Ukitaka kupata muktadha wa anachokisema Nape rejea maagizo ya serikali mwezi uliopita kuhusu michakato ya utekelezaji wa miradi nchini.
RAIS alitamka, siku anazindua mradi wa KINYEREZI TWO, kwamba hataki kusikia mradi wowote nchini unachelewa kwa vile eti kibali cha mazingira, au sijui cha Tanroads au cha EWURA hakijatoka.
Na ni hayo maagizo ndio yanatekelezwa sasa kwa kasi ya kutisha pale ambapo hatua za awali za mradi zinaendelea kabla ya kukamilika kwa ripoti ya tathmini ya athari kwa mazingira. Ni HATARI sana kwa nchi yetu. Next up watakuja watu hapa wanataka kuchimba Uranium kwa ajili ya miradi yao ya Nuclear (Iran walimtuma Vice President wao mwaka jana hapa na hatukuambiwa kafuata nini) na tutakubali kirahisi kwa sababu "tumeshachelewa sana," hatuwezi kupoteza muda na vimasuala vya environmental impact assessment.
Sheria zipo kutulinda, hatuna budi kuzilinda ili zituweke salama, serikali haipaswi kuwa kinara wa kuvunja sheria.