Nape Nnauye kama January Makamba, maji ya shingo yamfika. Amuangukia Rais Magufuli baada ya kumnanga

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,745
11,865
Mbunge wa Mtama Nape Nnauye amefika Ikulu jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kuomba msamaha. Ameomba msamaha na kusamehewa kosa aliliofanya miezi michache iliyopita.

001E4C28-8E4D-43A7-A628-E2B7C136BB7D.jpeg



Akizungumza akiwa nje ya Ikulu baada ya kuzungumza na Rais Magufuli, Nape Nnauye amesema "Kwanza nimekuja kumuona baba yangu lakini Mwenyekiti wa Chama changu, Rais wangu kwasababu wote mnajua mambo yaliyopita au kutokea hapo katikati na mimi kama mtoto wa CCM, kama mwanae, nimeona ni vizuri nije niongee na Baba yangu.

Nashukuru kwamba amenipa fursa ya kuja kumuona na ameniambia amenisamehe na amenipa ushauri na kwakweli kwa dhati ya moyo wangu nishukuru sana amenipa fursa kubwa sana."


EEGcGKqW4AA2PfC.jpg

Mbunge Nape anaendelea kusema "Kwa kweli Muheshimiwa Rais kama Baba yangu, kama mzazi wangu nashukuru sana kwa fursa uliyonipa kwa kunisikiliza, kwa kunisamehe, kunishauri, kunielekeza nifanye nini huko mbele ninapokenda."

Rais Magufuli amesma "Mimi nimeshamsamehe kwa dhati Nape, amekuwa akiandika 'message' nyingi sana za kuomba msamaha hata saa nane za usiku nimemuona huyu mtu akiomba msamaha'"

"Leo ameniomba hapa aje anione na kabla, amejaribu sana, ameenda kwa Mzee Mangula amefika hadi kwa Mzee Opson na Mama Nyerere, amehangaika kweli. Na kwamba sisi tumeumbwa kusamehe, na wewe umemuona asubuhi amekuja hapa nikasema siwezi kumzuia kumuona ngoja nimuone kwanza japo nilikuwa na kikao kingine na kikubwa"
ameongeza Rais Magufuli

"Anachozungumza ni kwamba naomba Baba unisamehe, najua kusamehe kunaumiza lakini nasema kwa dhati kabisa nimemsamehe kabisa na anaeleza yaliyokuwa yanamsibu na baadhi ya watu waliokuwa wanamrubuni. Wengine wapo kwenye chama lakini nasema yote tumesamehe kwa sababu bado ni kijana mdogo na ana 'future' nzuri kwenye maisha yake."

"Nikiendelea kumshikilia kwenye moyo wangu, kwanza ni dhambi kubwa kwa mwenyezi Mungu na imeandikwa tusamehe saba mara sabini na Mungu amtangulie katika shughuli zake, akalee mke wake na familia yake, akakitumikie chama na akawatumikie wananchi wa jimbo lake."
Amemalizia Rais Magufuli

EEGZnBJXYAAHVTA.jpg

Wakimalizia katika maongezi yao nje ya Ikulu, Rais Magufuli alimuuliza Nape "Kwa hiyo ulikuwa huna amani?"

Nape: Sana

Rais Magufuli: Uwe na amani na Mungu akusaidie

Pia soma;
 
Magu anamuhitaji Nape kwasababu anahitaji kura za watu wa kusini, na Nape nae anamuhitaji Magu ili ajiweke katika nafasi nzuri ya jina lake kupita kama mgombea 2020.

In short,kila mtu hapo anamuhitaji mwingine kuelekea 2020.

Ni kweli tunajua CCM hawategemei sanduku la kura kushinda, ila ni ukweli pia wangependa zaidi washinde kupitia sanduku la kura.
 
Magu anamuhitaji Nape kwasababu anahitaji kura za watu wa kusini.
Hee hee. Mnaanza kuhamisha magoli sasa. Hata aibu hamna. Mimi nilishawambia huu mtindo wa upinzani wa kushabikia mtu yeyote anayempinga rais Magufuli utazidi kuwaporomosha. Hawakujifunza kwa kina Lowassa, Wema na wengineo wengi? Chadema wataishia kutumika kama choo tu. Subirini na Nyalandu ni muda tu atawatoroka.
 
28 Reactions
Reply
Back
Top Bottom