Nape: Serikali haioni haja ya kutunga Sheria ili iwe kosa kumkaimisha mtu kwa muda mrefu?

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye amesema tatizo la watu kukaimu nafasi kwa muda mrefu limekuwa kubwa, na kuhoji kama Serikali haioni haja ya kutunga Sheria ili iwe kosa kumkaimisha mtu kwa muda mrefu

Amesema, "Tutunge Sheria ifikie ukomo kwa mwisho wa kukaimu ni hapa. Mtu akipitiliza tuchukue hatua ili tuondokane na hili. Mtu anakaimu miaka 9 na hakuna mtu anachukuliwa hatua"

 
Huo ni uzembe tu wa mamlaka za uteuzi kama kuna mtu anaekaimu miaka 9, unatunga sheria ya kazi gani kumbana mtu wa aina hiyo ili itoe ukomo wa kukaimu, dawa yao hao wateuaji ni kujiuzulu tu wameshindwa kazi.
 
Wakurungenzi nchini wengi wanakaimu na hawana sifa. Mfano geita town council, Moshi manispaa, nape uko sawa.
 
Hili tatizo limekuwa kubwa sana, unakuta mtu anakaimu zaidi ya miaka 3+. Tatizo hili lipo sio tu Tamisemi bali hadi baadhi ya Taasisi za Serikali.

Na inapotokea mtu unamkaimisha, kwanza anakuwa sio huru kufanya maamuzi kwa kuwa ana wasiwasi wa nafasi yake kuipoteza.

Nadhani jambo hili waliangalie kwa jicho la karibu Ku rescue situation
 
Back
Top Bottom