Nape rudi nyumbani Mtwara tunakuhitaji uwe Mbunge wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape rudi nyumbani Mtwara tunakuhitaji uwe Mbunge wetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pasco_jr_ngumi, Mar 10, 2012.

 1. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Mkuu Nnape,
  Pole na majukum ya kazi ya Chama chetuu cha CCM. Mimi niko huku nyumbani Mtwara. Nimefanya uchunguzi nikagundua kuwa ww ni mwana we kwetu, ikaniuma sana kuona ukipata tabu pale Ubungo wakati ungekuja hapa Tandahimba ungekuwaa Mbunge kiurahisi zaidi.


  Tatizo:
  Namlaumu mzee Nnauye kwa kukufumba macho na kushindwa kukuleta huku ukuliee kwani tungekujuwa kwa urahisi zaidi. Kwenu pale Chiuta karibu na Luagala na Litehu, looo!!

  Lakini hili ni tatizo la wasomi wengi wa kusin, najuwa wako wengi sana wakitoka kimaisha wanapotea kabisa. Hebu angalia mtu Kama Saidi Kalembo wa Nachingwea kule Mpiruka kijijin cjuw Mara ya mwisho kwenda ni Lini. Mains wa Mh. Ng'itu ilikuwa shida tupuuu . Kijijin hakuwa nyumba na ikalazmu ijengwe kwa haraka ndani ya cku 10.... Aibuuuu.

  Hali ya huku ni aibu tuu, wasomi hawarudi nyumbani wao ni kutokomea huko mijiniiii. Hata Hawa wabunge wetu wote wa kusin hawaonekani kwani Hata makazi hawana makazi huku, looo

  Hongera;
  JK alipokuchagua kuwa mkuu wa wilaya Masas ulifanya jitihada zako binafs kujua nyumbani. Najua uliwnda pale Chiuta ukatafuta ndugu zako, wajomba, na dada kwa kaka zako. Nafikiri ni mwanzo mzuri. Usiachie hapo uwe unaenda Mara kwa Mara Hata kila baada ya miezi mitatu.... Then, jenga kinyumba kadogo, nunua shamba la mkorosho, that's good look, watakujuwa kweli ww ni mzawa....

  Changampto za nyumban (jumbo la Tandahimba)
  Hadi Leo hakuna Mbunge wa kuliendesha jimbo na kuleta maendeleo. Mh.njwayo, CCM kakimbia kabsa baada ya kushinda kwa udanganyifu.... Hana strategy za kuliongoza jimbo... Ndio walewale wachumiaa tumbo!!

  Mh. Katani
  Huyu ni kijana wa CUF mropokaj, muongo, asiye na elimu ambaye anakubalika kwa mbwembwe zake. Ukianza harakati za kuja huku uwe Mbunge, ni rahis kummaliza kisiasa na kulichukua jimbo. Mi kwetu ni Mtwara Vijijin najua ni namna gan nitalitwaa jimbo Kwan Mh. Hawa Ghasia kashndwa kuwaongoza watu kujikomboa katika umaskini.

  Chonde Chonde Chondeeee!!!!!!!
  Mtwara itajengwa na vijana wa Mtwara, Njoo tusaidiane kuleta maendeleo. Kasi ya kukua kwa uchumi ni lazima kuwe na viongoz thabiti wa kusismamia mali za umma zisiibiwe. Tunachmba mafuta, gas, korosho zinalimwa, Mto Ruvuma Upo, bandari kubwaa ipo!! Njoo tusaidiane pale alioacha Dr. Mkapa, Mh. Dr. Mtavala, Mh .Sijaona Nangwanda tuijenge Mtwara yetuuuuuu

  Ahsante
  PJN
  Ncholi Village, Mtwara.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,475
  Likes Received: 19,866
  Trophy Points: 280
  mzee wa vipaji kibao..big up!
  Akimudu vilivyo gitaa la Solo.jpg Akipapasa Kinanda.jpg Nape Nnauye akipiga Drums huku Msafiri Diouf akiimba (1).jpg
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Mar 10, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,475
  Likes Received: 19,866
  Trophy Points: 280
  kaka huko kwenu hakuna uchawi na mambo ya kulogana kisa eti mtu kasoma ama kanunua gari? haya ndio hukimbiza watu.
   
 4. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Mbona Mimi nimesoma na kijijini kwangu wananipenda??? Uchawi ni sumu za mitishamba, unawekewa kwa chakula!! Hakuna Uchawi weweeeeeeee!!!!
   
 5. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #5
  Mar 10, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Bwana PJN, Barua yako hii ni ya mpiganaji na mzalendo halisi wa kusini. Unaipenda nchi yako kwa moyo wako wote na kwa mapenzi yako yoote umejitoa kuhakikisha kuwa unabakia kuwa na sifa ya mpiganaji wa msituni wa ndani ya ardhi yako tukufu.

  Wito wako si kwa Nape pekee bali ni kwa watu wote aina ys Nape. Wote wenye karama na vipaji kama vya nspe kuwa warudishe uwezo wao waliopewa na Mungu kwa alili ya kuijenga kusini yenu.

  Ni kweli kusini kila kitu kipo. Upungufu wake ni kukimbiwa na watu wake hasa wasomi. Hii ni bahsti mbaya kwa Kusini. Bahati nzuri Mungu amekuweka wewe kuwa sauti ya mtu aliye nyikani, wito wako ni wana kusini warudi kuijenga kusini.

  Ugenini hakuna heshima kama mtu hakumbukagi kwao. Ishi kwa mfano Dar, lakini hakikisha pia unaishi kusini. Ishi Dar, jenga kusini.

  NIKO PAMOJA NAWE, MHESHIMIWA NAPE NENDA KUSINI KAIMARISHE CHAMA KULE KUWA USIPOENDA CUF NA SASA NCCR WANAKIMOMONYOA KWA KASI CHAMA RAFIKI NA CHAMA DAMU KWA WATU WA KUSINI CHAMA MAPINDUZI.

  NAUNGA MKONO HOJA.
   
 6. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #6
  Mar 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,288
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Nape kwao sio Mtwara ni Nyangamara Lindi vijijini, cheki data zako kwa usahihi.
   
 7. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #7
  Mar 10, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Ivi nape sio mnyaturu? Umempa vizuri coz kama anataka kuwa mbunge labda ubungo igawanywe.
   
 8. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #8
  Mar 10, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,309
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  Hivi Nape keshawahi kuishi Ntwara? Au ni mahali tu Baba yake alitoka? Je, alikokulia siyo kuwa ndo home kwao? Mi nahisi Ntwara ni kwa kina mzee Moses Nnauye na si kwa kina Nape, kama hakukulia huko lakini.
   
 9. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #9
  Mar 10, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Bah! Chukulubu unatakiwa nyumbani kugombea ubunge kuntoa cafu. Chacha wachemaje njomba?
   
 10. B

  Buto JF-Expert Member

  #10
  Mar 10, 2012
  Joined: Sep 23, 2011
  Messages: 249
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  JPN umefanya vizuri kumkumbusha nape arudi kusini. Wasomi wengi wa kusini wamekimbia makazi yao na kutelekeza ndugu zao. Si una mkumbuka mbunge wa jimbo la Ruangwa marehemu Ng'itu alivyokuwa anakula bata Dar na kusahau kijijini kwao?NAPE RUDI KWENU KUSINI CHINGA WENZAKO WANAKUHITAJ USAIDIE KUSUKUMA GURUDUMU LA MAENDELEO. NAPE MKATAA KWAO NI MTUMWA
   
 11. samilakadunda

  samilakadunda JF-Expert Member

  #11
  Mar 10, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 1,701
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Makonde ndoo tabia yao,wanatakiwa kufundindishwa na kujifunza kwa wachaga,kwani wengine wanakana hata kabila lao.angalia mkapa kakimbia kwao anaishi lushoto Tanga hii nilaana amewajengea daraja iliwavuke kiurahisi wahame kwao.poleni ndugu zangu.
   
 12. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #12
  Mar 10, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sio kweli kwamba daraja lilijengwa ili tuhame kiurahisi bali tusafiri kiurahisi kutafuta bidhaa na vitu mbalimbali ili kuweza kujiletea maendeleo ya haraka zamani vitu vilikuwa bei juu(abnormal prices) kwa sababu ya usafiri wa tabu siku hizi nafuu ipo.Kwahiyo mkuu usipotoshe madhumuni ya Mkapa Bridge.Kusini inakua kwa kasi na ndani ya muda mfupi wasomi watamiminika kuusaka ubunge na kujiletea maendeleo, japo changamoto hazikosekani lakini tunakabiliananazo.
   
 13. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #13
  Mar 10, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Samahani mkuu kama nitakukwaza...

  Kwanza nikupongeze kwa kumhimiza mtu wa kuzini mwenzako kurudi na kugombea ubunge...

  Na pia,Nape ni kweli asili yake Chiuta,lakini Chiuta iko Lindi Vijijini,kwenye Tarafa iitwayo Nyangamara..
  Kwa hiyo basi,umshauri arudi agombee jimbo lake,lakini la Tandahimba,ni kwamba limepakana tu na kwao...

  Jambo jingine,alichouliza St Ivuga,kama kweli we wa kusini na umekulia kusini usimshangae yeye kuuliza swali hilo..
  Ila,kwa kadri ya uelewa wangu,mambo ya uchawi na kulogana yapo kusini,lakini si ya kuoneana kijicho kwamba fulani ana nini,hayo kwa Mkoa wa Mtwara yamepungua..

  Watamloga anayeiba mke wa mtu,na mwizi sanasana. Ila,with exception of Nyangamara,specifically Chiuta!!
  Huko mzee hakufaii.. Sehemu ni nzuri,zahanati ya muda mrefu,jengo la mahakama,shule ya sekondari ya muda mrefu..
  Majengo mengi hayo ni magofu kwa sasa.. Watumishi wakifika kuanza kazi,hawamalizi mwezi,wanarudi kuokoa maisha yao!

  Hujamkosea mtu hata mmoja,utaingiliwa usiku ndani na mwanaume au mwanamke kutegemea jisia yako,kujikuta umelala na nyoka,ndoto za ajabu,kujikuta umelala nje ya nyumba,n.k

  Wengine huuwawa! Mfano Mahakimu.. Fanya utafiti utaifahamu hii.

  Kwa hiyo hoja ya Saint,usiitupilie mbali kirahisi..
   
 14. e

  ebaeban JF-Expert Member

  #14
  Mar 10, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 1,834
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Edu . Kumwembe anajitahidi sana kurudi kwao Mtwara, hua ninamwo mala nyingi pale mdule mkubwa hata pale kwao Chimbuli ,Mikindani kwa juu, lakini siyo Nape. Hao wawili wasaidiane basi kuipaisha Mtwara ambayo sasa imefunguka.
   
 15. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #15
  Mar 10, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Namsubir Nape ajitokeze ili nirud jamvini kuchangia
   
 16. k

  kuzou JF-Expert Member

  #16
  Mar 10, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  alikua mbunge kwao na amewatumikia vya kutosha kwa miaka kadhaa,wengi wameamua kuishi dar,mkapa kuishi lushoto hamna shida
   
 17. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #17
  Mar 10, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,736
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  la msingi pia angeacha hizi porojo za ukatibu uenezi wa ccm akafanye ile kazi yake ya ukuu wa wilaya kwa huu muda uliobaki then 2015 agombee jimboni mwake hapo atakuwa ashajenga mazingira mazuri lakini kwa sasa naona yuko dar anakula posho za vikao na safari sijui yale majukumu yake ya ukuu wa wilaya kule masasi nani anayasimamia.
   
 18. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #18
  Mar 10, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Nimeipenda hiii......iwe kwao Lindi au Mtwara sawa maadam ni kusini ...........sikia kilio cha watu wako nenda kawakomboe.....ukiwa bado unakubalka kaskazini................usisubiri uchokwe ndo uende.....safi sana najua utajitokeza hapa kunjibu ntoa mada.
   
 19. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #19
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Nimependa komenti zenu wakubwaa... Mi ctoki huku..... Moshi nimeishi 4 yrs, songea 3 yrs, dar hom ndogo..... I am happy here at hom Ntwara!!!!!!!!!
   
 20. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #20
  Mar 11, 2012
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,399
  Likes Received: 1,524
  Trophy Points: 280
  ..........huyu jamaa made in Mbeya, hamna cha Mtwara wala nn, labda jina ndilo la mtr.. zameni vizuri data zenu
   
Loading...