Nape Nnauye CCM ina rasilimali zenye thamani zaidi ya sh. bil 50 yajipanga kutotegemea ruzuku | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape Nnauye CCM ina rasilimali zenye thamani zaidi ya sh. bil 50 yajipanga kutotegemea ruzuku

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 26, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na Irene Mark

  KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amesema chama hicho kimejipanga kutumia rasilimali zake zenye thamani ya zaidi ya sh bilioni 50 kujiimarisha kiuchumi ili kupunguza utegemezi wa ruzuku.

  Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi ndogo za chama hicho jijini Dar es Salaam jana, Nape alisema wamewaalika wafanyabiashara 30 wa Chama cha African National Congress (ANC) cha Afrika Kusini, ili kujifunza namna ya kutumia vema rasilimali za CCM.

  Alisema ujio wa wafanyabiashara hao wa ANC ni sehemu ya mageuzi ndani ya chama chao na kwamba wataingia nchini leo kwa ziara ya siku tano ambapo watashiriki kongamano la kibiashara lililoandaliwa na Tanzania Chamber of Commerce, Industries and Agriculture (TCCIA).


  "Itakumbukwa kuwa katika maamuzi ya kufanya mageuzi ndani ya chama yanayoendelea, Chama Cha Mapinduzi kiliamua kuongeza juhudi katika kukifanya chama kipunguze au kumaliza kabisa utegemezi wa ruzuku katika kuendesha mambo yake.


  "Hivyo basi, ziara hii ni sehemu ya utekelezaji wa maamuzi hayo… lengo ni kujipanua kiuchumi na kujifunza namna bora ya kuwekeza hasa tukizingatia kuwa ANC ni chama kikongwe kwenye siasa barani Afrika hivyo wenzetu wana uzoefu zaidi.


  "Wakati wenzetu wanachangishana kuendesha vyama vyao sisi tutawekeza," alisisitiza Nape na kuongeza kwamba watatumia vema makampuni yanayomilikiwa na CCM.


  Alibainisha kuwa malengo ya ziara hiyo ni kutafuta fursa mbalimbali za uwekezaji zitakazodumisha na kuendeleza uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya ANC na CCM ikiwemo kubadilishana uzoefu wa makampuni ya vyama hivyo.


  Alisema wafanyabiashara hao watatembelea kambi za Mazimbu mkoani Morogoro zilizotumika kuandaa wapigania uhuru wa ANC wakati wa harakati za ukombozi wa nchi yao.


  Alisema wataalamu mbalimbali wa CCM na jumuiya zake watashiriki kwenye ziara hiyo ili kujifunza na kupata uzoefu katika uanzishaji, usimamizi na uendeshaji wa vitega uchumi vya chama.


   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Rasilimali nyingi zilikuwa za Wananchi wa Tanganyika na Zanzibar; kwanini wasirudishiwe?
   
 3. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,338
  Trophy Points: 280
  Wezi tu hao ccm ipo siku tuzirudisha mikononi mwa umma hizo wanazodai kuwa ni rasilimali zao. Wanadai wana rasilimali bila hata aibu. Haya majizi haya...
   
 4. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,771
  Trophy Points: 280
  Baba unamwita jirani aje kukufundisha namna ya kupanga bajeti ya familia yako.
  Nape kakosa cha kuongea, Cha msingi ni hii issue ya M4C inawanyima raha wezi wa rasilimali za Tanzania.
   
 5. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  "Wakati wenzetu wanachangishana kuendesha vyama vyao sisi tutawekeza,"

  Wenzenu ndio akina nani?mbona wenzenu hasa kwa maana ya neno hilo ni CUF?Au unamaanisha CHADEMA?Kama ndivyo,kwani na nyinyi mnayo haja kweli ya kuchangiwa na wananchi?Kama hatufanani itikadi,kwa nini basi iwe lazima kuwa na mikakati inayofanana?
  kwani si mmekuwa mnasifika kwa kugawa pesa,pilau,chumvi...au mnadhani kile ambacho mmekuwa mnagawa hakiwaridhishi wapokeaji?
  Iweje mmekuwa mnadai kuna umuhimu wa kutenganisha siasa na biashara, halafu leo chama cha siasa, CCM ,kinatarajia kujihusisha na masuala ya biashara (kuwekeza)?Halafu inawezekanaje ufanye biashara bila kumnyonya mtu?
  Mpango huu ni kinyume kabisa na nadharia za Karl Max ambazo Kambarage alizitumia kuijenga TANU na baadaye CCM!!Alimradi mkanganyiko mtupu!!!
   
 6. T

  Topical JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  CCM warudishe viwanja vyote kwa wananchi kwanza..ikifutiwa na ofisi zilizojengwa kwa pesa za umma
   
 7. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,771
  Trophy Points: 280

  Hata baada ya nyie kuolewa na CCM hapo Zenji bado tu hamjanufaika na rasilimali hizi????
  Au ndo mke hajui password ya ATM card ya mumewe???
   
 8. T

  Topical JF-Expert Member

  #8
  Mar 26, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Sishange adui wenu ni CUF na siyo CCM..hapo ndio utajua ...nani ameolewa..
   
 9. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #9
  Mar 26, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Rasilimali za CCM? Walizopora au walizokwiba? Kuna kitu kwenye chama hiki kinawafanya wanachama wake wakose umakini kwa yale wanayoyatamka na wanayoyatenda, sijui ni laana gani hii! Ni kama nyang'au kusimamia rasilimali za mfugaji wa kondoo na mbuzi!  Nape: Kikao kijacho CCM kuja na maamuzi mazito.​
  Ni baada ya tambo hizi, RA akampiga marufuku Nape kukanyaga Igunga na leo hii EL hataki hata kuona sura yake Arumeru na Sioi aliyesemekana alipitishwa kwa rushwa ndiye anaipeperusha bendera ya CCM Arumeru. Wakati walafi kama Ole Sendeka wanalamba matapishi yao, masikini mnafiki Nape eti bado anasubiri kikao kijacho cha CCM kichukue maamuzi magumu!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #10
  Mar 26, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  afadhali kodi zetu zitumike kwa maendeleo yetu
   
 11. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #11
  Mar 26, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Wewe vipi, aliyeolewa si yuko kwa mumewe?
   
 12. I

  IWILL JF-Expert Member

  #12
  Mar 26, 2012
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 311
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  50 billions is not news! gaddafi alikuwa na pipes za mafuta na gdp za billions, lakini wapi alipo....CCM assets my foot! hayo majengo anayosema ni assets afikirie upya. it took few tnt to bring down na assets will be less than 50m. tutaifanya nchi mpya safari yetu ya nchi ya ahadi bado inaendelea. this is not the country we promised we will get there.
   
 13. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #13
  Mar 26, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hata mngekuwa na over 100bl kwa mtaji huu wa kugawa fedha ovyo ovyo haitoshi kabisa.

  Lingine CCM haina la kujivunia kwa sababu imenufaika sana na mfumo wa chama kimoja.
   
 14. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #14
  Mar 26, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hatutaharibu majengo yetu mkuu,hizo ni rasilimali za wananchi,zilipatikana kwa nguvu ya wananchi,c.c.m wasivyo na a**** wakajimilikisha wakiamini watatawala milele,rasilimali za zitarudi kwa wananchi mkuu,hii si nchi ya c.c.m bali ni Watanzania
   
 15. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #15
  Mar 26, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nape wanaokuja ni wafanyabiashara na siyo wanasiasa sasa nyie ccm mnafanyabiashara?huo ujio unaweza usiwe mtaji mzuri sana kama unavyotarajia.usizungumzie ruzuku tu zungumzia pia na pesa mnazochukuwa kwa wahindi na wafanyabiashara wakubwa na kuwapa vyeti.
  Tofautisheni ujio wa kisiasa na kibiashara
   
 16. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #16
  Mar 26, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kabla hawaja piga mahesabu ya mali zao ni bora wangerudisha mali zote walizozipora kwa watanzania kama viwanja, majengo na viwanja vya wazi na stendi ili hesabu zao zikae sawa kwani zitakapo rudishwa na utawala mwingine watajiona ni chama ambacho hakina assets nyingi kama wanavyofikiria.
   
 17. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #17
  Mar 26, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,913
  Likes Received: 213
  Trophy Points: 160
  Huyu anazungumzia rasilimali za Taifa ambazo CCM walijimilikisha wakati wa Chama Kimoja?
  Viwanja vya mpira, Jengo la Umoja wa vijana wa TANU, Baadhi ya majengo ya Serikali, Magari ya Serikali n.k
  Hata Ikulu ni mali ya CCM manake vikao vya Chama hufanyikia Ikulu siku hizi..

  Damn!!
   
 18. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #18
  Mar 26, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,936
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Hizo zote ni mali za wananchi. Mfano CCM Kirumba ni mchango wa wananchi, nakumbuka mimi nilichangia ujenzi wa Ali Hassan Mwinyi Tabora. Wakati nalazimishwa kuchangia sikuwa na chama, sasa kama mimi nimejiunga na chama cha siasa naomba nirudishiwe mchango huo ili niupeleke kwenye chamma changu pinzani. na njia nzuri ni kuzirudisha mali zote za CCM serikalini na kuendelea kutoa ruzuku kwa ajili ya kuendesha vyama vya siasa!!
   
 19. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #19
  Mar 26, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Inashangaza kwa kweli yaani chama cha kijamaa lakini kinafanya biashara za kuwanyonya wananchi? Ni bora watangaze tu kwamba ujamaa umekufa.
   
 20. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #20
  Mar 26, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,771
  Trophy Points: 280
  MOvement for Changes imewaogopesha CCM hadi Nape kaamua kutangaza kuwa CCM sio chama cha kijamaa bali ni chama cha kibepari.
  Serikali ya CCM imeshindwa kuendeleza viwanda na kuviua kwa kutumia sera ya ubinafsishaji, ni CCM hii tena inasema inaendeleza viwanda kwa manufaa ya chama???
  CCM is running away like headless chicken.
   
Loading...