Nape Nnauye anatarajiwa kwenda Houston -USA kusuluhisha mgogoro wa Tawi la CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape Nnauye anatarajiwa kwenda Houston -USA kusuluhisha mgogoro wa Tawi la CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kinepi_nepi, Oct 18, 2011.

 1. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi anategemea kusafiri kwenda nchini Marekani mwishoni mwa mwezi wa kumi. Akiwa nchini Marekani atakuwa na kazi ya kusuluhisha mgogoro wa Tawi la CCM Marekani lenye makao yake makuu jijini Houston na lisilo na wanachama wengi nje ya jiji la houston.

  Tangia kuanzishwa kwa Tawi hili limekuwa likikabiliwa na migogoro mingi ya kiutawala, na kushindwa kuwa na viongozi kwa muda sasa. Chanzo cha habari kinasema chanzo cha migogoro ni uchu wa madaraka, kujuana na undugu unaenziwa na wanachama wachache waliopo. Ujio wa Nape kwenye suluhu unaonekana ni neema kwa baadhi ya kambi kwani wanategemea kama ilivyo ada atachagua kuegemea upande huku baadhi ya mafungu yakitupwa pembeni. Mwanzilishi wa Tawi ameshapigwa pini na kuwekwa pembeni huku wajumbe wakizozana na kushindwa kufanya uchaguzi.

  Nape akiwa na ujumbe wa kuvua watu magamba anakibaraua cha kuwavua magamba wanachama wenzeka wa Houston ambao ni wachache kuliko katiba inavyohitaji uwepo wa tawi.

  Tawi hili la CCM jijini houstoni limekuwa likikumbana na vizingiti vingi ndani ya jamii ya wana-Houston wengi wao wakionyesha kutokuitaka CCM, na kuamini kila aliyekwenye Tawi ni kwa maslahi yake binafsi kwani hata wao kwa wao wameshindwa kuonyesha nini wanakitaka.

  Maisha ya Watanzania ndani ya Tanzania na sababu za wengi kuondoka Tanzania kwa sababu ya kuzorota kwa uchumi, kushindwa kwa utawala wa CCM kutoa haki, ajira na elimu bora ndio sababu za wengi kuondoka nchini. Ajira za kujuana na maendeleo duni huku umeme ukiwa kama bidhaa adimu kuliko huduma. Viongozi wakiwa ni wezi na kuenzi hujuma badala ya haki, wajibu na kazi, huku wezi mapapa wakiwa mitaani na dagaa ndio wakipata mijeledi keko na segerea.

  Utawala huu wa CCM umekuwa ni utawala dhalimu kwa maisha ya Mtanzania na kuwafanya vijana wengi kukosa imani na kila kiongozi wa CCM kwani ni viongozi mshahara na rushwa.

  CCM ikiwa imeshindwa kusimamia hata ahadi zake yenyewe, CCM imeshindwa kupambana na rushwa na wizi wa fedha za umma. Nape amekuwa akiimba wimbo wa kuvua gamba wakati kilichotakiwa ni kuwafungulia mashtaka wote wanaotuhumiwa na ufisadi na kuacha sheria zichukue mkondo. Kweli leo chama tawala kinacheza mchezo wa kuigiza, kimekubali kuwa kina mafisadi halafu kinabembeleza mafisadi waondoke madarakani yaaishe, na Nape kwa sababu alijua watanzania hawajui kuhoji akawapelekea wimbo kuvua gamba. Fisadi anapelekwa kwa DPP mahakamani na segera. Sijawahi sikia duniani kunaswala la suluhu na wezi wa mali ya umma. CCM mnakiri kuwa hao ni wahujumu, wezi, na mafisadi. Sasa mwanasheria mkuu, mahakama, Dpp, takukuru, cid , usalama wa taifa wanafanya nini mpaka mfanye hujuma siasa???????


  Sheria zisipofuatwa kwa sababu yeyeote ile ni maafa kwa taifa
   
 2. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  magamba yaliyoko Tanzania yamemshinda kuyavua hy ya usa atayawezaje? HAWA WT NI WANAFIKI WANAJALI MATUMBO YAO 2 WAMEKULA WAMEVIMBIWA SS WANATAFTA MCHAWI NA BADO
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Nape huyu siyo ? Yaani ndiye anaye aminiwa ?Na hilo tawi ni nguzo mno kwa CCM au kuna nini nyuma yake ?
   
 4. M

  Marytina JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Nape hana busara za kuwa msuluhishi naona anatafuta night allowances hapo
   
 5. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,381
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  Unafiki na ulafi na ufisadi ni jadi ya ccm, iwe bongo ama ughaibuni.
   
 6. Kabakabana

  Kabakabana JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 5,559
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mhxx,magamba kushnei,huyo nape bongo imemshinda ndo anaenda nje,anaenda kusaka mademu huyo
   
 7. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  kuwaza kwa kutumia masaburi ni tatizo sana. hivi hapa tz kuna tawi la chama cha labour, conservative, Democrat, Republican, KANU, ODM?? na mayo matawi ya ccm abroad yanamhudumia nani??!!
   
 8. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #8
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Sawa, Nape kama JK: kuzurura kila kona na kupiga porojo.
   
 9. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #9
  Oct 18, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hapo umemaliza kila kitu..........halafu ukute yanayogombea huko ni matoto ya magamba aliyoyaacha Tanzania.......

  Kuna mtu anaweza kutukumbusha majina yao tuone? maana nina wasiwasi ni matoto ya magamba yanatifuana hadi majuu
   
 10. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #10
  Oct 18, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni sifa za kipuuzi tu wala hawana lolote la maana hasa ukizingatia kuwa hata kupiga kura hawaruhusiwi......hapa ni kupotezeana tu kodi ndo maana hizi wanazoita ruzuku kwa vyama ni upumbavu na wizi mtupu unaowapa jeuri ya kupanda ndege kwenda kusuluhisha migogoro isiyo na manufaa yoyote kwa taifa.......

  NI UPUMBAVU NA USHENZI MTUPU
   
 11. J

  John Marwa JF-Expert Member

  #11
  Oct 18, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pili pili msio ila ina wawashia nini? Acheni kuifuatia CCM,acha wafanye mambo yao yanawahusu wao wenyewe na Chama Chao!
   
 12. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,843
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Matawi ya Maskini wa Igunga hawayataki wanataka Matawi ya Juu ili wawe wanakwenda Kutembelea Watu Kumi Kwa Kutumia $ 90,000!!! Hii ndio Nchi ya Waliwao!! Maskini Tanzania Yangu!! Mbona Wamarekani Hawana Tawi Lao la Chama Hapa Bongo?
   
 13. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wapo madarakani, upumbavu wao unatugharimu wote hata kama hatutaki. Ndio wanaotoa maamuzi kwenye maswala yote ya kitaifa. Raisi ni wa CCM na madaraka makubwa ya kikatiba yanatumaliza. 2015 wakiwa wapinzani tutawaacha wapumzike wala hatutawabughudhi ila kwa sasa wanatumia kodi zetu kutumaliza
   
 14. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #14
  Oct 18, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kaka unaweza kuwa sawa lakini sio sahihi.......unajua kuwa kwa Nap kwenda Houston anatumia gharama? Unajua kuwa gharama hizo ni sehemu ya yale mabilioni wanayopewa kama ruzuku?

  Je kwani hakuna migogoro mingi ambayo inaendelea Tanzania na Nap kama kiongozi wa Chama angeweza kuingilia kati kwa kuisukuma serikali ya chama chake kusimamia mambo kadhaa ya msingi na kutatua migogoro inayokumba jamii yake ya ndani? Hayo magamba ya nje yana manufaa gani kwa taifa kiasi cha kutumia Ruzuku itokayo kwenye kodi yetu???.......labda visingekuwa vinapata ruzuku ningekaa kimya
   
 15. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #15
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Namuonea huruma Nape, anaongezewa mzigo wakati ule wa mwanzo umemshinda. Malizana kwanza na hawa wa nyumbani kabla ya kwenda nje.
   
 16. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #16
  Oct 18, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Angeanza kwanza na mgogoro wa Arusha UVCCM.
   
 17. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #17
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,393
  Trophy Points: 280
  Anashindana na vasco da gama kwa safari
   
 18. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #18
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,210
  Likes Received: 3,622
  Trophy Points: 280
  Kambi isiyotambua kuvuliwa madaraka inaongozwa na Michael Ndejembi ambaye ni mwana familia wa Mzee Pancreas Ndejembi aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM-Dodoma na Mwenyekiti wa Wenyeviti wa mikoa ya CCM kwenye miaka ya mwanzo ya 2000;na kambi iliyonyakua madaraka kwenye uchaguzi wa jana inaongozwa na Salum Rajab ambaye ni mwana familia wa Katibu mkuu mstaafu wa wizara mbali mbali nyumbani TZ!
   
 19. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #19
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,344
  Likes Received: 19,522
  Trophy Points: 280
  Vioja......
   
 20. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #20
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,120
  Likes Received: 10,471
  Trophy Points: 280
  Nape ni muuza sura kama JK
   
Loading...