Nape: Posho sio Agenda ya CCM, Njoo utueleze Vizuri... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape: Posho sio Agenda ya CCM, Njoo utueleze Vizuri...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bigirita, Jan 31, 2012.

 1. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka Bw, Nape alikwenda kwenye Kituo cha redio cha Clouds wiki chache zilizopita, na akasema posho ya wabunge inayoongezeka sio agenda ya CCM wala hakubaliani nayo. Natumaini alikuwa anaongea kama:

  1) Kiongozi wa CCM
  2) MwanaCCM ambaye ni kiongozi

  Alisema pia kwamba hakubaliani na Mh. Ndugai kwamba posho ya kiasi cha Tsh 330,000 kwa sikuni halali yao.
  Alisema, " Mh. Ndugai, kwa hilo, nasema hapana''.

  Sasa nauliza hivi, aliyeongea habari ya posho kwa uhakika ni Mh. Anne Makinda (speaker), ambaye ni mwana CCM na kingozi ndani ya chama chake. baada ya kelele zote, mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete, amesaini matumizi ya kiwango kipya cha posho ya kukaa kikaoni ya Tsh 200,000 kwa siku.

  Nape, hebu tuambie, kama upandishaji wa Posho haukua agenda ya CCM, ilikuwa ya nani? mbona mwenyekiti wako amekubali?
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Sisi walipa kodib tumesema POSHO kwa wabunge kwa kazi walioiomba wenyewe hapana; kwa nini rais Kikwete atulazimishe?
   
 3. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mkuu, swali lako atalijibu kwamba wawakilishi wenu ndio walioleta hoja, wamelalamika posho haiwatoshi.

  kumbuka wawakilishi wetu ni hawa vibuyu wa CCM tuliowachagua wenyewe, wakipiga kura wanashinda wao.

  tunakuwa tumeliwa once again.
   
Loading...