Nape Nnauye anahitaji udhibiti wa kichama wa haraka, atatudhalilisha!

Natoa wito wa dharura kwa chama chetu cha Mapinduzi-CCM. Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama mkoani Lindi, anahitaji udhibiti na usaidizi wa haraka wa kichama. Leo, ameanza vibaya kwa kuuliza swali lisilo swali. Mara ya kwanza, kosa la kwanza halafu kubwa. Ameuliza swali la kiugomvi na kukwaza. Likakataliwa.

Alitaka pia kujinasibu kwa kujitambulisha kama asiyejulikana. Hata waliokuwa karibu yake wakamshangaa. Nani asiyemjua Nape pale Bungeni hadi ajitambulishe. Kama si ulimbukeni ni nini? Nje ya Bunge, ameendelea kutamba kwa maneno ya kejeli kwa wapinzani hapa Dodoma.

Nape hatakuwa Mbunge mzuri kwa kujenga hoja. Atakidhalilisha chama pale zitakapowekwa hoja mezani kujadiliwa na huku chama kikimpa nafasi ya kujinafasi. Atakidhalilisha chama chetu akiachwa aende kombo kama alivyoanza leo. Nape adhibitiwe na kuwa na ushauri wa kichama, hasa kutoka kwa Wabunge wazoevu. Afanyiwe hivyoo haraka!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)

- nonsense!!

le Mutuz
 
Oh. ahsante ngoja waje hapa litajadiliwa kwa undani kabisa ila mimi naona nyoka makengeza kambeba medee angemwachia ajibu tu kamnyima nape kupata jibu.sahihi
Jibu gani sahihi unalotaka hapo? Huyo Nape alichokuwa akikifanya hapo ni kuendeleza siasa za maji taka ambazo ndiyo zilizozoeleka kwenye chama chake cha magamba.
 
Jibu gani sahihi unalotaka hapo? Huyo Nape alichokuwa akikifanya hapo ni kuendeleza siasa za maji taka ambazo ndiyo zilizozoeleka kwenye chama chake cha magamba.

Sawa ole medee umshukuru nyoka makengeza kakusaidia kujibu
 
tunahitaji watu wa aina yake sana,,,atakutana na waropokaji wenzake akina lisu na genge lake,,,,tumekua na wajenga hoja wengi so tunashkuru sasa tunae km yy
 
Hivi bunge ambalo kuna watu waliyotaka kwenda huko bungeni ukisikia majina yao unashangaa huyu nae anataka kwenda bungeni? yote ni kutokana na hali ya bunge lililopita na ndiyo hata hao watu wakaona kazi ya ubunge ni rahisi kiasi cha wao nao kuimudu. Hivyo mie binafsi nao kile alichokifanya Nape ndivyo vitu vilivyomvutia yeye kwenda kule,hata baadhi ya waliyokuwa wagombea uspika wameliongelea hali ya bunge lililopita ambavyo lilivyokuwa.
 
ndugu wana jf kwa mara ya kwanza leo nape ameanza kuonyesha makeke yake bungeni wahenga walisema kila jambo na wakati wake tumeshuhudia kwa miaka mitano iliopita mheshimiwa lusinde akiwa ndie mbunge kilaza kuliko wote lakini kwa miaka hii mitano naona lusinde akimkabizi kofia nape kushikilia hiyo nafasi huku yeye akionekana anaafadhali kutokana na swali alilouliza nape linaakisi jinsi alivyo mweupe kichwani na nafikiri tutashuhudia mengi sana kipindi hiki cha miaka mitano ongera lusinde hongera nape kupokea kijiti
 
Anadhani bungeni nimahali pamipasho huyo. Not this time my dear Nape.Bunge la safari linaendesha kisomi na hata ukiangalia cv ya wabunge wengi pale ni wasomi. Kama hata wabunge wa chama ambacho alikuwa katibu mwenezi wamemshangaa atatoboa kweli?
God have mercy on Him is because of low thinking capacity
 
We mwenyewe kilaza kajifunze kiswahili kwanza ndio urudi kuwekaa mabandiko yako hapa nini maana kumkabizi??!!
 
Huyu jamaa mnamgwaya sana bavicha, mtamuelewa tu! Miaka mitano atawanyoosha tu! Chuki yenu ni kwa sababu mnamgwaya!
 
Back
Top Bottom