Nape Nnauye: Nahisi Mashabiki wa Kiba ndio waliokuwa wakipinga Diamond kupewa Bendera ya Tanzania

Ni suala la kutoa elimu tu kuwa kumpa bendera Diamond kulikuwa ni jambo jema kabisa kwa sanaa ya muziki wa Tanzania. Anapoingizia ishu ya ushindan wa Diamond na Kiba anaanza kuvua viatu wa uwaziri na kuvaa vya ushabiki.

Kwa kauli yake nimegundua yuko timu Mond na anaonyesha upendeleo wa wazi. Jiulizeni ni lini aliwahi kwenda kwa Kiba kujionea kazi zake za muziki?

Tatizo ni kumpa kazi ya uwaziri mtu aliyekuwa Katibu mwenezi wa chama. Kazi ya katibu mwenezi ni kuona rangi mbili tu-rangi ya watawala na ya wapinzani. Kama huna rangi ya chama tawala basi wewe ni wa upinzani. Kama unaponda Diamond kupewa bendera basi wewe timu Kiba. Hajui wengine wanakosoa kwa sababu hawajazoea tu, ndo tunafanya mara ya kwanza. Hawa wanahitaji kuelimishwa kwamba Diamond ana nafasi nzuri zaid ya kuutambulisha muziki wa Tanzania kwa Africa nzima maana Misri, Algeria, Tunisia na wengineo watakuwa wanafuatilia na njia rahisi kutambulisha nchi kwenye tamasha ni bendera.
Kiba hana office unataka amutembelee pale michikichini
 
Mimi ni shabiki wa Diamond, ila hii sio kauli inayopaswa kutolewa na Waziri
 
Kiba hana office unataka amutembelee pale michikichini
Haahaahah! Acha hizo ndugu yangu, hata ndege ana kiota. Afuatwe popote alipo. Lakini hoja muhimu ni kwamba Diamond sio mtanzania pekee mwenye mafanikio makubwa ya muziki.

Awe anaenda hata kwa Asha Baraka pale, aende DDC Mlimani Park, kisha kwa baba la muziki na mwisho awambie UVCCM wafufue bendi ya wana Air Pambamoto aka Vijana jazz. Asimwagilie mti ambao matunda yameshaiva tayari-hiyo ni janja ya kula matunda kinyemela.
 
Wala HAJAKOSEA ukweli ni lazima usemwe hata kama ni mchungu, TIMU KIBA NDIO WANAOMSHAMBULIA YEYE KWANINI AMPE MOND BENDERA,sasa aogope kuwataja kwani wao ni kina nani ktk nchi hii ........ wanatajwa waislam/wakristo kwenye ishu wanazohusika iwe hao wakina timu kiba ......???
Inaonekana unapenda sana timu. Wewe upo timu gani?:D
 
Kulikuwa na sababu gani waziri kulisemea jambo dogo kama hilo??

Mambo mengine ni yakupuuza tu ili kutochochea utengano usio na sababu za msingi!

Ni vigumu sana kuamini kama hawa watu walipata kufanya kazi na mzee wa msoga!
 
Kwani kwa mfano hapo utahoji kipi kimfanye yeye kuukana uwaziri wake ......... Kwamba ni kosa KUSEMA KUWA TIMU KIBA NDIO WALIOPINGA DIAMOND KUKABIDHIWA BENDERA YA TAIFA ??
Umesimamia show nzima mpaka vidole vimekuvba nahisi
 
Waziri wa sanaa na michezo Nape Nnauye amesema anahisi mashabiki wa upande wa Ali Kiba ndio walikuwa wakiponda kuhusu Diamond kupewa bendera kwa sababu kumekuwa na uhasama na chuki kati ya pande hizo mbili, yeye binafsi amedai hana tatizo na msanii yoyote kati ya hao wawili na wamekuwa marafiki zake kabla hata hajawa waziri

Wazir nape Mbona hyo kauli yako km ya kishabiki ukiwa km kiongozi kauli hukupaswa kuitoa sababu inaashiria km ww ni shabik wa upande fulani
 
Huo ndio ukweli hata kama ni mchungu,sasa kama keshagudua kuwa wanaomshambulia yeye kwa kumpa bendera DIAMOND kina timu kiba kwanini asiseme ........ Kwani serikali inakatazwa kusema kwamba wanaoponda kitu fulani ni kikundi fulani ........ Mbona serikali ilisema kuwa waliovunja viti vya uwanja wa taifa ni simba,mbona hakuna aliyesema serikali kwa sasa na wenyewe ni Yanga ........Na hata humu wanaomshambulia waziri kwa kauli yake ni timu kiba tunawajua,kisha mnakataa sio ndio mnaopinga bendera kupewa DIAMOND.Mbona Serikali huwa inasema kuwa waliofanya tukio fulani ni WAISLAMU,mbona hakuna anayesemaga kama serikali imekuwa ya kikristo .........Ila kwenye hili serikali imewakabili moja kwa moja watu fulani ndio wahusika wa hili tukio,imekuwa kosa......??
Hadi ridhwan kikwete team kiba bas
 
Back
Top Bottom