Nape Nnauye asema umefika wakati wa UAMSHO na JUMIKI kufutwa na mrajisi wa Serikali ya Z'Bar

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797


Katibu Mwenezi wa CCM Taifa Nape Nauye, alisema wakati umefika kwa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara Zanzibar (JUMIKI) kufutwa na mrajisi wa serikali Zanzibar. Kwani kuwepo kwa kundi hilo kuna zidi kuhahatarisha amani na umoja wa kitaifa tangu kuvamia shughuli za kisiasa Zanzibar.

Naye Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa amethibitisha kuwepo na vurgu katika eneo la Rahaleo majira y
a saa 1 usiku juzi baada ya kufanya maandamano wakitoka kwenye mhadhara katika Msikiti wa Msumbiji Magonakubwa na kupelekea majengo likiwemo tawi la CCM kuchomwa moto, thamani ya nyumba na bendera ya CCM. Uvamizi huo umesababisha uharibifu mkubwa wa mali na kituo cha umeme kunusurika kuwaka moto wakimwaga mafuta ya petroli katika jengo la ghala la kuhifadhia samani za nyumba na kuchoma moto pamoja
na bendera ya Chama cha Mapinduzi.

Inasadikiwa Mashambulizi haya yamefanyika kwa siraha za jadi na mawe. Naye katibu ameomba kufanyika uchunguzi wa kina baada ya kukana kuusika kwa kundi lake katika sakata ahilo.

Kadhalika Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja Kanali mstaafu Mahamoud Mzee alisema kitendo kilichofanywa na wafuasi wa Uamsho hakikubaliki mbele ya sheria. Alisema Zanzibar inaweza kuingia katika vurugu kubwa kama wananchi wataamua kuchukua sheria mkononi kupambana na watu wanaofanya vurugu. Ikumbukwe ni Mwezi Mei mwaka huu Jumuiya hiyo pia ilihusishwa na vurugu za ku choma makanisa na baa, visiwani humo.

Source; Mwanza Indigenous Society
 
Tuliwaambia kuwa hao ni bokoharam wakabisha..endeleeni kuwalea tena bora wamewageuka nyie wenyewe.
 

Ni kwanini CCM ndio wanaoongoza kwa Mapendekezo ya VYAMA au VIKUNDI vya KISIASA na VISIVYO vya KISIASA kupendekeza

Vifutwe? Hapo ndio CCM ijue kuwa kuna haja ya kuwa na CHOMBO HURU CHA KUDHIBITI VYAMA na VIKUNDI na sio kuwa kama CCM-B

Au kuingiliwa na CCM; Kuanzia kwa KURA... MFANO nchi zilizoendelea kuna VYOMBO ambayo Serikali haiwezi kuviingilia kama huku AFRICA na

Nchi za ASIA na MIDDLE EAST; kwa kuwa Demokrasia zetu bado zina UBABE wa watawala...
 
Kwani huyo Mrajisi wa serikali ya Zanzibar anamajukumu gani? Kwanini yeye asilione hili sikuzote mpaka aambiwe/ apewe maelekezo??
 
Who is NAPE? na hao UAMSHO ni kina nani? Na wapo kihalali au? na kwa nia gani?
Kwani wanachotaka ni nini hao UAMSHO? na kabla ya haya SERIKALI ilishawasikiliza maana ni haki yao kikatiba?
Mie nadhani tusikimbilie kuwafuta tu bali kutatua matatizo....kwani kuwafuta ni kufanya mambo kuwa more worse! kwa heri mie napita tu!
 
Watu wanataka nchi yao, lakini mnaendelea kuwang'ang'ania. Wangewachoma moto na viongozi wa ccm hapo ingekuwa safi...
 
Nape amepeta wapi mamlaka ya kuingilia siasa za nchi za nje? Jamhuri ya watu wa Zanzibar ni taifa 'huru' na lenye uwezo wa kusimamia mambo yake bila ya kuingiliwa na nchi nyingine (hata kama ni nchi jirani). Na kama Nape alituma wazee wa 'vitu vizito' kuchokonoa mambo kama walivyofanya Morogoro na Iringa basi ajue Zanzibar watamshikisha adabu. Mtoto (Nape) ana wazimu?!
 
Serikali ya mapinduzi ya zanzibar imekuwa ikicheza na moto bila yenyewe kujijua.

Kitendo cha Rais Shein kuendelea kucheza na uamsho kitamgarimu sana kwani itafika mahala hatashindwa kuwadhibiti watu hawa. wamekuwa wakichoma makanisa na biashara za watu huku serikali ikiwachekea bila hata mtu mmoja kukamatwa na kuchukuliwa hatua kali hili hali hii isijirudie.

Swala hili linachangiwa na udhaifu wa Rais Kikwete kwa kitendo chake cha kuakaa kimya bila ku demand explanation kutoka kwa shein kuakikisha vitendo hivi haviendelei.
 
Walipochoma makanisa walikuwa bado safi eti?!

Sasa wamechoma ofisi ya mume wa bosi wao ndio wanaonekana beyond repair
 
Ina maana J.K na CCM mmeshatosheka na udini mlioupanda mara tu? Waacheni tu endeleeni kuvuna mlichopanda. Na bado.
 
kudeal na uamsho ni kudeal na imani ya wazenji na response ya watu wa imani ile tunaifahamu ipo vipi. Ni busara pekee inaweza kumaliza matatizo ya wazenji
 
Yan kila mtu sisiemu ana mamlaka ya kuagiza vyama au kikundi kufutwa!
 
ningemuheshimu zaidi nape kama angesema kua chama cha ccm nacho kifutwe maana kimejihusisha na ndoa na chama cha CUF ambacho ndio UAMSHO full...so CUF na CCM VYOTE VIFUTWE...hapo ningeona kaongea cha maana
 
Mamba ambaye CCM walikuwa wanamfuga kwenye mtungi leo hii amekuwa mkubwa, kavunja mtungi na ameanza kula watoto wa mfugaji..............Hiyo ni mwanzo tu hadi pale CCM mtakapoacha sera zenu za kupandikiza udini.
 
nape amepeta wapi mamlaka ya kuingilia siasa za nchi za nje? Jamhuri ya watu wa zanzibar ni taifa 'huru' na lenye uwezo wa kusimamia mambo yake bila ya kuingiliwa na nchi nyingine (hata kama ni nchi jirani). Na kama nape alituma wazee wa 'vitu vizito' kuchokonoa mambo kama walivyofanya morogoro na iringa basi ajue zanzibar watamshikisha adabu. Mtoto (nape) ana wazimu?!

aka wazee wa vitu vyenye ncha kali!
 
Back
Top Bottom