Nape Nnauye ni chaguo la pili la Mungu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape Nnauye ni chaguo la pili la Mungu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by msolopa ganzi, Oct 19, 2011.

 1. m

  msolopa ganzi Member

  #1
  Oct 19, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 57
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  SALAAM Aleikum wapendwa wasomaji wa kalamu hii. Kwa wiki kadhaa hatujakutana hapa kwenye ukurasa huu kwa sababu za Igunga na yale yaliyofuatia baada yake. Naomba turejee katika kuendelea kuangalia mustakabali wa taifa hili kongwe linaloitwa changa na wanyonyaji wetu. Wasomaji, huko nyuma niliwahi kuandika nikikubaliana na Baba Askofu aliyemuita Kikwete ‘Chaguo la Mungu'.

  Niliweka bayana kwamba tunaweza kutofautiana na baba askofu sababu hasa ya kuamini kwamba JK ni chaguo la Mungu lakini tunakubaliana naye katika hitimisho kwamba kweli ni chaguo la Mungu. Nilieleza pia kwa nini naamini sasa kwamba JK ni chaguo la Mungu. Ni kwa sababu Mungu aliamua kumtumia kuiua CCM na hatimaye kuiondosha madarakani. Nilisema kwamba watanzania walishafungwa wakawa mateka wa watawala wetu kupitia chama dola cha CCM.

  Wakoloni weusi hawa wakawa wanawatenda wananchi watakavyo. Wakawanyima elimu, wakawanyima afya na mali pia. Wakawa mbumbumbu hata wa haki zao za asili na elimu ya kawaida tu ya uraia.

  Serikali haiwajibiki kwa wananchi kama inavyotakiwa na pale inapojisikia kufanya sehemu ndogo sana ya wajibu wake, wananchi wanapiga magoti kuishukuru utadhani walichokifanya ni hisani si wajibu. Ujinga huo wa kutofahamu hata mambo ya msingi yanayohusu maisha yao, jumlisha umaskini wa kutupa waliosababishiwa na chama hicho hicho na serikali yake, wakawa ni watu wa kupelekwa kama kondoo.

  Ni katika hali hiyo kwamba hata pale mfumo wa vyama vingi uliporejeshwa, CCM ikatumia umbumbumbu wa Watanzania kuwadanganya kwamba wasiamini chama chochote kipya. Wakaendelea kuamini kwamba kiongozi mzuri wa nchi hii lazima atoke CCM. Kazi iliyokuwepo sasa ilikuwa ni kutafuta kiongozi yupi ambaye anaweza kuleta mabadiliko lakini ndani ya CCM. Chama na serikali yake vikazidi kulielekeza taifa kusikoeleweka na wananchi wasijue la kufanya.

  Ndipo wakafikia mahali pa kukata tamaa. Wakaona nini kitafanyika kuboresha hali yao kama taifa. Mbona taifa linaangamia? Walikuwa wakiangalia utawala wa miaka kumi wa Mzee Ruksa na jinsi ulivyoliathiri taifa kwa kufutilia mbali Azimio la Arusha na kuwaingiza viongozi katika harakati za kujilimbikizia mali na hivyo kujihusisha na rushwa kubwa (grand corruption). Utawala huo ukafuatiwa na ule wa Mzee wa Ukapa ambaye aliuza kila kilicho cha umma na kugawa raslimali za taifa hili kama vile anagawa njugu kwa watoto.

  Katikati ya kukata tamaa bado wananchi hawakuwahi kufikiria nje ya CCM. Bado walidhani hakuna kiongozi nje ya CCM. Kelele za kuwaelekeza watanzania kuangalia nje ya CCM zilikuwa zinazidi kusikika lakini Watanzania walikuwa bado hawajaelewa sawa sawa. Na ndipo ghafla ukatokea mwangwi wa kile kilichoitwa JK.

  Mwangwi huo ukasikika kila kona ya nchi na watanzania wakasadikishwa kwamba ndiye pekee aliyekuwa amebaki ndani ya CCM kuleta mabadiliko tunayoyataka. Mungu anamfahamu Kikwete kabla hajazaliwa, anajua hata atakavyozeeka na hatimaye kufariki dunia kama anavyomjua kila mmoja wetu. Alijua kwamba watanzania tulikuwa tunapotea njia. Alijua kwamba Kikwete ataliharibu taifa kuliko wote waliomtangulia. Lakini hakuwa na jinsi. Alitambua kwamba hiyo ndiyo njia pekee ya kuwakomboa Watanzania.

  Aliwaacha wazidi kuzama na kudhani kwamba "Tumaini limerejea". Aliruhusu uwongo wa shetani kupitia kwa mafisadi utawale kwamba JK ndilo kimbilio pekee litakalobadilisha kabisa mustakabali wa nchi hii. Mwenyezi Mungu anajua yaliyopita, yaliyopo na yajayo. Aliona kabisa jinsi ambavyo watanzania watakatishwa tamaa na JK. Aliona jinsi ambavyo taifa litapitia wakati mgumu wakati wa kipindi cha uongozi cha mheshimiwa huyu. Aliona hali ya kiuchumi ikiwa ngumu kupita kiasi na kila Mtanzania akilia kwa kukosa umeme, baa la njaa na kupanda hovyo kwa gharama za maisha ikiwamo na bei za vyakula na bidhaa nyingine za muhimu katika maisha.

  Alitambua kwamba hicho kitakuwa kipindi kigumu sana kwa watanzania ambao pamoja na hali ya maisha kuwa mbaya kiasi hicho bado hakutakuwa na uongozi wa kuelekeza cha kufanyika. Mungu alijua kutakuwa na ombwe la uongozi litakalopelekea mafisadi kutamba watakavyo huku kila kundi la jamii likijifanyia litakalo hata kuitisha serikali. Alijua kwamba kuna wakati wafanyabiashara ya mafuta wataamua kufungia mafuta yao kwenye matenki na kukataa kuuza na hatimaye uchumi wa taifa kusimama kwa siku kadhaa.

  Aliyaona yatakayotokea baada ya uongozi wa taifa kuchukuliwa na mtu dhaifu akiwa ndiye mkuu wan chi na kiongozi wa chama tawala na kuruhusu kila mtu kujifanyia na kujisemea kivyake utadhani hakuna rais. Aliyaona madudu ya Richmond na Dowans na jinsi yatakavyolitesa taifa na hatimaye baada ya kulifyonza kwa miaka kadhaa taifa linadaiwa mabilioni ya shilingi na kuifilisi hazina.

  Alijua wakati wa uongozi wa awamu ya nne ya taifa hili utakuwa wa taabu na uchungu mwingi. Lakini alichokiona yeye ni yale yatakayojili mwishoni mwa awamu hiyo. Mwisho wa Awamu ya Nne Mwenyezi Mungu aliona jinsi watanzania watakavyokuwa wamekata tamaa na CCM. Aliwaona vikundi vikundi wakijiuliza, "Kama JK katufanya hivi, nani tena anayeweza kuaminika ndani ya CCM kwamba ataweza kufanya mabadiliko?" Kukata tamaa huko kukachagizwa na mwenendo wa vyama vya upinzani nchini.

  Vyama vikaanza kujichuja, vilivyo makini na mustakabali wa taifa hili vikaonekana. Vikafanya kazi kubwa ya kuelimisha jamii ya Watanzania nao wakaanza kuelewa kwamba "mabadiliko wanayoyahitaji hayawezi kupatikana kwa kupitia kwa mafisadi wale wale wa chama kile kile wakiendeleza madudu yale yale eti kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya".

  Yote hayo aliona Muumba kabla ya JK kutawazwa kuwa rais wa nchi hii. Na kwa sababu hiyo akamchagua rasmi JK kuwa rais atakayemfuatia Mkapa ili baada yake, watanzania wafanye mabadiliko waliyoyataka. Ndiyo sababu ya kuitwa ni chaguo la pili. Kazi aliyopangiwa JK kaimaliza salama. CCM yake haijapata kuwapo tokea kuumbwa kwa taifa hili.

  CCM ya JK imeparaganyika haijapata kutokea lakini mwenyewe anachekelea na kutabasamu kana kwamba hakuna kilichotokea. Wanachama wanaumana na kuchanana kila kukicha lakini mwenyekiti ndiyo kwanza anashangilia uimara wa chama. Hivi sasa kuna CCM zipatazo tatu kwa haraka haraka na kwa kuzingatia ukubwa wa CCM zenyewe.

  Lakini mwenyekiti ndo kwanza anafanya kazi ya kuhakikisha anakubalika kwa CCM zote zikiwamo zile ndogo ndogo ambazo hazijajionyesha sana, badala ya kuziunganisha ziwe moja. Leo CCM imefikia mahali jimbo ambalo wameliongoza kwa makumi ya miaka tena mara nyingine wakipita bila kupingwa kama ilivyokuwa Igunga, lakini uchaguzi mdogo wanalazimika kutumia mbinu za uani ili watangazwe washindi!! Lililo dhahiri ni kwamba CCM ya JK imedhoofika kupita kiasi, dhambi zake zimeilemea sana na mzigo wa madhaifu wake umekuwa mzito kupita kiasi.

  CCM inayumba yumba, inawaya waya na karibu itaanguka na haitainuka tena, kama Nabii Isaya 24 kuanzia fungu la 3 inavyoizungumzia sayari hii ya dunia. Wakati kazi ya JK ikifikia ukingoni na yeye akiwa sasa anaaga baada ya kukamilisha kazi Mungu akachagua chaguo la pili la kuhitimisha kile kilichoanzishwa na kufanywa na JK. Huyu si mwingine ni Nape Nnauye, Katibu wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi kuja kuhitimisha hiyo kazi ya kuiangusha CCM. Ni kama Yesu alivyokuwa anamaliza kazi yake hapa duniani akawaambia wanafunzi wake kwamba hamtabaki wapweke.

  "Nitawaletea msaidizi ambaye atawafundisha kuyashika yote niliyowafundisha na tazama nitakuwa nanyi hata ukamilifu wa dahari". Sisemi JK ana sifa kama za Yesu. Ninajaribu kulinganisha kazi aliyoifanya na hatimaye kuirithisha kwa Nape. Hivi sasa Nape anafanya kazi ya kuimalizia kazi hiyo kwa kukimalizia kabisa chama hicho.

  Ameibuka akikomalia magamba na ndio umekuwa wimbo wake. Ndiye aliyesababisha Rostam Aziz kujiuzulu. <BR>Mwisho wa siku walihenyeka na kufanya mbinu za ziada ili kutangazwa washindi. Wenye akili tukadhani ingawa wametangazwa washindi lakini biashara ya kuvuana magamba ingekuwa imefikia mwisho. Hatukutarajia baada ya mshike mshike wote huo uliotokana na kuvuana magamba, kuna kiongozi tena ndani ya CCM wa ngazi za juu angeweza kusimama na kudai wanaendelea kuvuana magamba.

  Ajabu tukashtukia Nape anaibuka mafichoni na kudai kwamba kuvuana magamba kumelipa. Watu ambao walikuwa hawajajua mambo ya Igunga wakaanza kufuatilia matokeo. Wakakuta kwamba wakati mwaka jana CCM ilipata 72%, mwaka huu imepata 50%. Wakashikwa na mshangao.

  Kimsingi ili Nape aseme kwamba kuvua magamba kumelipa ilikuwa iwe hivi: Kwamba mwaka jana CCM ilipata 50% halafu baada ya kuvuana magamba wamepandisha asilimia hadi 72. Hapo alikuwa na haki ya kutambia kuvuana magamba. Lakini kwa hali ilivyo, Nape kuendelea kupambana kwamba magamba yaendelee kuvuliwa ni sawa na kufanya kazi ya kukimalizia chama chake. Kazi ambayo anaifanya kwa uaminifu mkubwa.

  Nape Nnauye ni chaguo la pili la Mungu katika mchakato wa kuhitimisha utawala wa CCM katika nchi hii na kuleta matumaini mapya kwa watanzania waliokata tamaa. Na huu ndio mrejesho wa unabii ama utabiri wa M.M. Mwanakijiji aliyewahi kusema, "Kuanguka kwa CCM unabii utatimia" Ukisoma kwa pamoja na utabiri wa Kalamu ya Mwigamba uliosema, "Unabii wa kuanguka kwa CCM utatimia hivi".

  Ni suala la muda tu kazi ya Nape iliyoanzishwa na JK itakapokamilika, matokeo tutayaona.

  Tusubiri tuone!
   
 2. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Tafakuri yako safi ila labda kichwa cha habari kinahitaji alama (?) mwishoni.
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mimi nasema bila alama ya ? Yes ni chaguo la shetani CCM maana naye ni mungu kivyao wanavyo ishi.
   
 4. G

  Giddy Mangi JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 833
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Labda mungu wa Ccm yule wanayemwabudu chini ya Bahari.
   
 5. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Hicho kichwa cha habari kitasababishwa utukanwe bure... Sijasoma thread yako naiweka pending hadi lunch kwa kuwa ni ndefu, lakini kumuhusisha aliyetukana watu kuwa atawashikisha ukuta na Mungu ni dhambi kubwa.
   
 6. P

  Paul S.S Verified User

  #6
  Oct 19, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Siasa za nchi hii bana,
  Ni bora Nape ajiunge na akina mapacha watatu aanze kula nchi tu na yeye
  Maana akipinga ndani ya CCM anapingwa ndani na nje ya CCM
   
 7. prakatatumba

  prakatatumba JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,337
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Jamaa chaguo la popo bawa,ndyo maana amewaambia watu wa mwanza wanashikishwa ukuta.
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Jamaa hakubaliki maana ni mnafiki ila kibaya nje nako anatukana watu kisa hawatoi support kwa CCM ndiyo anapo vamiwa sasa kaka .Vinginevyo akikaa ndani ya mipaka hakuna wa kuhangaika naye .Ila kushikisha watu ukuta duh jambo kubwa hili mimi nina mke wangu anishikishe ukuta kisa nime enda kusikiliza upupu wake kwenyeh mkutano wa ma CCM .Aaaaaaaaaaaaah haijubaliki kaka .
   
 9. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Umesomeka mkuu.
  Mungu aaaaaaaliyemchagua jk ndiye huyo aliyempa nape kuwa msaidizi wake.
  Suala la ni mungu yupi sisi hatujui ila kazi yake inaonekana.
   
 10. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #10
  Oct 19, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,322
  Likes Received: 22,149
  Trophy Points: 280
  hata shetani ni mungu kwa wamuabuduo
   
 11. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  umenena hakika!
   
 12. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Makala ni ndefu lakini si riziki mana imejaa hisia badala ya uchambuzi wa uhalisi.ungesema kuwa ni maoni yako pengine tungekuelewa..
   
 13. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #13
  Oct 19, 2011
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kabla sijaisoma thread nilikuwa nakutafutia jibu la maudhi lakini baada ya kuisoma na kuielewa nimekubali ni chaguo la mungu, ila yule wa ccm.
   
 14. m

  mharakati JF-Expert Member

  #14
  Oct 19, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  POST nzuri ila mwandishi amesahau kuwa dola iko upande gani na baada ya kuharibu sana kwa Jk unafikiri hakuna mwingine wa CCM atayesema sasa mimi ndiyo mkombozi wenu wa kweli nimekuja kurekebisha mabaya yote? wananchi na ujinga wetu tutasema labda watajirekebisha safari hii baada ya kugombana wao kwa wao, labda labda watakuja wale wale kwani mfumo wa dhuluma umeota mizizi na hautabadilika kwa ndani, ila wapiga kura ndiyo watakaoamua kwani wakiwapa wapinzani 60% CCM itakua vigumu kuiba..tatizo hawa wananchi wako tayari?
   
Loading...