NAPE: Rais Kikwete hashinikizwi kufanya maamuzi juu ya ESCROW

Hii ishu imemkalia vibaya sana huyu mzee,manake navyoona mm uamuzi wowote atakao utoa utakuwa na madhara,ngoja tuone manake mpaka mtu uwe rais tena wa watu weusi unakuwa umeshakuwa exposed na fitna za kila aina.
 
...Uamuzi wa bunge ni uamuzi mzito unaopaswa kuheshimiwa na si rais tu baili serikali pia. ..

Tatizo lililopo ni kwamba ule ulikuwa ni USHAURI tu. Bunge letu halina kibari wala uwezo wa KUMUAMURU Rais afanye maamuzi, hata kama kuna ushahidi ''beyond doubt'' kwamba kuna maovu yamefanyika. Rais anaweza kuomba USHAURI mwingine kwa akina Werema kwa jambo hilo hilo, na akaamua kuutupilia mbali USHAURI wa Bunge na kuamua vinginevyo, based na USHAURI kutoka upande mwingine

Wananchi tuikatae rasimu ya katiba iliyochakachuliwa na kupendekezwa upya na akina CHENGE; na wananchi (kupitia BUNGE) tupewe uwezo wa KUMUAMURU Rais kufanya maamuzi kwenye mambo ya msingi, ikiwemo uwajibikaji
 
Shinikizo lipo kwa wafadhili walozuia mapesa Yao.tukubali Kama nchi tumekwama na Maamuzi ya haraka yanahitajika.Inawezekana tukawa tunawapenda sana kina Muhongo lakini ndo tumefika njia panda hatunabudi tuchague maslahi ya nchi.
 
Hope unasikiliza habari za nchi zingine. Nina maana ya nchi. Waziri wa usalama wa Raia na mkuu wa Polisi Kenya wamejiuzuru kwa sababu ya Al Shaabab kuua wasafiri na ktk machimbo ya kokoto, nje kabisa na Nairobi. Huko Mandera. Kwa nini wakenya wawe na akili sisi iwe ni zero? Ni elimu duni au ufahamu duni kama huu wa kwenu?

Munamuona Rais kama muumba vile! kwamba bila yeye hakuna uhai!

Angalieni,huo utafiti wa chumbani na akina Shonza Juliana ni Pepo,njoo upate maoni ya watu mtaa kwa mtaa,mtu akipata kashfa unasubiri Masia?
 
Asipowang'oa hao kisiasa , atang'olewa Pinda.
Na bunge linauwezo wa kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais.
 
My take: Hivi inawezekana kweli akina Werema, Muhongo na Maswi wakapeta maana Kikwete anaweza asiufuate ushauri wa Bunge? Sasa inaonekana akina NAPE wametumwa kufanya ''utafiti'' na kupima upepo; na sasa wanadiriki kusema kwamba wananchi hawalifuatilii tena suala la Escrow....Upepo umeshapita![/COLOR]

Huyu NEPI nafikiri ana matatizo ya akili, mbona anapingana na kauli zake mwenyewe, kweli ccm imepoteza mwelekeo na inaishi kwa ujinga wa watanzania,ujinga wetu ndiyo mtaji wa ccm kwa sasa
 
Wanasiasa wanashangaza kweli. Kwa hiyo kwa mujibu wa Nape Rais angefanya tu kama kungekuwa na tishio la chama kukosa ushindi 2015! Hii kwa maana ingine ni ruhusa kwa watendaji na wanasiasa kufanya makosa ya makusudi kuruhusu wizi na ukwepaji wa kulipa kodi ikiwa tu hautaathiri mawazo ya wananchi katika kukipigia kura chama. Ndiyo maana wanasiasa wanakwepa kulipa kodi na hawaoni kama ni tatizo isipokuwa tu wanapohusika watu wengine!

Kingine kinachonishangaza katika kauli ya Nape ni kusema kuwa mfumo mbaya serikalini ndiyo uliotufikisha hapo na kuwa kila mara kukitokeza tatizo waziri anawajibika lakini watendaji wanabaki na mfumo hauangaliwi. Kauli hii ingekuwa na mantiki kama nchi yetu ingekuwa imeshatawaliwa na chama tofauti na kilichopo madarakani sasa na kuuweka mfumo huu unaolalamikiwa na Nape. Ni ajabu pia kuwa Katibu Mwenezi atoe kauli hii wakati akijua kuwa wengi wetu tulipendekeza na kuunga mkono kutenganisha mihimili ya dola na hasa kwa hapa, mawaziri kutokuwa wabunge. Mantiki ya hili pendekezo ni kuwafanya mawaziri wasiwe sehemu ya siasa na wawajibike kusimamia wizara zao kitaalamu. Ni chama chake ndicho kilipigania kuacha mfumo wa sasa anaoulalamikia kuendelea - status quo.
 
Huyu NEPI nafikiri ana matatizo ya akili, mbona anapingana na kauli zake mwenyewe, kweli ccm imepoteza mwelekeo na inaishi kwa ujinga wa watanzania,ujinga wetu ndiyo mtaji wa ccm kwa sasa

Anachokiona Nape ndicho alichokiona David Cameroun kwa wanaume wa Kitanzania ndio maana akashauri nao wanaweza kuolewa pia maana hakuna uanaume ndani yao, kabla ya Kagame kwenda mbali zaidi na kutufananisha na wafu.
Tumekuwa waoga mno! Utadhani Mkwawa, Kinjeketile, Mangi Meri walitokea nchi nyingine.
 
Vilaza kazi yenu kupiga kelele tu pelekeni watoto shule wapate elimu wasiwe kama nyinyi mibichwa mikubwa tu leo hii bado ccm wanashika hatamu sababu hamna akili jipangeni
 
Eti wananchi hawafuatilii??!!!
Hii ni qualitative au quanti??!!
Saturation ilifikia n ikiwa ngapi na N ikiwa ngapi??!!

Hii nchi iko mikononi mwa baashi ya watu wepesi sana!!!
 
Usithubutu kukutwa na hili jubwa jinga..... wakati linabwabwaja.

Hata kama ulikuwa msafi itakubidi ukaoge tena.

Lol
 
Ole Sendeka alieleza kitu kizuri kwamba tatizo bunge letu halina kamati ya kudumu ya kufuatilia maazimio yake, lakini alikuwa amechelewa na hakuna aliyemsikiliza. Hali itaendelea kuwa kama ilivyo ya kusema "Rais hashinikizwi" au "tatizo ni mfumo". Maana halisi ya bunge kuisimamia serikali ni ipi?

Mtakumbuka tangu mwanzo wanaCCM wengi hawakutaka kabisa suala la kuwawajibisha hao jamaa, kwa hiyo kwa namna yoyote wataendelea kutetea msimamo wao wa tangu mwanzo.

Nawasifu wabunge wa upinzani kipindi hiki hata walipoona adhabu inapangwa na mmoja wa watuhumiwa hawakutoka nje ya bunge kama ambavyo wamekuwa wakifanya kipindi cha nyuma walipokuwa wakichakachuliwa, walisimama wakaanza kuimba nyimbo za kutiana hamasa bila kutoka hadi mama makinda alipoahirisha bunge na likaendelea kesho yake. Wangetoka ingekuwa nafasi nzuri kwa upande wa pili kujipangia mambo yao kwa masilahi yao wenyewe. Naona hii mbinu ya kukatalia mle ndani na kupoteza utulivu ni nzuri zaidi ya kushinikiza mambo yenye masilahi kwa taifa.

Nashauri, kama maazimio ya bunge hayatatekelezwa, katika vikao vijavyo vya Bunge waingie bungeni kama kawaida lakini wasikubali kumsikiliza waziri yeyote (wapoteze utulivu) hadi siku maazimio ya bunge yatakapotekelezwa. Hiyo ndiyo njia pekee ya kuishinikiza serikali kutekeleza maazimio ya bunge.

Ikumbukwe kwamba wabunge ni wawakilishi wa wananchi, hivyo maamuzi ya Bunge ni maamuzi ya wananchi milioni 45.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom