Nape Nnauye: Bila upinzani imara hakuna CCM Imara

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,498
51,090
1. Bila upinzani imara hakuna CCM Imara
- Ewe mwanachama wa CCM bila ya kuwepo kwa CCM imara, wewe ni nothing, bure kabisa, huna thamani yoyote ndani ya chama, utakuwa na thamani gani wakati hawakuhitaji kukaa madarakani?. Kwa hiyo uwepo wa upinzani angalau ni sababu ya hawa walioshika madaraka kukupetipeti, kukupa poshoposho ndogo angalau na wewe ujisikie mtu. Fahamu kwamba Upinzani unakufanya upate thamani japo kidogo

2. Bila ya Upinzani imara, CCM itaongozwa na mtu mmoja, ila akiwa na soni kidogo itaongozwa na Politburo ya watu wachache sana wasiozidi kumi, Hii ndo itakuwa De facto serikali. Hawa watakuwa na wanachama wao wachache tu waliokwenye database, ikitokea event ya kutaka kuonekana kuna chama nyuma ya maamuzi yao, watawaita , kuwapa Tshirt na kuwapakiza kwenye makarandinga na kuwapa jukumu la kushangilia. Wewe mwanaCCM mwingine huna thamani, nchi itaongozwa na kikundi cha watu wachache, Chama kitageuka rubeber stamp.

3. Bila Upinzani Imara, CCM itageuka chama cha kinafiki zaidi, Sasa hivi kuna unafiki, lakini CCM ikibaki pekee, na kwa kuwa mwenyekiti wa Chama ndiye rais, tegemea Unafiki na kujipendekeza kupita kiasi, tegemea kuchongeana na kufitiniana zaidi, maana mfalme hashikiki, yeye ndiye CCM na CCM ndiyo, mtathubutuje kumgusa?

4. CCM inajidanganya kutaka kuwa kama chama cha Kikomunisti cha China. Chama cha Kikomunisti cha China mtu hawi mwanachama mpaka awe na potential fulani, ya kielimu, ya kipaji, ya mchango fulani katika jamii!, CCM wao wanachukua kila kokoro.
Chama cha Kikomunisti kina ajenda na kinaisimamia, kwa mfano ajenda yao ya sasa ni kuifanya China kuwa powerhouse ya sayansi na tekinolojia. CCM ya leo mara waje na kilimo kwanza, mara viwanda, ilani inasema tutaendeleza mchakato wa katiba, lakini aliyebeba ilani anasema katiba si kipaumbele chake ilmradi vuruguvurugu!. Bila ya kuwepo upinzani wa kuwastuastua hiki chama kitavimbiwa zaidi na kuiharibu nchi

Kwa hiyo mimi nakuunga mkono bwana Nape, umeongea ukweli mtupu.
Nyerere aliyetawala chini ya chama kimoja kwa zaidi ya miaka 20 aliliona hili, aliona kuwa bila ya kuwepo upinzani imara CCM ni mzigo mkubwa sana kwa Taifa. Nawashauri wana CCM kataeni juhudi za Mwenyekiti wenu kuupiga vita Upinzaniz akifanikiwa kuushinda basi nanyi huko hamko shwari, atageukia upinzani ndani ya chama chenu ili ajihakikishie total obedience. Na klikishafika hatua hiyo thamani yenu siyo hoja tena ndani ya chama, bali umahiri katika kukata mauno kucheza Sebene la kumsifu Mwenyekiti, Umahiri katika kutoa kauli mwanana za kumsifu mwenyekiti.
 
Aliyeua upinzani "bao la mkono" leo anaimbiwa mapambio na majani ya migomba na cherekoz
Nape endelea kuwaimbia blues ... wanaanza kucheza romantically:D:D
 
Aliyeua upinzani "bao la mkono" leo anaimbiwa mapambio na majani ya migomba na cherekoz
Nape endelea kuwaimbia blues ... wanaanza kucheza romantically:D:D
Hata kama alitukosea lakini joka kuu nduli idd amin limeingia ndani lazima tushirikiane kulitoa
 
Hata Nyerere mwaka 1965 alitukosea sana kutuondelea vyama vingi, lakini alipoona kosa na kulirekebisha mwaka 1992 sisi tunamshukuru kwa hilo
 
Hata Nyerere mwaka 1965 alitukosea sana kutuondelea vyama vingi, lakini alipoona kosa na kulirekebisha mwaka 1992 sisi tunamshukuru kwa hilo
 
Baada ya kuona amepoteza thamani ndani ya CCM saa anaona umuhimu wa wapinzani, Huyo jamaa ni faa kweli, atulie tu ni zamu ya wengine.
 
Back
Top Bottom