Nape Nnauye: Anachofanya Trump kwa vyombo vya Habari, ingefanywa Afrika kingetokea nini??!!

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
Anachofanya Trump kwa vyombo vya Habari, ingefanywa Afrika kingetokea nini??!!
tmp_8265-Screenshot_2017-02-26-12-03-08-411112428.png

Nini maoni yako kuhusiana kauli hiyo ya Nape Nnauye?
White House blocks CNN, BBC, New York Times, LA Times from media briefing
 
Nape amesahau alivyotunyima uhuru wa kujieleza?, umesahau mmetuwekea sheria za kandamizi kwenye mitandao ya kijamii? Hasa Kuna utofauti gani?
 
Huyu Nape vipi tena? Wamefanya mangapi kuminya vyombo vya habari na leo anatukejeli ujingaujinga ametuona sisi ni kama wajinga.
 
MBONA NDIO UNACHOKIFANYA NDUGU NAPE NA NDUGU MAGUMASHI HAPA TZ
 
Mbona ameona tu suala la vyombo kwanini wahaigi mazuri yao, yaani wanasubiri mabaya ya huko ili wafananishe na hapa TZ?
 
Vyombo vya habari vya USA vinacheza na akili ya Trump vinamgeuza vinavyotaka.

Amewafukuza CNN na baadhi ya vyombo vingine Ijumaa Ikulu Kuchukua habari zake.
 
Kwani Trump amevifanyaje vyombo vya habari??
Si anavikosoa tu.. Wao hapa Tanzania wanavifanyaje?
 
Nape labda amesahau ule mswada wa kukandamiza uhuru wa kutoa maoni kwenye social media
Kwani Trump amevifanyaje vyombo vya habari??
Si anavikosoa tu.. Wao hapa Tanzania wanavifanyaje?
 
Hasichanganye na msituchanganye
Trump kawazuia kushiriki kwenye mkutano wa waandishi na rais ikulu tu kwa kuwa wanapotosha taarifa sake.
Hajawazuia kuripoti au kusema wanachotaka au kuandika watakachoona

Hilo LA trump hata hapa linafanyika kwamba ikulu inaamua nani aje nani hasije kwenye mkutano wake, na sio wote wanashiriki mkutano ya RAIs japo Tuseme marwkani vilivyozuiliwa mi vyombo vikubwa
Pia trump amekataa kushiriki dhifa ya wanahabar hilo hata magufuli anaweza kukataa sio suala LA uafrica au uzungu
 
Anachofanya Trump kwa vyombo vya Habari, ingefanywa Afrika kingetokea nini??!!
View attachment 474685
Nini maoni yako kuhusiana kauli hiyo ya Nape Nnauye?
Nape naye asitake kutufanya sisi majuha.

tofauti kati ya Trump na kina Nape i wazi....

Trump hafurahishwi na media, so anakataa isifanye coverage kwenye presser zake but hazuii cha kuandika/kutangaza wala hazifungii. kwa jinsi hii, media ipo huru kuripoti inachoona kinafaa, hata mbofumbofu dhidi ya Trump mwenyewe!

on the contrary, akina Nape wao wasipofurahishwa na media, wanakimbilia kuvifungia. hapa media freedom hakuna!
 
Hasichanganye na msituchanganye
Trump kawazuia kushiriki kwenye mkutano wa waandishi na rais ikulu tu kwa kuwa wanapotosha taarifa sake.
Hajawazuia kuripoti au kusema wanachotaka au kuandika watakachoona

Hilo LA trump hata hapa linafanyika kwamba ikulu inaamua nani aje nani hasije kwenye mkutano wake, na sio wote wanashiriki mkutano ya RAIs japo Tuseme marwkani vilivyozuiliwa mi vyombo vikubwa
Pia trump amekataa kushiriki dhifa ya wanahabar hilo hata magufuli anaweza kukataa sio suala LA uafrica au uzungu
Nilitaka kushangaa,marekani kuweka sheria kandamizi kama huku TZ???? Freedom of speech ni namba moja kwa wenzetu kabla ya kuwa rais ,na lazima uheshimu hilo.Fanya utumbo wako wote lakn heshimu freedom of speech.
 
freedom of matusi ndo mnachopigania
 
Ni sawa na marekani mnakojidaia ninyi humu ndani, maana kitu kidogo oh! Bora Trump atutawale, sasa na huko ndo hayo ya nchini mwetu, hivo tukae ziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiik!
 
Back
Top Bottom