Nape: Puuzeni vitisho vya chadema.

HAMY-D

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
7,149
3,817
* Adai kesho ulinzi upo wa kutosha.
* Awapongeza Arusha kuitosa CHADEMA.
* Asema CCM kuzoa kata zote.
* Awasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura kesho.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM amewataka wananchi kupuuza vitimbi na vitisho vya CHADEMA na badala yake wajitokeze kwa wingi kupiga kura kwa amani na utulivu.

Nape amesema kwa ujumla kampeni zimekwenda vizuri, ukiacha matukio machache ya vurugu yaliyo kuwa yakiratibiwa na CHADEMA na wafuasi wao baada ya kuvuta bangi na kunywesha vijana wao viroba.

"Nimekuwa Arusha kwa siku mbili tatu, hakuna mashaka kuwa Arusha wamechoshwa na vurugu za CHADEMA, baada ya kuangaishwa kwa miaka mitatu na CHADEMA wameamua sasa kurudisha heshima ya jiji la Arusha, hivyo nawapongeza sana"

Alipo ulizwa juu ya vitisho vya CHADEMA alisema, "ni kweli hata mie nimesikia wenzetu baada ya kuona maji ya shingo wameamua kutumia vitisho ili kuwatisha watu hasa wakina mama na wazee wasiende kupiga kura, ila nawahakikishia kuwa CCM imejipanga kuwalinda waende kupiga kura kwa amani na utulivu.
 
Moto unawatafuna mtaondoka tu ccm hakuna namna ya kupona ushauri wangu kina Nape chungeni kauli zenu ili mpokelewe na umma hapo baadaye
 
unadhani angesemaje hata kama anajua fika kuwa maji yako shingoni?
 
mkuu ni kweli ilikuwa afanye mkutano muda sawa na wa chadema ila ikashindikana baada ya kuzomewa ikabidi atoke nje ya mji kuanza msafari upya baada ya kamanda wa anga kuondoa majeshi mbulu?
 
vipi hakufafanua ile kauli yak kuwa cdm ni ya watu wakaskazi? au kama kawa wananchi hawakuhoji hilo?
/
 
Du kwel kuna watu wamezaliwa kinafk nafk tu hata km ukwel anaujua still atapanda jukwaan na kuongea yale ambayo hata anayesema hayaamin!!!Waarusha kila la heri hyo kesho.Msiwape hata kata 1 hao nyinyiem
 
nimetokea kuichukia ccm ghafla na kuanzia leo najivua uanachama wa ccm na siyo mfuasi tena nimekereka na yanayoendelea arusha,japo siwezi sema nani anahusika au hata kumjua ila ccm tena kwangu noooo.
 
Back
Top Bottom