Nape Nnauye: Fichueni uozo wa serikali ya Rais Magufuli

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametaka magazeti ya Serikali kumsaidia Rais John Magufuli, kutumbua majipu kwa kuibua uozo serikalini.

Akizungumza katika kikao cha wafanyakazi wa Kampuni ya Tanzania Standard (Newspapers) Ltd Dar es Salaam jana, inayochapisha magazeti ya Daily News, HabariLeo na Spotileo, Nape ametaka magazeti hayo yasimung’unye maneno kwa kuandika ukweli; kwenye nyeusi yaandike nyeusi na kwenye nyeupe, yaandike nyeupe.

Alisema vyombo vya habari vya Serikali vina wajibu wa kumsaidia Rais kutumbua majipu kwa kuandika habari bila woga, upendeleo wala kuomuonea mtu, ili kama kuna dosari ziko mahali ziibuliwe kwa lengo la kupata suluhu.

“Unajua vyombo vya habari vinaaminika na vinasomwa na wengi na hasa wananchi wanapotaka ukweli wa jambo, wanaangalia kama limeandikwa, sasa kama jambo litaandikwa kwa kufichwa fichwa haitaisaidia Serikali, kama ni nyeusi sema nyeusi, kama ni nyeupe sema nyeupe na hiyo ndiyo suluhu,” alisisitiza Nape.

Alisema majipu yanayoendelea kutumbuliwa na Rais, mengine yanaibuliwa na vyombo vya habari na ili kumsaidia na kusaidia Taifa, vyombo vya habari vya Serikali lazima viibue hayo, pia viaminiwe mpaka na watumishi wa Serikali, wavitumie kuibua uozo.

Nape alisisitiza kwamba kuficha ukweli kwenye jambo ovu, ni kuendelea kuharibu hivyo kuibuliwa kwa maovu kutaisaidia Serikali na watendaji wake kuchukua hatua madhubuti. “Kuna hili jambo la baadhi ya watendaji kusema mfumo hautaki hili, hakuna cha mfumo ni maneno yao wanayatumia kama kichaka cha kufanya uchafu,” alisema Nape.

Nape alitoa onyo kwa watendaji wa serikali kuacha tabia ya kuzuia habari zisitoke kwa maslahi yao na kutaka wenye pingamizi ya kutoka kwa habari, wawasiliane naye na si kuingilia chombo cha habari.

Katika taarifa ya wafanyakazi wa TSN kwa Waziri huyo, walimuomba kuangalia changamoto zilizopo ikiwa ni pamoja na maslahi duni, uhaba wa vitendea kazi na baadhi ya viongozi kufanya uamuzi kwa kukiuka sheria na utaratibu.

Akijibu hoja kuhusu Muundo wa Utumishi wa kampuni hiyo, ambao umelalamikiwa na wafanyakazi kuwa umepitwa na wakati na umekuwa na malalamiko mengi ya upendeleo, Nape alitoa mwezi mmoja kwa Menejimenti ya TSN, kulifanyia kazi na kulimaliza.

“Sipendi kufukuza watu kazi, ila inapobidi itafanyika, natoa mwezi mmoja menejimenti na mtu wa utumishi kaeni, pitieni muundo huo... kwanza umeisha muda wake uletwe mpya na wafanyakazi walipwe malimbikizo ya nyongeza ya mishahara kwa muda wote ambao hawajaongezwa,” alisisitiza Nape.

Chanzo: Habarileo
 
Kwa mtu asiyefahamu anaweza akadhani kuna Nape Nnauye wawili!

Mmoja ni yule Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa.

Mwingine ni huyu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Unaweza ukadhani Nape wa utawala wa Rais Kikwete siyo huyu wa utawala wa Rais Magufuli!

Nape is a master at the game of politics!
 
Wakiibua wanafungiwa
Msingi wa uandishi wa habari ni ethics based on professional conduct, morality and the truth. Kinyume chake inakuwa ni misrepresenting or misleading.

Misrepresenting or misleading inaweza kusababisha taharuki au maafa katika taifa.
 
Tatizo la kwanza ni Nape mwenyewe, tumeona katika kipindi kigupi cha uwaziri wake akilifungia gazeti ambalo liliweka wazi ukweli, sasa anasema nyeupe iitwe nyeupe na nyeusi iitwe nyeusi. Huyo ni Nape,
Tumeona akiwanyima Watanzania haki ya habari, hakuna kuonyesha bunge, huyo ni Nape. Yaani ameshasahau ya. juzi. Anadhani nasi tumesahau.....
 
"Did Nape Say what he mean and did he mean what he Say" Propaganda za kusimamia misingi tofauti na unayoiongea ni siasa za zamani...hapo anataka watajwe wengine wakitajwa wao mawaziri atakuja juu na kufukuza hao waandishi.
embu mwandishi mmoja atuchunguzie zile nyumba za serikali zilizosemekana kuuzwa bei chee na waliouziwa.
 
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametaka magazeti ya Serikali kumsaidia Rais John Magufuli, kutumbua majipu kwa kuibua uozo serikalini.

Akizungumza katika kikao cha wafanyakazi wa Kampuni ya Tanzania Standard (Newspapers) Ltd Dar es Salaam jana, inayochapisha magazeti ya Daily News, HabariLeo na Spotileo, Nape ametaka magazeti hayo yasimung’unye maneno kwa kuandika ukweli; kwenye nyeusi yaandike nyeusi na kwenye nyeupe, yaandike nyeupe.

Alisema vyombo vya habari vya Serikali vina wajibu wa kumsaidia Rais kutumbua majipu kwa kuandika habari bila woga, upendeleo wala kuomuonea mtu, ili kama kuna dosari ziko mahali ziibuliwe kwa lengo la kupata suluhu.

“Unajua vyombo vya habari vinaaminika na vinasomwa na wengi na hasa wananchi wanapotaka ukweli wa jambo, wanaangalia kama limeandikwa, sasa kama jambo litaandikwa kwa kufichwa fichwa haitaisaidia Serikali, kama ni nyeusi sema nyeusi, kama ni nyeupe sema nyeupe na hiyo ndiyo suluhu,” alisisitiza Nape.

Alisema majipu yanayoendelea kutumbuliwa na Rais, mengine yanaibuliwa na vyombo vya habari na ili kumsaidia na kusaidia Taifa, vyombo vya habari vya Serikali lazima viibue hayo, pia viaminiwe mpaka na watumishi wa Serikali, wavitumie kuibua uozo.

Nape alisisitiza kwamba kuficha ukweli kwenye jambo ovu, ni kuendelea kuharibu hivyo kuibuliwa kwa maovu kutaisaidia Serikali na watendaji wake kuchukua hatua madhubuti. “Kuna hili jambo la baadhi ya watendaji kusema mfumo hautaki hili, hakuna cha mfumo ni maneno yao wanayatumia kama kichaka cha kufanya uchafu,” alisema Nape.

Nape alitoa onyo kwa watendaji wa serikali kuacha tabia ya kuzuia habari zisitoke kwa maslahi yao na kutaka wenye pingamizi ya kutoka kwa habari, wawasiliane naye na si kuingilia chombo cha habari.

Katika taarifa ya wafanyakazi wa TSN kwa Waziri huyo, walimuomba kuangalia changamoto zilizopo ikiwa ni pamoja na maslahi duni, uhaba wa vitendea kazi na baadhi ya viongozi kufanya uamuzi kwa kukiuka sheria na utaratibu.

Akijibu hoja kuhusu Muundo wa Utumishi wa kampuni hiyo, ambao umelalamikiwa na wafanyakazi kuwa umepitwa na wakati na umekuwa na malalamiko mengi ya upendeleo, Nape alitoa mwezi mmoja kwa Menejimenti ya TSN, kulifanyia kazi na kulimaliza.

“Sipendi kufukuza watu kazi, ila inapobidi itafanyika, natoa mwezi mmoja menejimenti na mtu wa utumishi kaeni, pitieni muundo huo... kwanza umeisha muda wake uletwe mpya na wafanyakazi walipwe malimbikizo ya nyongeza ya mishahara kwa muda wote ambao hawajaongezwa,” alisisitiza Nape.

Chanzo: Habarileo
Jamani nyie waandishi wa habari,nape anasema mfichue uozo sasa hebu fichueni uozo pale kwenye gazeti la uhuru wafanyakazi hawalipwi mshahara,gazeti haliba mhariri mkuu
 
Lakini Nape yuko smart sana, maana anajua hayo magazeti hayana wasomaji, hivyo hata yaandike nini hizo habari zitaishia kufungia vitumbuatu hahahaaa.
Hebu awaruhusu Mwananchi, Tanzania Daima, Mtanzania, Mwanahalisi...... Aone moto wa gas!!!!! Kama kesho yake hajayafungia yote. Nape acha unafiki
 
Back
Top Bottom