Nape Nnauye kupandishwa kizimbani kwa kuingilia uhuru wa mahakama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape Nnauye kupandishwa kizimbani kwa kuingilia uhuru wa mahakama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by palalisote, Oct 29, 2011.

 1. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  JAJI wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Aloyce Mujulizi, ameamuru Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, afikishwe mahakamani kwa madai kwamba anatoa matamshi yaliyoingilia uhuru wa mahakama.

  Jaji Mujulizi alitoa uamuzi huo jana mara baada ya kusikiliza hoja iliyowasilishwa mahakamani hapo na Wakili Method Kimomogoro anayemtetea Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, ambaye alidai kuwa Nape amesema kwamba ana uhakika CCM itashinda katika kesi hiyo.


  CHANZO: TANZANIA DAIMA

   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nape na mhariri wa Nipashe kupanda Kizimbani Arusha Novemba 16 mwaka huu.


  Mahakamani Arusha - Shauri la kupinga matokeo ya ubunge


  Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imetoa hati ya kuitwa mahakamani hapo,
  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye na Mhariri wa Gazeti la Nipashe
  kwa maelezo kwamba waliingilia mwenendo wa kesi ya Lema. Nape na mhariri huyo wanapaswa kufika mahakamani hapo, Novemba 16 mwaka huu.

  Wito huo unatokana na hoja ya Wakili wa Lema, Method Kimomogoro aliyesema kwamba upande wa utetezi hauna imani na Jaji anayesikiliza shauri hilo, Aloyce Mujulizi kutokana na matamshi yaliyotolewa na Nape na kunukuliwa na Gazeti la Nipashe. Wakili huyo alisema matamshi ya kiongozi huyo wa CCM yanaashiria kuwapo kwa njama za walalamikaji kushinda kesi hiyo isivyo halali.

  Akiahirisha kesi hiyo jana, Jaji Mujulizi alikubaliana na hoja za Kimomogoro za kuitwa mahakamani hapo watu hao wawili na kwamba Nape anatakiwa aieleze mahakama hiyo juu ya matamshi yake yaliyonukuliwa na Nipashe toleo la Oktoba 9, mwaka huu. Alisema mhariri wa gazeti hilo anapaswa kufika mahakamani ili kutoa uthibitisho juu ya matamshi aliyotoa Nape kupitia gazeti lake.

  Mapema Kimomogoro aliieleza mahakama hiyo ya kuwa kitendo cha Nape kutoa matamshi yanayoashiria kuharibu mwenendo wa kesi hiyo ni kosa na kwamba kufanya hivyo ni kuingilia uhuru wa mahakama. Wakili huyo alisema sehemu ya habari hiyo ilisema: "Nnauye alisema kwa sasa wako katika mchakato wa kwenda kupiga kambi katika Mkoa wa Arusha ili waweze kulichukua jimbo hilo. Alisema wana uhakika wa kushinda kesi yao dhidi ya Lema na kulichukua jimbo hilo uchaguzi utakapofanyika." Kimomgoro alisema matamshi hayo hayajawahi kukanushwa hadharani na kusisitiza ya kuwa mteja wake ambaye ni Lema, Chadema pamoja na wafuasi wa chama hicho wana shaka na kauli hiyo.

  Hata hivyo, maelezo hayo yalipingwa na wakili wa walalamikaji, Alute Mughai ambaye alisema hizo zilikuwa mbinu za kuchelewesha kesi. Kuhusu hoja ya kauli iliyotolewa na Nape, Wakili Mughai alisema mahakama hiyo haiwezi kusikiliza mambo yote yanayoandikwa kwenye magazeti hapa nchini huku akitoa onyo ya kuwa endapo mahakama hiyo itakuwa ikisikiliza mambo ya magazetini, basi huenda ikakwamisha shughuli zake.


  CHANZO:
  Gazeti la Mwananchi
   
 3. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,142
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  atapatika wapi wakati yuko kozi US? au ataahirisha mwaka? labda angekuwa Lema au kamanda yeyeto wa CDM

  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
   

  Attached Files:

 4. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hayo maneno ya mfa maji zipo nyingi za aina hiyo zilizokwisha tolewa na CDM, mbona kama zile za madai ya mauaji ta watu wa Tarime na ziko mahakamani au hakimu wa huko Tarime hajui sheria?

  LISSU mbona haitwi mahakamani? au kwa vile alikuwa anaongelea ndani ya mhimili mwingine? CDM sasa naona wamebaki kuvizia kauli za viongozi ili iwe ndo ushahidi wa kesi ya LEMA? mbona CDM wanakuwa wa kwanza kushangilia ushindi hata kabla matokeo kutangazwa katika chaguzi mbalimbali?

  Tume ya Uchaguzi haijui sheria? Waache hizo bana, watafute hoja za msingi za kuongelea.
   
 5. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Aliripoti hii si Grace Macha. Yule mie namfahamu fika njaa sana na fitina za mambo fulani, labda angekuwa mwingine.
   
 6. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Grace Masha anaripot kwenye Tanzania Daima na Mwananchi ? Mkuu usiwe bias kihivyo hata kama karipoti ni yeye hapa tunapaswa kuijadili content na siyo mtu
   
 7. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mwananchi la tarehe ngapi?
   
 8. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Kwa nini Nape aseme ana Uhakika kuwa watashinda kesi??

  Hapo kuna walakini, wenye akili zao lazima watagundua kuna mambo hapo. Nape ni mvujishaji wa siri za CCM. Kuna mkakati umepangwa, hivyo NAPE alijisahau akaropoka, ona sasa inavyomcost.

  Hata Gazeti lao la Uhuru na Mzalendo waliandika hayo maneno ya NAPE.

  Naomba huyo wakili wa Mheshimiwa Lema, apate nakala ya Gazeti la Uhuru na Mzalendo.

  Ole wako NAPE- hata ulikuwa unavujisha Siri za NEC kwa CCJ
   
 9. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Nape vs hakimu TUSUBIRI TUONE KM HAKI ITATENDEKA
   
 10. Kamkuki

  Kamkuki JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  mbwelambwela kama bi,omr si watu wa kupewa nafasi ktk jamii ya leo, maana mpaka hapo anatia mashaka kama ni mtz anayezijua sheria za nchi yake!!
   
 11. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,555
  Likes Received: 4,682
  Trophy Points: 280
  Kama jambo hulijui kwa nini usikae kimya ukaficha upumbavu wako?
   
 12. E

  ESAM JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 962
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Tatizo wewe kichwa chako kimejaa maji ndiyo maana hata kama hoja iko wazi kwako huwez kuona labda ile inayounga mkono ufisadi na upu-uzi na ujambazi wa Magamba. Suala sio kutoa maonin bali ni maoni juu ya jambo gani na kwa namna gani. Na kwa taarifa yako yale ya Nape sio maoni bali alisema tutalichukua jimbo la Arusha mjini kana kwamba amepewa uhakika na mahakama kwamba ushindi wa Lema lazima utenguliwe na hivyo uchaguzi mdogo kufanyika.

  Wakati mwignine tujaribu kuweka ushabiki wa vyama pembeni na kuongelea hoja iliyoko mbele yetu na bila kuegemea upande wowote ule.
   
 13. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,152
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  Leo tarehe 29/10/2011, umelipitia? Soma sehemu kichwa cha habari kimeandikwa ''mbunge awakimbia polisi''
   
 14. M

  Makupa JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Maji yako shingoni Lema jiandae kuachia ngazi CCM msimamisheni yule kijana wetu Nasari
   
 15. O

  Omr JF-Expert Member

  #15
  Oct 29, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hizi ni kelele za mfa maji, nyie wasiwasi wenu ni kuwa Huyo Jambazi atashindwa hiyo kesi na uchaguzi utarudiwa. Nape aliyo sema wala si sababu. Na msitake kujifanya mnajua sheria wakati mambo yanauma kwenu. Kesi ngapi mlishatoa hukumu hapa JF?

  Haya maneno ya Nape ni mawazo yake binafsi na nyie magwanda kama hamjiamini basi poleni sana. Ombeni mungu uchaguzi usirudiwe lasivyo jimbo linakwenda CCM mbele ya macho yenu.
   
 16. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #16
  Oct 29, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Uhuru wa mahakama kwa kutoa maoni?
  OTIS.
   
 17. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #17
  Oct 29, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  je helikopta itatumika kumpeleka nnape mahakamani arusha?
   
 18. P

  Paul S.S Verified User

  #18
  Oct 29, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Siasa za nchi hii bana we acha tu
  Sasa kwa kauli hii ndio anaitwa mahakamani au ni mbinu tu za kucheleweshs kesi
   
 19. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #19
  Oct 29, 2011
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Enyi makamanda wa a town uchaguzi ukirudiwa wala msihofu nyie kazi yenu iwe ni kupiga kura tu siku ya uchaguzi ,kampeni na ulinzi wa kura tutakuwepo siye makamanda toka mwanza mbona patamu na magamba hawatafurukuta.Wenyewe hapa tuna hamu ya kurudia uchaguzi wa ilemela ajabu mashahidi wa magamba wanaingia mitini daily
   
 20. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #20
  Oct 29, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,769
  Trophy Points: 280
  Siasa za maji ya chooni zimemponza huyu green guard.
   
Loading...