NAPE: Rais Kikwete hashinikizwi kufanya maamuzi juu ya ESCROW

Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
9,181
2,000
Dar es Salaam. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema watu wanaomshinikiza Rais Jakaya Kikwete kutoa uamuzi haraka kuhusu watuhumiwa wa escrow, wamepotoka kwa kuwa Bunge lilitoa mapendekezo na siyo shinikizo.

Kauli ya Nape inakuja siku chache baada ya baadhi ya watu wakiwamo wanasiasa kuhoji ukimya wa Rais Kikwete kuwachukulia hatua mawaziri na viongozi waliotajwa kuchota sehemu ya Sh306 bilioni kutoka Akaunti ya Tegete Escrow ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Katika mapendekezo yake, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (PAC), iliviomba vyombo vya uchunguzi kufuatilia kama viongozi hao wa umma, walifuata matakwa ya sheria na hatua kali zichukuliwe kama itabainika kuwa hawakufuata, ikiwa ni pamoja na kuvuliwa nyadhifa zao za kuchaguliwa au kuteuliwa, kufilisiwa na kufikishwa mahakamani.

Akizungumza jana, Nnauye alisema utafiti alioufanya amebaini kuwa wananchi hawalifuatilii suala la escrow kama linavyoandikwa kwenye vyombo vya habari na kwamba hata kama Rais Kikwete hatawawajibisha wahusika CCM haitatetereka kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

"Rais hafanyi kazi kwa shinikizo la watu, anafuata sheria na Katiba ya nchi. Wanaoshinikiza wamepotoka, Bunge lilishafanya kazi yake, halikushinikiza lilipendekeza wahusika wachukuliwe hatua," alisema Nnauye.

Kiongozi huyo alisema kinachofanyika hivi sasa ni baadhi ya watu kutumia vyombo vya habari kulikuza suala hilo, wakati mfumo mbaya serikalini ndiyo uliowafikisha viongozi hao mahali walipo.

"Mara nyingi waziri amekuwa akiwajibishwa bila kuangalia mfumo uliochangia. Unakuta katibu mkuu anakuwa na nguvu sana kuliko hata waziri, lakini mambo yanapoharibika waziri ndiye anayewajibishwa," alisema.

Aliongeza: "Hata kama tungemleta malaika kutoka mbinguni, kama mfumo hautabadilishwa hataweza kufanikiwa, ndiyo maana chama kimekuwa kikishauri uwajibikaji."

Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila alisema kauli zinazotolewa na CCM zinaonyesha kuwa chama hicho kimepoteza udhibiti wa Serikali, kwa kuwa haiwezekani maoni yanayotolewa na chama tawala yakapingwa na viongozi serikalini.

"Hakuna uhalali wa kuendelea kuwa chama tawala kama hawasikilizani. Serikali kutofanya uamuzi ni udhaifu wa chama, lakini Rais anapogoma kuchukua hatua ndiyo uhusika wa Ikulu katika hili unathibitika," alisema Kafulila.

Mbunge huyo ambaye amekuwa kinara wa kulifuatilia sakata hilo, alisema ili ukweli ubainike kwa nini Serikali inasitasita kutekeleza mapendekezo ya Bunge, ipo haja ya kuwekwa hadharani Ripoti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) iliyochunguza kuhusu uchotwaji wa fedha za escrow.

"Taarifa za akaunti ya Stabic iliyopo kwenye ripoti ya Takukuru ikiwekwa hadharani nchi itatikisika, ina majina ya wakubwa," alisema.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Mstaafu Amir Manento alisema haki inatakiwa kutendeka bila kuhusisha hisia wala itikadi za uhasama wa kisiasa.

Hata hivyo, Manento alisema kuwajibishwa kwa viongozi hao kutategemea msimamo wa Rais Kikwete kutokana na muundo wa serikali ulivyo.

"Niliwahi kutoa mapendekezo yangu kwenye katiba kwamba, mawaziri wasiweze kuwa sehemu ya Bunge lakini haikuwezekana, hali hiyo inachangia viongozi wa Serikali kutowajibishana," alisema na kuongeza:

"Watuhumiwa ambao ni mawaziri wanakuwa sehemu ya Bunge, halafu wakati huo huo wanashiriki vikao vya mawaziri kwa ajili ya kutolewa uamuzi kupitia kwa mwenyekiti wake ambaye ni rais, na hao hao ndiyo wanaokaa kwenye Kamati Kuu ya CCM."

Akizungumzia suala hilo, Profesa Gaudence Mpangala wa Chuo Kikuu cha Ruaha (Ruco), alisema kauli zinazotolewa na CCM ni za kujihami.

"Hao wanatafuta lugha za kujihami kwa sababu wameingia kwenye sakata hilo wanafahamu kwamba linaweza likawaadhiri," alisema Profesa Mpangala.

Aliongeza: "Ndiyo maana hata wakati sakata hilo lilipokuwa linajadiliwa bungeni Katibu Mkuu wa CCM (Abdulrahman Kinana) na mwenzake Nape Nnauye walikuwa Mtwara.

"Walikuwa wanashinikiza kwamba hao wanaohusika na sakata hilo ndiyo wachukuliwe hatua za kinidhamu na za kisheria kwa sababu hilo suala ni la watu binafsi na wala si la chama."

Aliongeza kuwa, kwa kuwataka wananchi wasiwe na haraka kujua hatua zilizochukuliwa, wanaonyesha dhahiri kuwa wako katika hali ya kujihami kutokana na kwamba dhambi hiyo imetendwa na viongozi wao.

"Wanataka kuonyesha kwamba kashfa haihusiani na CCM jambo ambalo si kweli kwa sababu hiyo ndiyo serikali ya chama tawala, kwa mfumo wetu ni kwamba chama kinachoshinda ndicho kinachounda Serikali na wale wenye kashfa wote ni wana CCM kwa hiyo hawawezi kukwepa hilo. Kwa namna yoyote ile hili lazima litawaadhiri," alisema na kuongeza: "Hiyo inaonyesha dalili kwamba CCM ndiyo chimbuko la kashfa zote za ufisadi na rushwa."

Alibainisha kuwa, kashfa kama hizi zinaibuka wakati wa maandalizi ya uchaguzi kutokana na kwamba fedha zinazochotwa ni kwa ajili ya kazi hiyo.

Alisisitiza kuwa jambo lolote linalozungumzwa na wabunge ni la wananchi, hivyo kama wawakilishi hao wanataka kujua hatua zitakazochukuliwa na serikali wanahoji kwa niaba ya watu waliowachagua.

"Wabunge si ndiyo wawakilishi wa wananchi na wao si ndiyo wamelivalia njuga suala hilo kwamba lazima wahusika wachukuliwe hatua, sasa hao wananchi wanaosemwa hawana haraka na hao watu kuchukuliwa hatua ni nani?

"Wananchi wenyewe ndiyo sisi, tunashangaa rais tangu arejee kutoka kwenye matibabu amekaa kimya, kwa nini hatekelezi maazimio yale nane ya Bunge?" Alihoji Profesa Mpangala.

Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bashiru Ally alisema hayo yanayojadiliwa hivi sasa yapo kwenye mfumo uliokumbatiwa na vyama vya siasa.

"Huo mfumo siyo wa CCM tu ni wanasiasa wote… Ukishakumbatia mfumo wa ubepari uchwara mtapata matatizo tu na mtabaki mnajadili matatizo tu.

"Ndiyo maana hata Zitto Kabwe alisema hata kabla hilo yalijamalizika kuna kashfa nyingine nne na ataendelea kufichua kashfa hadi mwisho wa maisha yake ya siasa kwa sababu mfumo wenyewe unazalisha kashfa," alisema Ally.

Makamu Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe alisema, "Hatuna mamlaka na mawaziri, siyo kwamba hatuwawezi ila ni wadogo sana kwetu. Sisi tuna mamlaka na rais na waziri mkuu.

"Kimsingi Bunge kusisitiza hilo ni kwa nia njema…, watafanyaje kazi na Bunge wakati limesema halina imani na wao? Kimsingi aliyetoa wazo ni mshauri tu. Sasa ni suala la uungwana ndilo lililobaki," alisema Filikunjombe.


Chanzo
: Gazeti la MWANANCHI


My take: Hivi inawezekana kweli akina Werema, Muhongo na Maswi wakapeta maana Kikwete anaweza asiufuate ushauri wa Bunge? Sasa inaonekana akina NAPE wametumwa kufanya ''utafiti'' na kupima upepo; na sasa wanadiriki kusema kwamba wananchi hawalifuatilii tena suala la Escrow....Upepo umeshapita!
 

mjepo

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
4,917
1,225
Hakuna mahala watu kama muhongo wamehusika kilichopo hapa ni chuki za kisiasa kwa kumchukia muhongo kutokana na msimamo wake kwenye nishati na madini.
 

win8

JF-Expert Member
Nov 13, 2014
926
250
Prof Muhongo alisema ikibidi kujiuzulu au kuuzuliwa basi ardhi ya Tanzania itatikisika maana yake hapa ni kwamba kuna wakubwa zaidi atawataja kushiriki kwenye mgao wa Escrow. sasa JK anahofia hilo.
 

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,871
2,000
Nakubaliana na msimamo wa Nape. Rais ni mkuu na ukuu wake haushinikizwi kwa maslahi ya kisiasa
 

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,448
2,000
Nape funga hilo domo lako, tunajua uliomba kazi ukapewa uDC, baadaye huo ukasuku wako na ukatulia, nyamaza huna msaada kwa waTZ zaidi ya tumbo lako. Nchi sio ya mama yake wala ya babu yako usime umemgawia, tunaibiwa fedha harafu unasema rais hashinikizwi, kwa ufupi sana anashinikizwa na kuwajibika kwa wananchi. Mdanganye kasuku wewe vile una njaa na mali, usitumlaumu sie mlaumu aliyekuleta duniani akakuacha maskini wa akili na mali pia
 

MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
3,698
2,000
Rais hafanyi kazi kwa mashinikizo bana kila anachofanya hufuata sheria siyo kuonea watu.
Semeni Rais hakuna kitu. Uwezo wake ni mdogo sawa na mtoto anayekaa uchi bila hata kujali. Binadamu aliye na akili komavu hahitaji kuambiwa na Bunge. Hasira ya kawaida tu bila hata kuwa Rais lazima ikufanye mtu uchukie mabaya, iweje huyu Prof. J hajui afanye nini!

Ndo maana nimekuwa na hisia kwamba labda huko US amehasiwa na sasa haamini itakuwaje kwa kamchezo alikozoea?
 

laticka

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
347
225
Nape funga hilo domo lako, tunajua uliomba kazi ukapewa uDC, baadaye huo ukasuku wako na ukatulia, nyamaza huna msaada kwa waTZ zaidi ya tumbo lako. Nchi sio ya mama yake wala ya babu yako usime umemgawia, tunaibiwa fedha harafu unasema rais hashinikizwi, kwa ufupi sana anashinikizwa na kuwajibika kwa wananchi. Mdanganye kasuku wewe vile una njaa na mali, usitumlaumu sie mlaumu aliyekuleta duniani akakuacha maskini wa akili na mali pia
---- mkubwa Nape Nnauye
Kwanza nikimuona nachukia CCM Mara milioni
 

Kiby

JF-Expert Member
Nov 16, 2009
6,070
2,000
Hakuna mahala watu kama muhongo wamehusika kilichopo hapa ni chuki za kisiasa kwa kumchukia muhongo kutokana na msimamo wake kwenye nishati na madini.
.
Kuwajibika sii lazima uhusike.
Kuhusika ni kosa la jinai na hivyo kinachofuata ni kuburuzwa kwenye makama cha kisheria.
Kuhusu rais kushinikizwa, sii tu kwamba anashinikizwa kutekeleza maamuzi tu bali pia anaweza kushinikizwa kuachia ngazi na marais wengi tu wameondolewa kwa njia hiyo.
Nape ni kama kiziwi na kipifu kwa pamoja.
.
 

MUSSA ALLAN

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
18,939
2,000
Narudia tena. Nitashangaa sana, Rais Kikwete akitengua uamuzi wake wa kumteua Prof.Muhongo kwa kushinikizwa na wanasiasa wenye chuki dhidi ya Muhongo!
 

mzamifu

JF-Expert Member
Mar 10, 2010
4,896
2,000
Ni kweli raishi hashinikizwi lakini bunge lina nafasi yake na linaweza kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais. Uamuzi wa bunge ni uamuzi mzito unaopaswa kuheshimiwa na si rais tu baili serikali pia. Nape anazungumza kishabiki na kitoto zaidi. suala hili si la kishabiki hata kidogo.
 

Buldoza

JF-Expert Member
May 2, 2013
2,304
1,225
Rais hafanyi kazi kwa mashinikizo bana kila anachofanya hufuata sheria siyo kuonea watu.
Alipotezee tu hili swala la Escrow, kwanza halitaweza kuiangusha serikali ya ccm pia hata Kagame alishamwambia kwamba anaongoza wafu.
 

MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
3,698
2,000
Nakubaliana na msimamo wa Nape. Rais ni mkuu na ukuu wake haushinikizwi kwa maslahi ya kisiasa
Hope unasikiliza habari za nchi zingine. Nina maana ya nchi. Waziri wa usalama wa Raia na mkuu wa Polisi Kenya wamejiuzuru kwa sababu ya Al Shaabab kuua wasafiri na ktk machimbo ya kokoto, nje kabisa na Nairobi. Huko Mandera. Kwa nini wakenya wawe na akili sisi iwe ni zero? Ni elimu duni au ufahamu duni kama huu wa kwenu?

Munamuona Rais kama muumba vile! kwamba bila yeye hakuna uhai!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom