Nape Nnauye kama January Makamba, maji ya shingo yamfika. Amuangukia Rais Magufuli baada ya kumnanga

Roving Journalist

Roving Journalist

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2017
Messages
266
Points
1,000
Roving Journalist

Roving Journalist

JF-Expert Member
Joined Apr 18, 2017
266 1,000
Mbunge wa Mtama Nape Nnauye amefika Ikulu jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kuomba msamaha. Ameomba msamaha na kusamehewa kosa aliliofanya miezi michache iliyopita.

001e4c28-8e4d-43a7-a628-e2b7c136bb7d-jpeg.1204116Akizungumza akiwa nje ya Ikulu baada ya kuzungumza na Rais Magufuli, Nape Nnauye amesema "Kwanza nimekuja kumuona baba yangu lakini Mwenyekiti wa Chama changu, Rais wangu kwasababu wote mnajua mambo yaliyopita au kutokea hapo katikati na mimi kama mtoto wa CCM, kama mwanae, nimeona ni vizuri nije niongee na Baba yangu.

Nashukuru kwamba amenipa fursa ya kuja kumuona na ameniambia amenisamehe na amenipa ushauri na kwakweli kwa dhati ya moyo wangu nishukuru sana amenipa fursa kubwa sana."


eegcgkqw4aa2pfc-jpg.1203639

Mbunge Nape anaendelea kusema "Kwa kweli Muheshimiwa Rais kama Baba yangu, kama mzazi wangu nashukuru sana kwa fursa uliyonipa kwa kunisikiliza, kwa kunisamehe, kunishauri, kunielekeza nifanye nini huko mbele ninapokenda."

Rais Magufuli amesma "Mimi nimeshamsamehe kwa dhati Nape, amekuwa akiandika 'message' nyingi sana za kuomba msamaha hata saa nane za usiku nimemuona huyu mtu akiomba msamaha'"

"Leo ameniomba hapa aje anione na kabla, amejaribu sana, ameenda kwa Mzee Mangula amefika hadi kwa Mzee Opson na Mama Nyerere, amehangaika kweli. Na kwamba sisi tumeumbwa kusamehe, na wewe umemuona asubuhi amekuja hapa nikasema siwezi kumzuia kumuona ngoja nimuone kwanza japo nilikuwa na kikao kingine na kikubwa"
ameongeza Rais Magufuli

"Anachozungumza ni kwamba naomba Baba unisamehe, najua kusamehe kunaumiza lakini nasema kwa dhati kabisa nimemsamehe kabisa na anaeleza yaliyokuwa yanamsibu na baadhi ya watu waliokuwa wanamrubuni. Wengine wapo kwenye chama lakini nasema yote tumesamehe kwa sababu bado ni kijana mdogo na ana 'future' nzuri kwenye maisha yake."

"Nikiendelea kumshikilia kwenye moyo wangu, kwanza ni dhambi kubwa kwa mwenyezi Mungu na imeandikwa tusamehe saba mara sabini na Mungu amtangulie katika shughuli zake, akalee mke wake na familia yake, akakitumikie chama na akawatumikie wananchi wa jimbo lake."
Amemalizia Rais Magufuli

eegznbjxyaahvta-jpg.1203618

Wakimalizia katika maongezi yao nje ya Ikulu, Rais Magufuli alimuuliza Nape "Kwa hiyo ulikuwa huna amani?"

Nape: Sana

Rais Magufuli: Uwe na amani na Mungu akusaidie

Pia soma;
 
Iringa Native

Iringa Native

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2011
Messages
936
Points
1,000
Iringa Native

Iringa Native

JF-Expert Member
Joined Nov 9, 2011
936 1,000
Naona uwanja wa vita umekuwa mgumu kiasi kwamba Battalion Commander anaanza kuludisha Comrades aliowastaafisha kwa kusema kuwa wamezeeka, hawana msaada nk!,aliwastaafisha na majukumu yao akawapa watoto aliodhani watamfaa sasa uwanja umekuwa mgumu imebidi aludishe wanaojua vita lakin ili kuficha ukweli anatuambia kuwa comrades ndio wanaomba kuludi........
 
TUTUO

TUTUO

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Messages
2,904
Points
2,000
TUTUO

TUTUO

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2013
2,904 2,000
Mkuu utachoma mafuta kwenda kuomba msamaha kwa mtu bila kumtendea kosa?
Wamejidhihirisha wazi kuwa sauti za kashifa zilizozagaa mitandaoni ni za kwao.
Mpaka sasa lile ni kosa la jinai kumfanyie vile Rais wetu nashangaa DPP yupo kimya na wote sauti tulizisikia
 
R

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Messages
19,014
Points
2,000
R

Retired

JF-Expert Member
Joined Jul 22, 2016
19,014 2,000
Kweli shetani lucifa hufurahia mafanikio ya muda mfupi,

Lucifa alipowatumia wayahudi kumuua Yesu alifurahi sana,

kimbembe ni pale Yesu kufa na kwenda kuzimu akamyanganya funguo lucifa, Siku ya tatu akapaa mbinguni, furaha ya Lucifer ilikoma ikabaki majuto, alinyongonyea mpaka kesho
Amen, ubarikiwe kwa neno zuri
 
K

Katavi yetu

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2018
Messages
404
Points
500
K

Katavi yetu

JF-Expert Member
Joined Jul 30, 2018
404 500
Upinzani waige kusameheana laiti kama upinzani kusingekua na kufukuzana kwenye chama upinzani ungekua imara zaidi but mtu akikosea kidogo tu basi anatimuliwa uanachama matokeo yake kuzigawa kura za watanzania
 
Mother Confessor

Mother Confessor

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2016
Messages
16,724
Points
2,000
Mother Confessor

Mother Confessor

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2016
16,724 2,000
Shikamooni wake wa Wanasiasa wote!!
Mie roho yangu naijua mwenyewe; kifua cha kustahimili mume wangu akifanya mambo kama haya sina😒😒
Hahaha,.fedheha haistahimiliki kirahisi jomoniii chaa!!!
 
R

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Messages
19,014
Points
2,000
R

Retired

JF-Expert Member
Joined Jul 22, 2016
19,014 2,000
Muulize Nape mwenyewe alifanya makosa gani hadi kwenda kuungama kwa Mheshimiwa Rais.
Ni njaa, lkn nafsi ya ndani inajua haikutenda kosa lolote!
 
mng'ato

mng'ato

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2014
Messages
16,682
Points
2,000
mng'ato

mng'ato

JF-Expert Member
Joined Oct 27, 2014
16,682 2,000
Hivi nape hajawai kukana zile voice notes kweli....au kumbukumbuka zangu zinaenda harijojo???
Aliulizwa kule azam tv hio sauti ni ya kwako akaanza kujibu majibu yasiyoeleweka'ooh kimsingi hili suala lina ujinai ndani yake sijui nini',inshort hakueleweka alichokua anakisema.
 
ngozimbili

ngozimbili

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2011
Messages
1,215
Points
2,000
ngozimbili

ngozimbili

JF-Expert Member
Joined Jul 28, 2011
1,215 2,000
Huyu baba anapenda kudhalilisha watu,kwanza makamera ya nini na mtu keshaomba msamaha,mpaka umtangaze duh wanasiasa wana kazi
 
U

udagadagaa

Senior Member
Joined
Nov 21, 2013
Messages
107
Points
225
U

udagadagaa

Senior Member
Joined Nov 21, 2013
107 225
kafanya la maana mtaani kugumu nyie oooh na walivyozoea Maisha ya Raha
 

Forum statistics

Threads 1,336,688
Members 512,697
Posts 32,547,673
Top