka saba au kumi ijayo with no issue.
Ona matumizi ya TANESCO katika Gridi ya Taifa hayafiki hata Gigawati moja kwa sasa. Huwezi ukaamini baada ya saa tano usiku matumizi yanakuwa kama 0.5 ya Gigawati (500MW)
Tusije tukafanya tena mambo ya bomba la gesi tumekopa hela nyingi sana tukajenga bomba kubwa sana 36" la uwezo wa 750mmscfd na two gas plants (Songo Songo na Mtwara) lakini hadi saa hii matumizi yake ni kama 60mmscfd ambayo ni 8% ya kusudio lake. Pamoja na hayo haizuii wa TZ kulipa mkopo wa China EXIM Bank, mishahara kwa wazawa na wachina na gharama za uendeshaji. As such tunatoa hela hazina kuendesha mradi huu wa gesi badala ya kujiendesha na kupelaka hela hazina.
Wako wapi ma economists wa nchi hii hasa wa Ministry of Energy???????????

Kwani wanashaurika? Yeye alishazaliwa akijua kila kitu. Zigo zito haswa hili time will tell
 
Back
Top Bottom