Nape Nnauye, kujiuzulu ni uungwana

Chifu Mkwawa, umeichambua vizuri kwa kiasi chake na ninachongoja ni kuona Mh. Nape atakapopita (anaweza akawa ameisoma tayari) ni lazima aache maoni yake na hii itatusaidia kujua 'udodoki' wake ulipo!

Chief Mkwawa, Siko la kufa halina dawa. Nilimwambia Nape hapa hapa JF mapema wakati akichaguliwa ya kwamba ni kawaida ya JK kuwachagua wale wanaopiga kelele na kuwapa lishe, mamlaka yasiyoweza kutoa maamuzi isipokuwa kuwakwaza zaidi na hata kuharibu majina yao. Wapo vijana wengi CCM ambao walikuwa mwiba wa Mafisadi na wameenguliwa ktk uchaguzi wa UVCCM, kisha wamefungiwa ktk zizi la mbuzi walikilishwa majini kwa majira ili hali wengine wakila kwa marefu ya kamba zao. Hii sisi wenye hekima huita - HIFADHI ya MBUZI.

Mbuzi alofugwa zizini akilia sana huwa ni dalili ya njaa, wanachokupa ni lisho la majani na maji kukidhi njaa yako ukiwa bado bandani. Na ukisha shiba unajiona beberu ndani ya zizi usione uzio ule upo kwa ajili yako usitoke bandani na wala usije kuliwa na mbwa mwitu. Umehifadhiwa tu mdogo wangu.

Chifu Mkwawa, umeichambua vizuri kwa kiasi chake na ninachongoja ni kuona Mh. Nape atakapopita (anaweza akawa ameisoma tayari) ni lazima aache maoni yake na hii itatusaidia kujua 'udodoki' wake ulipo!
Hivi nyie hamumjui Nape atakuja hapa na maneno ya dharau hamtaamini.

Chief Mkwawa

Asamte sana kwa Ushuri wako Mzuri Kwa Huyu ''DOMO KAYA BWANA MDOGO NAPE NAUYE''

Naomba kila anapoamka asubuhi asikilize ule wimbo wa Mwananziki wa kizazi kipya kutoka Kenya JAGUAR, Wimbo unaitwa KIGEUGEU

Ndipo atajua Boss wake/Mwenyekiti wa chama chake (JK) ni KIGEUGEU

Wanasiasa Vigeugeu

Nani kakuambia unaweza kusukuma gari ukiwa ndani ya gari? Kama Nape ni mwanamageuzi wa kweli na ana nia ya dhati ya kutetea maisha ya walio wengi na ameshatambua ufisadi wa ccm inampasa sasa atoke nje ya gari ili aweze kulisukuma. Kinyume na hapo nitamwona kama msanii tu

Nape my dear brother. We trust on your brother, but umetuangusha kijana mwenzetu. Hivi kinachokufanya usichukue hatua kwa msimamo wako ni kipi? Hapa umesalitiwa na wenzako wote. Yu wapi Samwel Sitta, Olesendeka, na wenzake wengi wanaojiita wapinga ufisadi. Hapa mngeungana pamoja mngelishinda hii vita.

Hii vita mlikuwa hamjui adui zenu ni akina nani. Hapa mlikuwa mmezungukwa na maadui wengi sana lakini hukupata hekima ya kuwajua. Sasa umewatambua maadui unaopaswa kupambana nao. Sasa uamuzi upo kwako wewe kama kusuka au kunyoa.
Tulitabiri CCM haiwezi kubadilika, Leo hii Sita hajaongea chochote kuhusu kusafishwa kwa Rostam, Olesendeka, Mama Kilango, January Makamba wote ni kimya kabisa.

Rostam kasafishwa tena kwa mara ya pili kwa mbwembwe na vifijo na Rais Mstaaafu sasa nani tena ndani ya CCM wa kuguna?

Mkwawa analysis yako imetulia na ukweli umeusema bila kumungunya maneno - Rostam naye kwa uwoga wake anakula matapishi yake kwa kuzifakamia siasa uchwara alizozitapika bila kimyaa.

Chief Mkwawa, umenena. Nape ujumbe mzito huo, utakufanya ujipambambanue kuwa wewe ni nani.. Kazi kwako.

To Nape this is employment opportunity! To resign!!, so then, where do you want him to go? He hasn't more skills than then and there, he hasn't options than bending and be flexible as far as possible provided he earns what he aims, that is how our politicians are, they have politics on both hands and nothing in their head.

Your advises are the best possibilities but they can't work for someone who hasn't gone to school and hasn't somewhere to go from his own experiences, skills and education, try to advise someone else as for the concerned guy this looks like misleading advise.

Nape it is high time now kufikiria kuachana na magamba kwani huu mpango wa kampeni Igunga ni wanakudhalilisha na upiganaji wako unakuwa hauna maana think twice na uachane na magamba bora ukaendeleze chama choko cha CCK

HUYU JAMAA NI KILAZA SANA! Hawa ndo vijana maslahi

chief Mkwawa hili umenena,yaani hakuna chakukosoa wala kujazia ujumbe umefika kama ana akili safi na timamu na kama akili yake bado ipo kwenye moto bila shaka atakuwa amekuelewa

Sina cha kuongeza wala kupunguza nisije punguza radha ya ujumbe, napenda ufike kama ulivyo. Na mwenye macho haambiwi tazama!

ni aibu! atajificha wapi?anaowasafisha wanazidi kujaa matope, anaowachafua wanazidi kutakata na kuwa Lulu!

Hawezi kujiuzulu kwa maana hakuwahi kufanya kazi nyingine zaidi ya kuwa mwanasiasa sasa mnataka ajiuzulu akafanye kazi gani

To Nape this is employment opportunity! To resign!!, so then, where do you want him to go? He hasn't more skills than then and there, he hasn't options than bending and be flexible as far as possible provided he earns what he aims, that is how our politicians are, they have politics on both hands and nothing in their head.

Your advises are the best possibilities but they can't work for someone who hasn't gone to school and hasn't somewhere to go from his own experiences, skills and education, try to advise someone else as for the concerned guy this looks like misleading advise.

Arafat, this is more than punching Nape from both left and right hadi kwenye map**b*, ila Mzee Makamba alimwambia kafungiwa duniani hadi mbinguni! I miss his jokes...

Makamba.jpg

Bora mwenzake alijivua gamba na kuachana na siasa uchwara sasa anafuga ng'ombe zake!!

'That is how our politians are, they have politics on both hands and nothing in their head' by Arafat.

Ndani ya hicho chama wote ni magamba ila inategemea ni wakati gani gamba lako linaonekana na linahitaji kutolewa.wakongwe wanajua jinsi ya kuficha ugamba wao...wakiona ugamba wao unakaribia kuonekana wanakua wadogo na kujipendekeza kwa mkuu wa magamba.
Sasa hawa wakina NEPI namaanisha NAPE hawalijui hilo,hawajui kwamba kwenye chama chao mda wowote unatolewa kafara hasa kama hauna upendo kama wa ALBWARD (mzee wa kempisk).
Namshauri nape atafakar na kuchukua hatua

Ni vijana wachache sana kwa tanzania wenye msimamo wa kusimamia kile wanachokiamini.
Nape ushauri uliopewa hapo juu ni muhimu sana kama kweli unaipenda tz na kama kweli unapenda kusimamia yale unayoamini.!! Embu tudhihirishie kua kelele zako za tangu zamani hazikua ni njaa ya kutafuta mshahara mnono!!

Lakini ndugu zangu mi siegemei upande wa magamba tu!! wapo vijana wengi wamewahi kujitokeza katika kupigania maslahi ya nchi lakini wote wameishia kuonyesha njaa.
Yule kijana wetu kabwe aliyekua anatetea maslahi ya mapato ya madini yetu sana siku hizi kaishia wapi?....kwa nini vijana mnapenda maisha ya kununuliwa sana!!! Umaskini mmbaya sana ndugu zangu.

41 Reactions
Reply
Back
Top Bottom