Nape nnauye kanunuliwa na mafisadi?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape nnauye kanunuliwa na mafisadi??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jul 18, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,351
  Likes Received: 5,653
  Trophy Points: 280
  Ndugu wapendwa kweli naona kunaitajika kuwa na wakina pengo zaidi ya alfu moja tunapokwenda....huyu bwana ni kaka yangu jamaa yangu na zaidi ya yote amenisaidia katika baadhi ya mambo yangu kiisias...tangu alipoanza kuiibua ile dili ya kina lowasa kuuza ofisi za CCM pale umoja wa vijana ...wakakimbizana ....walipoona mmmhh kijana ana madhara wakamhakikishia kumpa ulaji kwa kila uchaguzi....sikatai kama ni mwananchama wa ccm wajibu wake kufanya ama kutimiza ilani ya chama....

  Leo hii natoka kumwangalia kwenye TV akisema viongozi wa dini achaneni na serikali kabisa...katika moja ya maulidi alioalikwa kama mgeni maaluum...kama ni mafisadi waombeenii wabadilike na si kushindana na serikali ama kukimbizana na serikali........,wapeni nafasi serikali ...namnuukuu..............sasa huyu bwana ana maana viongozi wa dini wakiona serikali inaiba wakae kimya tu...anaweza kutuonyesha .....wapi pameandikwa viongozi wa dini wasiiirekebishe serikali kama wanakosea...........mmmmmmhhhhhh nnape


  unatutisha ndugu
   
 2. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Unajua waTanzania wengi wanaamini.
  1. Siasa ni kazi na chanzo cha mapato
  2. Bila CCM huwezi kufanikiwa kupanda ngazi ya mafanikio, kiuchumi au kisiasa
  3. Mambo mazito yanazungumzwa kwenye vikao, na walio nje ya vikao si haki yao kujua
  4. Tanzania ni mali ya wachache.

  Kwa hiyo siwezi kushangaa huyu Kijana wa Mzee Moses tunaye mfahamu kuwekwa chini na kueleweshwa kuwa hatuendi hivyo. Watu makini tulishajua kuwa yupo nao toka siku ile JK aliposema hawajamfukuza uanachama wa CCM hata kama UVCCM watamvua uanachama, Pale kengere ya tahadhari ikagonga wala hawamtoi kwenye NEC hata atofautiane na akina Nchimbi 100X
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,604
  Trophy Points: 280
  Soon nae atapewa u DC yote yataisha ataenda akale maisha wilayani huko njaa na kelele kwisha habari yk....sasa wanampika na kumjenga ili aje awe DC mtaona akipata cheo atakavyotulia....kama hayupo vile...siasa TZ ndiongazi la sivyo uwe upinzani...labda ameshakalishwa akapewa facts na ahadi.....
   
 4. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Kana njaa haka kabwana!lazima akaunti yake 'ilimwagiwa maji' kakaamua kutulia!pia wamekahakikishia kwamba kasubiri tu katashika mpini!

  Kinachonisikitisha na hawa 'vijana' ni ile hali ya kuzitumia vibaya IQ zao,wanafichua maovu kwa njaa zao tu!wakihakikishiwa ''maisha-bora'' wanasahau kuna watu hawana uhakika wa mli hata mmoja!

  Mdogo wangu Nape,sitaki uhame ccm LAKINI SIPENDI KUONA UNATETEA DHAMBI!kinyume na hili naomba nikutahadharishe nape,hutafika popote b'se we can't accept this non-senses in our existence!kizazi hici tumeshajitolea maisha yetu for our future generation!I AM WARNING YOU

  Waacheni wahubiri watimize wajibu wao!AM WARNING YOU BROTHER
   
 5. B

  Bob K Member

  #5
  Jul 18, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa kweli upande fulani ni lazima viongozi wa dini wakemee ufisadi kwani wao ni walezi wa kiroho mpaka kwa hao viongozi ambao huwaheshimu sana hata bwana mkubwa akiambiwa shehe mkuu au baba askofu fulani anahitaji kuonana na wewe lazima ampe nafasi haraka sana,kijana katereza lakini tusimtenge kwenye kambi ya wapinga ufisadi ni mapema mno kumuhukumu
   
 6. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #6
  Jul 18, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Hapa ndipo nashindwa kuwaelewa Watanzania - hivi tumelogwa ? Toka lini ukapanda maharage ukavuna nanasi, toka lini ukaogelea kwenye tope ukatoka msafi, toka lini ukashiriki wizi ukadai wewe si mwizi, toka lini ukajipaka kinyesi ukanukia marashi, toka lini ?

  Nape kama walivyo makada wengi ndani ya CCM - wamevuliwa, wamepikwa na wameiva na sasa hawaoni, hawasikii wala hawanusi. Adui yao mkubwa ni yule anayethubutu kuwanyooshea kidole kwa ulafi wao - hapo wanakuwa na mshikamano wa kutisha.

  Shuhudia usalama wao unapokuwa hatarini - hapo nguvu zote zitatumika hata ikibidi kuvunja sheria, kutumia vitisho na kusema uwongo. Hapo hamna tena utawala wa haki wala usawa - ni survival at all cost na watajilinda kwa kutumia nguvu za dola ikibidi.

  Vijana kama Nape ni hatari zaidi kwani hawayawezi maisha nje ya CCM - wamezaliwa, wamepakatwa na wamelelewa humo toka utotoni. Wamekua wakiamini CCM ndio baba na mama na uongozi wa nchi hii ni halali yao kuurithi - si ulimilikiwa na baba zao ?
  Kaazi kweli kweli..:(
   
 7. H

  Honey K JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2009
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wakubwa heshima kwenu!
  Nimelazimika kuingia mapema kujaribu kuweka mambo sawa ili mjadala uwe na manufaa.
  1.kwa aliyeangalia vizuri taarifa ile wakati mimi nazungumza nilichokisema ni kuwa, MCHANGO WA VIONGOZI WA DINI KATIKA AMANI NA UTULIVU WA NCHI YETU NI MKUBWA MNO NA WANASIASA WAUHESHIMU. LAKINI PIA NIKASISITIZA KIZAZI HICHI CHETU KUKABILIWA NA KANSA MBAYA YA UFISADI NA RUSHWA NA KUWAOMBA VIONGOZI WA DINI WASAIDIE SERIKALI KATIKA VITA YA KUKIOKOA KIZAZI NA KANSA HII.
  2. KAMWE KATU HAKUNA BEI YA UTU WANGU,NA KWAKWELI KUSEMA NAPE KANUNULIWA KWANGU NI ÑATUSI MAKUBWA.NACHUKIA UFISADI LEO KULIKO JANA..NA GRAFU ITAENDELEA KUPANDA YA KUCHUKIA UFISADI NA KUUPIGA VITA.

  3. NAAMINI KATIKA UZALENDO KWA NCHI KWANZA CHAMA BAADAE,NIMEKUWA NIKIYASEMA HAYA NA KUYAAMINI HADHARANI,HIVYO SI SAHIHI KUSEMA ETI KWA NAPE CCM NDIO BABA NA MAMA YAKE. KUMBUKENI NILIKUWA TAYARI KUFUKUZWA CCM KWA KUSIMAMIA HAKI LEO KUTUMIA MANENO YA KEJELI KAMA HAYA SI SAWASAWA NADHANI.

  4. NAAMINI YAPO MAMBO HAYAWEZEKANI KWA NGUVU YA SIASA PEKEYAKE INAHITAJIKA NGUVU YA DINI/MUNGU,NA KWAKWELI KATIKA HILI NIMESOMA WARAKA WA MAASKOFU TOKA MWANZO MPAKA MWISHO SIJAONA KASORO NATAMANI TUUCHUKUE UWE SEHEMU YA ILANI YA CHAMA. NAWAPONGEZA MAASKOFU.

  Sasa tujadili.
  Nape Nnauye
   
 8. H

  Honey K JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2009
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Na kwakuanzia ni mimi niliyetoka hadharani na kuwaomba viongozi wa dini wawafukuze mafisadi kwenye nyumba zao za ibada,leo kugeuka jiwe siwezi kwani naamini hao mafisadi wanapaswa kuwa harrased kwa nguvu zote ili kukifunza kizazi chetu kuwa ufisadi sio style ya maisha balii ni wizi na unyang'anyi. Kama tunachoma moto wanaopora simu ya shilingi hamsoni elfu kwanini hawa wa mabillioni wasiadhibiwe pia?
   
 9. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280

  Asante Mkuu Nnauye, kwa kuja kutoa ufafanuzi na msimamo wako. Naona tetesi hii haina maana tena wala hakuna haja ya kujadili kwani hoja ya mjadala ilikuwa juu ya tamko lako dhidi ya waraka ambapo umekanusha. So, naona thread ife tu sasa.
   
 10. H

  Honey K JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2009
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mie nashauri tufungue thread tujadili kwa kina waraka wa kanisa katoliki, tusijadili kwa jumla jumla bali hoja baada ya hoja, yaani kwa mfano, WARAKA WASEMA NINI JUU YA ELIMU YETU NA SISI INDIVIDUALLY TUNASHAURI NINI!
   
 11. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #11
  Jul 19, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  GOOD!i was going to..................
  anyways GOOD STUFF young star
   
 12. M

  Makabe Member

  #12
  Jul 19, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Huyo lazima aegemee kwenye siasa na kuwabeba mafisadi. inasemekana shule ilimshinda India alipokuwa akilipiwa na bwana mkubwa mmoja wa serikali iliyopita, sasa tutegemee nini?
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Jul 19, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Makabe, mbona kama hiyo treni imeshapita??? Nape kajieleza muda si muda

  Nape: Watu wote hukosea na kuteleza si kuanguka, naamini maneno yako kwa sasa na nasubiri matendo...you still have my vote so far!!!!
   
 14. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #14
  Jul 19, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280

  Mpiganaji NAPELELE heshima mbele!!!!

  katika vijana ndani ya ccm wanaoweza kutunishiana misuli na wapambanaji wa CHADEMA,wanaharakati na wapinzani kwa ujumla ...bila shaka wewe ni mmoja wao,unapigana vita hii kwa imani na vitendo...

  HUU NI UDHIBITISHO KUWA CCM HAIJAISHIWA NA WAADILIFU ..TATIZO UMILIKI WAKE UMEHAMA KUTOKA CCM YA BABA WA TAIFA YA JEMBE NA NYUNDO[Kuwakilisha wakulima na wafanyakazi]...HADI CCM YA MAFISADI ..hasa baada ya azimio la zanzibar...na utekelezaji wake unaoendelea kwa kasi!!! chama kimehama kabisa!!...na wajinga wanataka tuamini ndio ccm ileile ....sidhani..,lazima kama ccm inataka uhalali ..irudishwe kwa wenyewe...

  TUNAPOONGELEA RUSHWA,MAADILI NA SERA KWA UJUMLA ...tuondoe siasa za chama ..lazima kama taifa tukutane bila kujali vyama na tushirikishe vionggozi wa dini ,jadi na wa vyama vya hiari..TUJE NA DOCUMENT ...document itakayoitwa MISINGI AU NGUZO ZA KUENDESHA TAIFA...naelewa msingi mama ni katiba ..lakini kwa sababu za kisheria katiba haiwezi kubeba sera,na baadhi ya miiko au imani...misingi ya taifa itatakiwa kutekelezwa na kiongozi yeyote anayekuja ...tusiyumbe ,watu wa usalama na jeshi pamoja na jukumu la kulinda katiba watakuwa na jukumu la kuhakikisha hakuna mtu anacheze MISINGI YA TAIFA!!

  niwape mifano midogo ya mataifa yanayoendeshwa kwa misingi ya taifa badala ya sera ni marekani na uingereza ...akiingia rais kabla ya kuapishwa anapewa miezi miwili kwanza kama induction ya kumtoa kwenye stress za ahadi za kisiasa kwenye kampeni .....na kumuingiza kwenye dola...,utendaji wa kiongozi kwa namna yeyote akishaapishwa hautagusa maamuzi yanayohusu taifa hata kama hayaendani na sera zake za chama ,kwa sera kuu ndiyo hiyo.Watu walifikiri mfano akiingia obama basi angefuta yale yote ya bush....lakini hawajuwi kuwa kwenye tamko lililopo kwenye foundation za wamarekani ..uamuzi wa kuteka muslim or arab world ili kujijengea nguvu ya mafuta uliafikiwa toka enzi ya JIMMY CARTER .....[democrat].....REAGAN ,BUSH ,CLINTON NA BUSH jr Wote waliutekeleza aidha kwa kuendelea na inteligenzia au vita kamili....

  Ameingia obama watu wanafikiri anaenda nje ya misingi ya zera za ulinzi za marekani...baada ya kukutana na majemedari na wakuu wa CIA ,FBI etc ...ahadi zake zote za kisiasa ziliyeyuka na akaendelea na marshall plan iliyopo kwenye sera ya taifa.....kwa approach tofauti ..kwenye millitary strategy ni kama vile wame retreat...ili ku build up....na obama anatumiwa kutokana na charisma yake kuleta maelewano..na muelekeo mpya wa kimahusiano..lakini hata siku moja marekani haiwezi kuacha kuendelea na utekelezaji wa sera yake yoyeto...iwe ya ghuba,korea,afrighanistan,africa[especially horn of africa]....,russia ,sera ya nuclear na makombora ya masafa marefu[ICBM]..ETC.Watu wanatulizwa ili marekani itibu makovu yake ...huku inteligenzia ikifanya kazi ya ziada ..baada ya hapo HITMAN[REPUBLICANS] wanarudishwa ....kutekeleza ..mkakati kamili !!

  Nimeongelea hayo hapo juu ili kuweka changamoto juu ya imani kwa nchi zaidi ya chama ....ni muhimu kama taifa tuwe na sera yetu.Sera za chama zitakuwa ni kwa ajili tu ya kutofautisha vipaumbele,kama uingereza wakiingia LABOUR ...sera hazibadiliki ila approach hubadilika kidogo..na priorities huegemea zaidi kushoto...au watu wa tabaka la chini na kati hupendelewa zaidi,wakati wakiingia CONSERVATIVES hali huwa tofauti....wapiga kura wa nchi hizi wana tabia ya kupiga kura kwa kuzingatia mahitaji ya wakati husika!
   
 15. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #15
  Jul 19, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,968
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  Tukiwa na upeo mdogo wa kuchambua mambo tutamlaumu kila mmoja.Lakini tujiulize wafadhili wa makanisa na misikiti ni wasafii.Tazama orodha ya wote wazito wanaokuwa katika kamati mbalimbali za kuendeleza kanisa au jimbo la kanisa jee wasafi.Mimi naona nauye ameongea hoja haswa.Viongozi wa dini waache kabisa kuongelea masuala ambayo hawayaelewi.wazungumzie hoja ya mtu kupata ufalme wa mungu,
   
 16. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #16
  Jul 19, 2009
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  As Frank Uhahula-Now DC Tarime?
   
 17. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #17
  Jul 19, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  DU NAPE; NA WEWE SIKU HIZI UNATIKISA KIBERITI CHA KANISA!! MBONA MAELEZO YAKO HAPA NA ULICHOSEMA NI TOFAUTI; KANISA ULILIKATAZA KUINGILIA SIASA HAPO HAPO UNATAKA KUCHUKUA WARAKA UWEKE KTK ILANI: SO U MEAN KTK CCM HAMNA WAANDAAJI WA ILANI; AU ILANI NYIE NI MAANDISHI; UNATAKA KUSEMA BAADA YA ENZI ZA MWALIMU UFISADI UPO KTK MAANDIHSI KTK VITENDO ZERO
  JENGO LA UVCCM NA MRADI WA LOWASSA UMEFIKIA WAPI? JE UMEFIKIA WAPI KUPINGANA NA RICHMOND? EPA? MEREMETA? kGODA?TANGOLD? MAANA UMO MLEMLE NI RAHISI KUJUA UPDATE. UMEFANYA CHOCHOTE CHA MAANA AU KIJIWENI UNATUPIGA KWA POROJO TU? ANYWAY SIKU HATUTAKI POROJO ETI UNATAKA KUSEMA UNAWEZA KUKATA MTI ULIOUPANDA INAWEZEKANA KWELI???????
   
 18. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #18
  Jul 19, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Binafsi Nape ulinivutia sana ulipo simama kidete kupinga ufisadi wa jengo la UVCC,
  Hapa umejieleza, lakini twambie point blank, hukusema kweli kwamba Kanisa lisiingilie siasa? ulikuwa una maana gani hapo?
  Make usije kuwa na Kauli mbili, kwenye TBC ulisema hivi, na hapa unatupinga changa..
   
 19. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #19
  Jul 19, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kaka, unauzungumziaje waraka huu wa Padri Karugendo?

  WAKATI wa uchaguzi mkuu wa 2005 nilikuwa mratibu wa Mkoa wa Mtwara, wa waangalizi wa uchaguzi kupitia TEMCO. Pia nilikuwa nimepatiwa kazi ya kuandika mada juu ya upinzani mkali ndani ya vyama wakati wa kura za maoni, na upinzani mkali baina ya vyama vyama vya siasa wakati wa uchaguzi mkuu.
  Baada ya uchaguzi, mwaka 2006, Redet iliandaa mkutano wa hali ya kisiasa Tanzania, uliofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mimi na wenzangu tuliokuwa tumepewa kazi ya kuandaa mada mbalimbali juu ya uchaguzi mkuu wa 2005, tulipewa nafasi ya kuwasilisha mada zetu. Na baadaye mada hizi zilijadiliwa na wadau mbalimbali waliokuwa wamehudhuria mkutano huo.
  Mada yangu ilijikita sana juu ya matumizi ya fedha kwenye kura za maoni ndani ya CCM. Kwamba ushindani mkali uliojitokeza ndani ya CCM kule Mtwara Mjini na Vijijini uliongozwa na nguvu ya fedha kuliko kuangalia sifa na uwezo wa mtu.
  Wasomi wengi waliojitokeza kugombea ubunge wa kiti cha Mtwara Mjini, walitupwa nje na kumpitisha mtu aliyekuwa na kisomo cha kawaida, lakini alikuwa mtu mwenye fedha. Alitembeza bahasha wakati wa kura za maoni. Pia nilionyesha jinsi ushindani mkali uliojitokeza kati ya CCM na NCCR-Mageuzi Mtwara Mjini uliongozwa na nguvu ya fedha.
  Ushindani ulikuwa mkali kiasi kwamba viongozi wa juu ndani ya CCM, walikuwa wakipigana vikumbo kuja Mtwara kuokoa jahazi. Misafara ya magari ilikuwa mingi, na ni wazi kulikuwa na matumizi makubwa ya mafuta. Dalili kwamba fedha nyingi zilitumika wakati wa kampeni.
  Vitu kama khanga, sukari na sabuni vilikuwa vikigawiwa nyumba hadi nyumba. Kule Mtwara Vijijini ambako mwanzoni walimkataa mgombea mbele ya Rais Jakaya Kikwete, walilainishwa na nguvu ya fedha na kusahau kabisa malalamiko yao juu ya mgombea. Kampeni zilipopamba moto walianza kuimba nyimbo za kumsifia huyo mgombea.
  Nakumbuka vizuri swali nililokuwa ninarudia mara kwa mara wakati nikiwasilisha mada yangu lilikuwa ‘fedha hizi zinatoka wapi’. Kusema kweli nilishuhudia fedha nyingi zikitumika wakati wa kampeni. Nilishindwa kuelewa kama zilikuwa zikitoka kwa watu binafsi au zilikuwa ni za chama.
  Na kama zilikuwa zinatoka kwa mtu, alikuwa na biashara za namna gain. Na kama zilikuwa ni za chama, mbona nilikuwa nimeshuhudia sehemu mbalimbali za Tanzania, watendaji wa CCM, wanaishi muda mrefu bila mshahara?
  Wakati ule nilikuwa ninashindwa kuelewa ni wapi fedha hizo zilizokuwa zikitumia kwenye kampeni zinatoka. Leo nina jibu! Baada ya kashfa ya EPA, swali langu lina jibu!
  Katika mada yangu, nilionyesha wasiwasi wangu wa chama kutawaliwa na fedha, badala ya kutawaliwa na fikra na sera. Pia nilihoji mambo ya kushangaza yaliyojitokeza kwenye kampeni za CCM; mfano mgombea wa CCM alikuwa anajigamba kwamba ana uraia wa nchi mbili - Tanzania na Msumbiji.
  Hakupata shida! Maofisa Uhamiajia waliendelea kumsikiliza na kumshangilia. Tanzania, nchi inayowafukuza watu ambao ni wahamiaji haramu, inamkumbatia mtu mwenye uraia wa nchi mbili kwa vile ni mgombea wa CCM, ni jambo ambalo sikulielewa wakati ule na hadi leo hii silielewi, maana nina imani jamaa huyu bado ana uraia wa nchi mbili.
  Pia, nilielezea jinsi viongozi wa serikali Mtwara, walivyokuwa wakimpigia kampeni na kumuunga mkono jamaa huyo kwa vile walikuwa wakifanya biashara pamoja. Kwa ujasiri na kwa kujiamini nilifafanua hali ya ufisadi iliyokuwa inaishambulia CCM na kudhoofisha demokrasia nchini. Na kama kuna kitu ambacho ni adui wa demokrasia, basi ni nguvu ya fedha.
  Hoja kubwa katika mada zetu ilikuwa ni kama uchaguzi unaimarisha au unadhoofisha demokrasia. Baada ya kuwasilisha mada yangu, Nape Nnauye, alinyanyuka na kunitukana. Siwezi kusahau wakati ule katika maisha yangu.
  Ingawa sikutarajia kuungwa mkono asilimia mia moja kwenye mada yangu, lakini sikutarajia matusi. Nilitegemea nguvu ya hoja badala ya hoja ya nguvu.
  Kusema ukweli wakati Nape anachambua mada yangu, hakutoa hoja, bali alitoa matusi. Alinitukana kwa kusema uongo na kukisingizia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutumia fedha nyingi wakati wa uchaguzi mMkuu.
  Kwamba siku za nyuma alikuwa akiniheshimu sana kwa makala zangu nilizokuwa nikiandika, lakini siku hiyo kwa vile nilisema uongo na uzushi dhidi ya CCM alinidharau. Aliwashambulia watu wote wanaoichafua CCM na kuipaka matope.
  Alisema CCM ni chama safi chenye watu safi. Na kwamba ushindi unatokana na mapenzi ya watu.
  Nakumbuka sikujibizana naye kwa kuogopa sote wawili tusionekane ‘hamnazo’. Tunashauriwa katika maandiko matakatifu kwamba tusirudishie tukano kwa tukano. Baadhi ya wachangiaji walijaribu kumrudi Nape, lakini yeye kwa jeuri na kiburi cha chama, aliendelea na matusi yake.
  Wakati wa kunywa chai, nilimfuata na kumpatia ushauri wa bure. Kama ni mtu anayetunza kumbukumbu, atakuwa anakumbuka vizuri ushauri wangu kwake. Sikumsikia tena baada ya siku ile aliponitukana hadi juzi alipojitosa kwenye vyombo vya habari na kushutumu ufisadi ndani ya chama chake kisafi na chenye watu wasafi.
  Sasa wakati yeye mwenyewe, Nape Mnauye, anawashutumu baadhi ya wana-CCM kuwa mafisadi, ninachoweza kumwambia ni ‘Nape Nnauye kuwa uyaone.’
  Waswahili wanasema kuishi kwingi ni kuona mengi. Mimi niliposema ufisadi ndani ya CCM nilitukanwa. Yeye naye ameuona ufisadi ndani ya chama chake na kusema! Nina imani atashangiliwa kama itakuwa kinyume, huko ndiko kukua na kuyaona mengi!
  Nape alifikiri mimi ni msaliti, alifikiri mimi siipendi Tanzania. Kwa maneno yake alinitaja kama mpinzani na kama nilivyoona, wapinzani kwake ni wasaliti.
  Ingawa kweli sina chama na wala mimi si mwanasiasa. Je, yeye leo hii ni msaliti? Au ni mzalendo anayekerwa na ufisadi? Ni miongoni mwa watu wanaokerwa kuona nchi inatawaliwa na fedha badala ya kuongozwa na fikra pevu? Imekuwaje watu aliowashangilia kuwa wasafi jana, leo anawatuhumu kwa ufisadi? Au ana lake jambo?
  Nina shaka kama ataweza kuwa mwenyekiti wa vijana wa CCM. Mwaka ule alinitukana mimi kwa kuwalalamikia CCM, kukubali kuongozwa na fedha badala ya kuongozwa na fikra pevu na sera. Leo hii yeye analalamika kwamba kuna mafisadi ndani ya CCM, na kwamba mafisadi hawa wanaweza kuingilia uchaguzi.
  Tumejenga utamaduni wa kuongozwa na fedha badala ya fikra. Hivyo kwa vile Nape anapigana vita na mafisadi, hawezi kufanikiwa kuwa mwenyekiti. Atakayechaguliwa ni yule aliye upande wa vizito, ni yule anayekubali kuongozwa na fedha. Mwenyekiti wa vijana ni muhimu sana kwa uchaguzi mkuu wa 2005. Hivyo makosa hayawezi kufanyika.
  Ni bahati mbaya kwamba Nape amechelewa kuona ufisadi uliotanda ndani ya chama cheke cha CCM. Ninasema ni bahati mbaya kwa maana amefumbua macho amechelewa, kama angelifuata ushauri wangu, akafumbua macho mapema, labda angefanikisha matumaini yake.
  Hata hivyo, yeye bado ni kijana, bado ana wakati wa kusahihisha makosa aliyoyafanya, bado ana muda wa kujiunga na wale wanaoamini kwamba ili chama kiwe kizuri, kiwe cha Watanzania maskini na wanyonge, ni lazima kiongozwe kwa fikra. Sasa awapishe wenye fedha wachukue nafasi zao!
   
 20. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #20
  Jul 19, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280
  mtu kama kingunge ...amekuwa wa mwanzo kujibu waraka wa kanisa katoliki kwa sababu kwa miaka mingi ..kingunge kwa wale vijana wa zamani mnakumbuka mara zote amekuwa mwenyekiti wa kamati ya chama inayoandaa ilani ....au ile the so called MIPANGO YA MIAKA KUMI AU 25.....Kwa mfano mwaka 1987 ...kingunge aliandaa sera au mwelekeo wa miaka 25...nitatafuta kile kitabu niangalie kama kilikuwa ni hekaya au kuna utekelezaji wowote lifanyika..kwa sababu ule mpango utekelezaji wake unaishia mwaka 2012.....[natoa changamoto tuutafute wote]

  ilani ya wakatoliki ...haiana lolote baya kwani haiongelei ubatizaji...nadhani kama kuna mazuri yanayofaa kwa taifa kuyafuata yawe adopted ..tena bila hata kutoa bibliography ..kama yamenakiliwa huko ...,nadhani ni bora kingunge angesoma kwa makini..kwani muda sio mrefu ataaza yeye na kamati yake kuandaa ilani ya chama ya 2010-2015.
   
Loading...