Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Baadhi ya nukuu za Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akizungumza kwenye kipindi cha Joto Kali la Asubuhi TVE na EFM Radio leo Oktoba 17, 2022.

BE4290E3-E204-44E7-B812-25C9390AAE32.jpeg


Kuhusu kutishiwa Bastola
Anaamini kuwa lilitokea kwa kusudi maalumu, na lilileta mafunzo makubwa kwake, waliopanga, waliowatuma na kwa kila mtu. Ameamua kufunika kombe, na hana muda wa kulipa kisasi. Amesamehe

Mikutano ya kisiasa
Anaamini katika ushindani kwa hoja kupitia mikutano ya kisiasa, hata hivyo anaheshimu maamuzi ya Rais ya kuunda kikosi kazi kitakacholeta utaratibu na mapendekezo ya jinsi ya kuendesha mikutano hiyo.

Maamuzi haya ni mazuri kwa kuwa Rais Samia amekuwa tofauti kidogo na mtangulizi wake aliyezuia kabisa kufanyika kwa mikutano hiyo.

Nguvu ya Makatibu Wakuu wa Chadema, Dr. Slaa na Mnyika
Anaamini Dr. Slaa alikuwa habari nyingine, ilikuwa ni ngumu zaidi kupambana naye kwa hoja kwa sababu maneno yake yalikuwa ni kama kanuni kwa jamii.

Hata hivyo, Kwa sasa CCM inao watu imara sana kama Mzee Kinana ambao wanaweza kushughulikia aina hii ya hoja.

Anwani za makazi
Amesema zoezi limefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 98 kwanza kwa kuwa awali hapakuwa na bajeti ya kutosha ambapo limehitaji bilioni 28.

Kazi iliyopo saivi ni kuboresha, mfano baadhi ya sehemu kuna majina mawili yanayofanana, mengine yamekosewa.

Bei za bando za internet
Amesema bei za bando hazibadiliki mara kwa mara, makampuni hutageti soko kwa kubadilika kwa kuongeza au kupunguza, watu hawaangalii kupungua, wanalalamika tu kuongezeka.

Kila baada ya miaka 4 kuna tathimini inafanyika, mfano uwekezaji, gharama za uendeshaji. Hakuna kampuni ya simu inapandisha tu gharama pasipo kupata kibali cha TCRA. Serikali imewabana sana.

Kwa ukanda wetu, Tanzania ipo chini sana kuliko wengine. Hata hivyo, purchasing power ya watu bado ni ndogo, ndiyo maana gharama bado inaonekana kubwa. Mwezi huu wa 10 watafanya tena tathimini.

Kuhusu Youtube
Amesema Mtandao ni dunia pana, kama nchi ni nzuri kuwa na regulations. Lazima kuwe na usajili, mfano mtu aliandika Mwakyembe kafariki.

Hii itasaidia kuzifahamu. Kuhusu kufanya iwe bure kabisa hadhani kama itawezekana, maana gharama pia zimepungua kwa zaidi ya asilimia 50.

Matumizi salama ya Mitandao
Amesema baada ya kuona matumizi ya watu mtandaoni yaneongezeka pamoja na matukio ya kihalifu, wameona waweke nguvu kubwa katika kutoa ufahamu kwa watu juu ya matumizi salama ya mitandao.

Pia kuna mmomonyoko mkubwa wa maadili, watu watunze faragha zao. Ndiyo maana kuna sheria nyingi zinakuja ili kulinda watu.

Amebainisha pia kuna changamoto ya wingi wa line za simu, zipo milioni 58 ambazo zimesajiliwa, ndiyo maana wanakuja na sheria ya data protection. Katika mazingira hayo line za kitapeli lazima ziwepo, haiwezekani nchi ya watu milioni 60 iwe na line milioni 58.

Kukusanya taarifa za watu
Amesema wameandaa sheria itakayoweka utaratibu wa nani akusanye taarifa binafsi za watu mfano Jina, DNA na zitaenda kutumikaje.

Leo unaweza kununua vitumbua mtaani na ukakuta ile karatasi ina majina yako. Kuna taarifa za watu zinaenda nje ya mipaka ya nchi, taarifa lazima zilindwe. Ni hatari sana.

Mfano ni matangazo ya biashara, unatumiwa matangazo mengi ambayo hata hujui hata yametoka wapi ndiyo maana wanataka kulinda privacy.

Kukamata wapinzani, Katuni za ushoga na mengine
Kada huyu aliandika mtandaoni kuwa bei ya umeme imepanda, Yeye kama waziri hana mamlaka ya Kumkamata, lakini alitoa maoni yake kuwa jambo hilo halikuwa sawa na vyombo husika vikachukua hatua.

Hata issue ya ushoga kupitia katuni zinazoweza kuharibu watoto aliikemea hadharani kwa kuwa siyo kitu kizuri. Alienda mbali kwa kuwaambia hao wanaozitetea wasije kulia baadae wakiona watoto wao wa kiume wanawaletea wachumba nyumbani.

Serikali inajenga mkongo wa taifa wa Mawasiliano kutoka ziwa Tanganyika kwenda Congo ili wapate access ya internet. Pia serikali itakwenda Congo na wadau wa TEHAMA kwenda kusaka fursa.
 
Ilileta funzo kwake yeye aliyetaka kushindana na tawala na ndio maana mwisho wa mchezo alienda kupiga magoti kwa kutembea kilomita kadhaa.

Uzuri waliweka rekodi nzuri na tunayo hadi kesho.
"Yupo miongoni mwenu asiye na hekima naye aombe Mungu atampatia"...Tanzania njema is a must project, apende au asipende mtu..
 
Bado tu anaendelea kumnanga Magufuli.

Huo uwaziri wake sio kwa ajili ya kumsema Magufuli.

Afanye kazi za Wananchi.

Asifikiri kila mtu anafurahia anachokifanya.

Hatupendezwi na hiyo tabia yake mbaya.
 
Huo upuuzi wa kusema sisi kwa Afrika mashariki tuna gharama za chini za bando ndio huwa sipendi kuusikia, kama watu bado wana lalamika inamaanisha bado wame banwa

sasa hivi vijana wengi walio kosa ajira wameamua kujiajiri kupitia mitandao kama YouTube na Instagram, na huko tena mnawafinya alafu mnakuja kuwa nanga baadae eti "vijana msisubirie ajira za serikali mjiajili"
 
Nadhani hizi bando zimepandishwa na tozo. Watuoneshe charges zipo vipi. Miezi 2 iliyopita laki moja ilikuwa inanitosha kwa mwezi lakini sasa hivi, duh
 
Hawa jamaa huko CCM wanaonesha dhahiri vile huwa hawakubaliani na baadhi ya maamuzi ya serikali yao, tatizo lao ni uoga.

Hapo kuhusu mikutano ya kisiasa, kama kweli anaamini kwenye ushindani wa hoja alitakiwa kusimamia hapo hapo, ili akawaeleweshe wenzake wa CCM wenye vichwa vigumu nao wajue, akawe mwalimu wao.

Lakini badala yake, anarudisha maamuzi kwa wale anaoamini hawako sahihi, kusubiri majibu ya kikosi kazi kwenye jambo unaloamini tofauti, ni sawa na kusema akili yako haina kazi tena, yupo mwingine anayefikiria kwa niaba yako, na chanzo cha haya yote ni hofu ya kupoteza mkate.
 
Binafsi nachukia sana mtu anayejinasibisha kuwa ni kiongozi wakati kiuhalisia hana hata sifa moja ya kuwa kiongozi.

Unapokuwa na tabia za undumi la kuwili, ukikaa gizani unaongea mengine ukiwa katika media unaongea vingine, huku raia tunaona vingine tofauti kabisa. Upumbavu sana huu.
 
Ilileta funzo kwake yeye aliyetaka kushindana na tawala na ndio maana mwisho...
Lililopigiwa magoti kwa kujifanya limungu lishakufa, madogo wapo wanadunda na afya tele.

Mijitu yenye roho mbaya huwa haina uhai mrefu, jitu linajifanya ye mungu mtu
 
Nape Nnauye umeshindwa kudhibiti mitandao ya simu inajipandishia tu gharama za vifurushi. Hebu fikiria ndani ya mwaka huu mitandao ya simu imebadilisha vifurushi na kupandisha gharama za vifurushi zaidi ya mara tatu mfululizo.

Mwaka jana tu, tumenunua vifurushi GB 1 kwa TZS 1000 na 1500, lakini tangu tuanze mwaka huu mpaka sasa hivi vifurushi TZS 3000.

Hivi kweli umeshindwa kudhibiti mitandao ya simu isiwe inapandisha gharama kiholela pasipo utaratibu maalumu?

Watu wengi siku hizi wanafanya biashara kwa kutumia mtandao wa intaneti, sasa mnapopandisha gharama kiholela hamuoni kama mnazidi kuongeza ukali wa maisha kwa Wananchi?
 
Nje ya mada..vile vi nukta kwenye uzi wa Yoga vina maana gani??

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom