Nape Nnauye kama January Makamba, maji ya shingo yamfika. Amuangukia Rais Magufuli baada ya kumnanga

Hii inaonyesha wewe jinsi gani unavyo penda mabifu mifarakano na utengano. Huwezi jenga taifa kama hamuwlwani
Hii inaonesha Tanzania tuna watu wa wanamna gani! Jinsi gani watu walivyo vigeugeu wasiyo jua wanacho simamamia na hao ndiyo viongozi wetu, dah! Nawaonea huruma sana mnao panga foleni kwenda kuwachagua hao wanao itwa viongozi.
 
Hiyo staili ya kutembezwa umbali mrefu pale mjengoni inaitwa babu seya.
Hufanyiwa wale wote ambao huenda kusema asante kwa wema ulionitendea mimi nisiye stahili au samahani sana kwa kukukwaza bwana mkubwa, mimi lofa.
Hiyo staili hakuna muwekezaji wa matrilioni anaweza fanyiwa hata iweje.
 
Kweli maendeleo hayana chama ila yana kisasi dogo ameogopa kama alimtuma Mke Wa mwenye heri Nyerere hakuambulia kitu
 
Hiyo staili ya kutembezwa umbali mrefu pale mjengoni inaitwa babu seya.
Hufanyiwa wale wote ambao huenda kusema asante kwa wema ulionitendea mimi nisiye stahili au samahani sana kwa kukukwaza bwana mkubwa, mimi lofa.
Hiyo staili hakuna muwekezaji wa matrilioni anaweza fanyiwa hata iweje.

Kufa na tililioni zako.... who gives a fwaa
 
Sinema hii ila Director wake ni BOMU. Eti Nape kaenda kuomba samahani na kuna mtu alikuwa anamrekodi 😂😂😂😂😂😂🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Nimeona Nape anatembea umbali mrefu sana ndani ya maeneo ya Ikulu.

Alishushiwa nje ya geti kuu la kuingia ikulu ?

Niliona mpaka anajifuta jasho kwa kutembea umbali mrefu.

Nimeona kama ametembea umbali mrefu sana.

Haaminiki ?
View attachment 1203928
 


Mbunge wa Mtama Nape Nnauye amefika Ikulu jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kuomba msamaha. Ameomba msamaha na kusamehewa kosa aliliofanya miezi michache iliyopita.


Akizungumza akiwa nje ya Ikulu baada ya kuzungumza na Rais Magufuli, Nape Nnauye amesema "Kwanza nimekuja kumuona baba yangu lakini Mwenyekiti wa Chama changu, Rais wangu kwasababu wote mnajua mambo yaliyopita au kutokea hapo katikati na mimi kama mtoto wa CCM, kama mwanae, nimeona ni vizuri nije niongee na Baba yangu.

Nashukuru kwamba amenipa fursa ya kuja kumuona na ameniambia amenisamehe na amenipa ushauri na kwakweli kwa dhati ya moyo wangu nishukuru sana amenipa fursa kubwa sana."



Mbunge Nape anaendelea kusema "Kwa kweli Muheshimiwa Rais kama Baba yangu, kama mzazi wangu nashukuru sana kwa fursa uliyonipa kwa kunisikiliza, kwa kunisamehe, kunishauri, kunielekeza nifanye nini huko mbele ninapokenda."

Rais Magufuli amesma "Mimi nimeshamsamehe kwa dhati Nape, amekuwa akiandika 'message' nyingi sana za kuomba msamaha hata saa nane za usiku nimemuona huyu mtu akiomba msamaha'"

"Leo ameniomba hapa aje anione na kabla, amejaribu sana, ameenda kwa Mzee Mangula amefika hadi kwa Mzee Opson na Mama Nyerere, amehangaika kweli. Na kwamba sisi tumeumbwa kusamehe, na wewe umemuona asubuhi amekuja hapa nikasema siwezi kumzuia kumuona ngoja nimuone kwanza japo nilikuwa na kikao kingine na kikubwa"
ameongeza Rais Magufuli

"Anachozungumza ni kwamba naomba Baba unisamehe, najua kusamehe kunaumiza lakini nasema kwa dhati kabisa nimemsamehe kabisa na anaeleza yaliyokuwa yanamsibu na baadhi ya watu waliokuwa wanamrubuni. Wengine wapo kwenye chama lakini nasema yote tumesamehe kwa sababu bado ni kijana mdogo na ana 'future' nzuri kwenye maisha yake."

"Nikiendelea kumshikilia kwenye moyo wangu, kwanza ni dhambi kubwa kwa mwenyezi Mungu na imeandikwa tusamehe saba mara sabini na Mungu amtangulie katika shughuli zake, akalee mke wake na familia yake, akakitumikie chama na akawatumikie wananchi wa jimbo lake."
Amemalizia Rais Magufuli

Wakimalizia katika maongezi yao nje ya Ikulu, Rais Magufuli alimuuliza Nape "Kwa hiyo ulikuwa huna amani?"

Nape: Sana

Rais Magufuli: Uwe na amani na Mungu akusaidie

Pia soma;
 
hahaa, Magufuli kasema Nape alimtafuta sana, alimtumia watu kibao kuanzia akina Mangula hadi mke wa Nyerere, kutuma msg usiku wa saa nane ila akawa kimya tu
Na tusi kubwa lilikua "Mshamba" limemgharimu yote hayo..

Bado Watu mpaka leo wanashindwa kung'amua aliyeamuru kushambuliwa Lissu.

Mungu aliyeumba Dunia na vyote vilivyomo kumuomba Msamaha ni bure tena huhitaji wapambe na vyombo vya habari.
 
Back
Top Bottom