idawa
JF-Expert Member
- Jan 20, 2012
- 25,284
- 38,312
Karibu tuwafutulie hawa wanasiasa vijana na Mwandishi mkongwe juu ya mstakabali wa siasa za Tanzania.
Nappe..
Akizungumzia kuhusu hama hama ya viongozi kwenye vyama amesema yeye sio muumini wa kuhama hama vyama .
Anasema kuna haja hii hama hama iangaliwe upya isiwe kirahisi rahisi.
Nappe anasema yeye hawezi kuhama chama eti kwa sababu ametofautiana na mkubwa fulani.
Nappe anasema kuna haja ya kuchora mstari kutenganisha Taasisi ya Urais na Uenyekiti wa Chama kwa sababu limekuwa likileta migongano mara kwa mara kwenye utendaji wa kazi.
Nappe anasema kuhama hama vyama hakuna tija yoyote kwa Taifa.
Mtatiro.....Bado analaani serikali kuzuia shughuli za kisiasa..anasema jambo ambalo lipo kikatiba hakuna wa kulipinga hata Rais aweje...
Kuhusu hama hama Mtatiro anasema hawezi kuhama CUF kwa sababu ya Lipumba sababu yeye hakujiunga kumfuata mtu.
Akizungumzia wabunge wanaohama anasema wengi ni wale wanaopewa rushwa ama kununuliwa.
Anasema serikali ya Magufuli huko nje inasifiwa kwa kupambana na rushwa Lakini ndani ya nchi hali ni tofauti....na mbaya zaidi serikali hii inachagua wa rushwa za kushughulika nazo....
Mtatiro...anasema upinzani lazima ujenge vijana wake na sio kutegemea wanasiasa wanaohama vyama..
Anasema ni kosa vyama vya upinzani kuwapokea wanachama wa vyama vingine na kuwapa nafasi za juu bila kuwachunguza.
Matokeo yake ndio hao wanaohama hama .
Nappe...anasema ili vyama vya upinzani viwe imara ni lazima wawekeze kwa vijana.
Anasema yeye ni mfano ccm imewekeza toka akiwa mdogo amekulia kwenye itikadi ya chama.
Hiyo hawezi kuhama kwa haya mawimbi madogo madogo yanayomtokea..
Dr.Shoo anahoji wabunge wanaohama vyama na kuacha mamilioni ya ubunge je ni kwa mapenzi yao binafsi.
Anahoji ccm kama kweli wanaowanunua hao watu wanafaidika nini kwa maslahi ya nani.
Anasema chama chochote hakiwezi kushika dola kama hakijawekeza kwenye mashina...
Upinzani lazima uwekeze mashinani kuliko ndio iliko dola.