VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Alipotangazwa kuwa ni Waziri, nilipatwa na kizunguzungu. Nikameza hata tembe kadhaa za vidonge kwakuwa sikuwa vizuri. Nilipatwa na hali hiyo kwakuwa Nape namjua. Namjua kuwa hana uwezo wowote wa kuwa Waziri. Nape ni mtu wa propaganda. Ni mtu wa kutaka sifa. Ni mtu wa kupenda kuongea aonekane na asikike. Ni wa kuropoka. Ni wa kupenda kubishana.
Ni wa kupenda kujadiliwa. Ni wa kupenda kujiona na kudandia hoja. Ni wa kuiba hoja za wengine na kuzifanya za kwake. Ni mwanasiasa anayewekwa mjini na maneno yake yasiyo na mbele wala nyuma. Nape ana sifa zote za kuwa mwanasiasa wa kichama na si kiserikali.
Ni kwakuwa Nape ni mwanasiasa anayeweza kuufanya uongo kuonekana ukweli; na ukweli kuwa uongo. Ni mwanapropaganda. Kwa siasa zetu za Tanzania, ambapo wapinzani hawatakiwi kutamba, Nape anafaa sana. Hana hoja lakini ana vihoja vya haja. Kisiasa, anashangiliwa na kufagiliwa.Anafaa.
Sasa Nape yuko njiapanda. Amewekwa hapo na Rais Magufuli. Hajui atende kama Waziri au Msemaji wa CCM. Hajui aseme kama Waziri au Msemaji wa CCM. Hajui kama yeye ni Waziri au Msemaji wa CCM. Anachanganya mambo. Anarukia hili na lile; anasemea hili na lile. Shaghalabaghala! Rais Magufuli amembebesha mzigo mzito Nape Nnauye.
Kwakuwa hawezi kutofautisha vya kichama na kiserikali,anafaa zaidi kichama na si kiserikali!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam