Nape: Ruge alikuwa jasiri kwa kutaja hadharani watu waliovamia Clouds

Papushikashi

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
8,596
2,000
Nimemsikia Nape Nnauye wakati anahojiwa na clouds kwenye msiba amesema wakati Clouds imevamiwa aliongea na Ruge na kumuuliza kama ana ujasiri wa kuliongelea suala la kuvamiwa kwa Clouds , aliongea kuwa yeye haogopi na ataliongelea hadharani bila kumuogopa mtu yeyote.

Swali ambalo najiuliza ni kwanini hili suala amelifufua kipindi hiki ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
joseph1989

JF-Expert Member
May 4, 2014
6,735
2,000
Unafiki huu sijui TZ utaisha lini yeye mwenyewe kuwataja mafisadi na kukemea wenzake CCM anashindwa,hapo kaongea ili mradi aonekane.Kipindi kile yy alikuwa kimbele mbele kuzuia bunge lisirushwe live na goli lake la mkono.
 
Nyaka-One

JF-Expert Member
Oct 27, 2013
3,571

Naona na wewe uko kama mimi kwa kuwa nyuma katika kujua mambo yanayoendelea hapa nchini. Hata hivyo kwa upande wangu nilibahatika kumsikia kiongozi mkuu kabisa akisema hadharani kwamba ni yeye aliyezuia bunge kutoonyeshwa live.
 
Kwa nini hakumkemea au basi hata kumshauri,manake hata yeye alikuwa anaunga hoja,bunge lisiruke live.Kuwa mwanaharakazi ni kazi ngumu sana unatakiwa uongee bila kuogopa chochote wala kumuogopa mtu yoyote as long huvunji sheria za nchi,kinyume chake utabaki kuwa mnafiki kama Nape.
 
Kwani Nape ni mwanaharakati? Pamoja na yote lakini angalau kwenye huo uvamizi wa Clouds Nape hakuwa mwoga.
 
joseph1989

JF-Expert Member
May 4, 2014
6,735
2,000
Kwani Nape ni mwanaharakati? Pamoja na yote lakini angalau kwenye huo uvamizi wa Clouds Nape hakuwa mwoga.
Hana unaharakati wowote anatapatapa sababu kanyang'anywa tonge mdomoni,wewe jiulize kafulila una msikia siku hizi?.
 
M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
12,525
2,000
Kunamatukio tulitarajia kuwafahamu wasiojulikana. Lakini Ni matukio mawili tu yaliwekwa wazi na watendewa.

1. Clouds tuliwaona live, hongera Ruge kwa hili
2. Tukio la kuvamiwa zakaria mfanyabiashara Musona alipowalamba risasi maafisa usalama.

Tafadhali Roma Na MO tunasubili ushuhuda wenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
umewasahau wale triger-happy wa Lissu..
hawa nao wanajulikana kwa kauli zao za sasa!
 
Nyaka-One

JF-Expert Member
Oct 27, 2013
3,571
2,000
Hana unaharakati wowote anatapatapa sababu kanyang'anywa tonge mdomoni,wewe jiulize kafulila una msikia siku hizi?.
Unavyoona alipoamua kufuatilia lile tukio la uvamizi hakujua kuwa gharama yake inaweza kuwa ni kunyang'anywa tonge mdomoni na kujiweka tayari kwa hilo?
 
joseph1989

JF-Expert Member
May 4, 2014
6,735
2,000
Unavyoona alipoamua kufuatilia lile tukio la uvamizi hakujua kuwa gharama yake inaweza kuwa ni kunyang'anywa tonge mdomoni na kujiweka tayari kwa hilo?
Kaka unaoneka wewe mgeni wa wanasiasa wa Tanzania,tupo ngojea siku apewe cheo ndio utaona upuuzi wake Ref Masha kakosa ubunge akawa mwanaharakati na chama kahama,leo karudi CCM sijui kapewa cheo gani kelele hatusikii tena,mwisho wa siku kawaharibia wenzake akina Mbowe.Mimi mwenzio wanasiasa wa TZ kauli zao sizitilii maanani hasa wa CCM sababu wengi ni wanafiki.
 
Papushikashi

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
8,596
2,000
Kwamba wengi wasingeweza kulisema lakini Ruge alikuwa na ujasiri wa kusema hadharan....hii ina maana kwamba kuna watu wanafanyiwa mambo ya kuonewa lakin bado wanakaa kimya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom