Nape Nnauye, ni kivuli cha baba yake u mwendelezo wa usaliti? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape Nnauye, ni kivuli cha baba yake u mwendelezo wa usaliti?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DUNIANGUMU JR, Apr 22, 2011.

 1. D

  DUNIANGUMU JR Member

  #1
  Apr 22, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NAPE NNAUYE, NI KIVULI CHA BABA YAKE AU MWENDELEZO WA USALITI???

  ninapo sikia jina la Nape Nnauye linanikumbusha enzi ile ya baba yake mwandani wa baba wa taifa mwalimu julius nyerere!! baba yake alikuwa hodari wa kuhamasisha vijana wa Tanu na ccm, chipukizi, nyimbo zake nyingi ni za kizalendo kiasi kwamba ukiziimba unajione kweli uko tanzania na mtanzania halisi!!! lakini sasa baada ya kufariki baba wa taifa na mzee huyu, mvuto wa ccm kwa wananchi umepunguwa kwa vile viongozi ambao nyerere aliwakampenia na kuhakikisha kuwa wataendeleza pale alipoachia wakamsaliti na kumpumzisha butiama ili waweze kuuza mashirika ya umma na nyumba za serikali.
  Sina hakika huyu Nape nnauye atakuwa kama baba yake au naye atafuata usaliti huo huo, lakini mie namuonya akienda kinyume na alivyokuwa baba yake hatafika mbali!!!! Hata hivyo ninaimani naye kwani ni Mtu katika umoja wa vijana aliyethubutu kumtaja Lowasa kama ni fisadi amukula fedha za jengo la umoja a vijana, na ndiyo maana akafuzwa kwa hila, sasa ni zamu yako kuonesha kuwa una damu ya nyerere.
   
 2. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Like father like son
   
 3. m

  mbungula Member

  #3
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nape na mwezie chiligati wamepata ajali
  wakiwa jukwaani wakiwa iringa naona
  mapacha watatu wanataka kuwaonyesha
  kuwa hawako peke yao
  chanzo cha habari ni redio cloud fm
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wakati mwingine mnyama simba aweza kuza Simba-Mbweha.

  Hii hali japo mara nyingi huonekana kuwa ni wa ajabu saaaaaaaaaaana tu lakini kila kitu hapa hutegemeana tu na ukweli kwamba wakati wa kuongeza kizazi ulimwenguni ni mnyama yupi na yupi hasa ambao ndio waliokutana katika zoezi zina.

  Katika hili nashauri ni vema watu tukamuachie MUDA msema kweli kuja kutupa majibu sahihi juu ya hilo.
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Labda walikua wanatunga kauongo fulani usiompendeza Mungu ndipo wakapata kutetemeshwa kidogo ili wapate kuamka kutoka kwenye njozi za maangamizi vile.

   
 6. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mod umechakachua kuunganisha hizi thread mbili hazifanani. Umezuia watu kufuatilia na kujadili anachosema sasa hivi.
   
 7. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #7
  Apr 22, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kijana yupo poa bt chama alichopo ndio mzinguo!
   
 8. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #8
  Apr 22, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 9. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #9
  Apr 22, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kwani babake alikuwaje?alikuwa mzalendo eeeh ndo maana alikatwa kichwa na taleban afghanistan kujifanye kwenda kusaidia vita....unalea mambo yako ya kufundisha mgambo wakamata ubwabwa wa mama ntilie unapeleka kwa taleban!!!! hahaaaaa....
   
 10. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #10
  Apr 22, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Moses Mnauye baba yake Nape alikuwa kada safi wa ccm na hakuwa mnafiki kama walivyokuwa wenzie; ndio maana alipoona Mkapa anaanza kumsaliti mwalimu akiwa Rais ,ikabidi ajiuzulu kama mshauri wake wa mambo ya siasa. Alikuwa mtu makini sana kisiasa. In fact ni huyo baba yake Nape ndiye aliyemjenga Yusuf Makamba akiwa kama RC pale Singida; wakati huo Makamba alikuwa katibu kata na Mungu wake akamsaidia mpaka hapo alipofikia! Sasa kama Nape atakujakuwa kama baba yake time will tell.
   
 11. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #11
  Apr 22, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Ila aache kutetea familia ya JK, hii ni dalili ya kujipendekeza na mtu yoyote anayejipendekeza huwa kuna kitu anatafuta. Jasiri anasimama kwenye ukweli na ukweli ni kwamba Ridhiwani Jk ana hela nyingi kuweza kupatikana kihalali kwa kijana wa kitanzania. Nape kama ni jasiri alisemee hilo.
   
 12. Mkenazi

  Mkenazi Senior Member

  #12
  Apr 22, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Baba yake Nape alikuwa na cheo kikubwa jeshini - Brigedia general. kama unavyojua watu wa vyeo hivyo maisha ni mazuri sana. Upande wa ng'ombe mzima bure, vinywaji bure kwa ujumla wake ni kama kuishi zero cost. Kwa hiyo kuimba na kuhamasisha watanzania si hoja kwamba aliipenda Tanzania bali ilikuwa ni katika kufurahia shibe yake. Hivyo hivyo huyu Nape amaekulia mazingira yale yale ya Zero cost. Namwona kama mtu anayejitetea, Hajui hata PAYE kwenye mambo ya kodi. CCM ni shamba ambalo mazao yake tumeyaona- UFISADI kila eneo la maisha ya Mtanzania.
   
 13. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #13
  Apr 22, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,556
  Likes Received: 486
  Trophy Points: 180
  Kitendo cha kuwa msemaji wa CCM peke yake kinatosha kumwona Nape ni mtu wa aina gani.CCM hii anayoitetea na kuisemea Nape ni tofauti na CCM aliyokuwepo mzee wake.Kwaiyo ingawa wote ni makada safi wa CCM utofauti ni kuwa Kada wa sasa wa CCM ana malengo tofauti na kada wa zamani wa CCM.
   
 14. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #14
  Apr 22, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  kweli,CONGOLESE style! ulishwe na kunyweshwa kutoa zako tabu.!
   
 15. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #15
  Apr 22, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,556
  Likes Received: 486
  Trophy Points: 180
  Kitendo cha kuwa msemaji wa CCM peke yake kinatosha kumwona Nape ni mtu wa aina gani.CCM hii anayoitetea na kuisemea Nape ni tofauti na CCM aliyokuwepo mzee wake.Kwaiyo ingawa wote ni makada safi wa CCM utofauti ni kuwa Kada wa sasa wa CCM ana malengo tofauti na kada wa zamani wa CCM.
   
Loading...