Nape Nnauye atoa Tamko Maalum la CCM kuhusiana na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini

NAPENDA KUKUSHAURI NAPE, USITUONE SISI WANANCHI KAMA MATOI YA KUCHEZEA KWA KUJIFICHA KWENYE KIVULI CHA KURA YA MAONI, MMEKATALIWA KWASABABU MMECHOKWA,WIZI,MANYANYASO KWA WANANCHI NA UBABE USIO NA TIJA.

LAZIMA TUAMBIANE UKWELI.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kilifanya makosa katika baadhi ya maeneo ambayo yamekigharimu na kusababisha wananchi kupiga kura za hasira kukiadhibu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matokeo ya uchaguzi huo ambao umeonyesha kuvinufaisha vyama vya upinzani kupitia umoja wao wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Nape alisisitiza kwamba makosa hayo ndiyo yaliyosababisha wapinzani kujinyakulia mitaa kadhaa kwa wepesi.

"Tumejifunza na tumekuwa tunajaribu kila wakati kubadili mfumo wetu wa kura za maoni lakini bado kumekuwa na matatizo. Kwa mfano, kuna Mtaa Mwenge Dar es Salaam, wanaCCM waliamua kumchagua mgombea wa upinzani baada ya jina la waliyempenda kutorudi," alisema Nnauye na kuongeza:

"Tunajua kwamba kuna maeneo mengi ambayo wapinzani wameshinda. Ukiangalia CCM tulifanya makosa katika kumweka mgombea, hivyo kusababisha hasira ambazo kwa kweli zimewafurahisha wapinzani lakini sisi zimetugharimu," alisema.

Alisema chama chake kitafanya tathmini ili kubaini kama sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow nalo ni miongoni mwa mambo yaliyochangia kupoteza baadhi ya mitaa.

Hata hivyo, Nape alisema wapinzani hawapaswi kuufurahia ushindi walioupata, bali iwe ni changamoto kwao katika kuhakikisha wanawatumikia wananchi waliowaamini.
 
ni vichekesho sana Nape anapolalamika kama Mpinzani wakati serikali ni ya CCM, hakuna siku ambayo Nape ataongea bila kuitaja Chadema, naamini anaipenda sana basi tu. eti CCM wana asilimia 84% hahahhaahaaa kazi ipo

Nape anajua hesabu huyo? Huyo ndiyo wale wasemao 3+3 = 33
 
Changamoto gani wewe acheni kutuhadaa kwa ngonjera zenu ccm nina hasira na nyie huna hata aibu eti mnaangalia changamoto za wananchi itafahamika msitufanye mazezeta enzi zimepita someni alama za nyakati case study iwe huu uchaguzi serikali za mitaa@mwanadiwani
 
Hili ombi la Nape kwamba Wakurugenzi wa baadhi ya Manispaa waadhibiwe, maana yake ni kwamba Wakurugenzi hawa wameikosesha CCM ushindi wa kishindo kwenye maeneo hayo?


 
Hizo takwimu,za Nape za kudanganya mazuzu na wasiojitambua. mayb watt wa standard 1 ndo wanaweza danganywa hivo
 
Back
Top Bottom