Nape Nnauye amjibu Mangula, ni Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,889
2,000
Salaam Wakuu,

Baada ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula kuzungumzia Bandari ya Bagamoyo kwamba haipo kwenye ilani, Mbunge wa Mtama Moses Nnauye(CCM) ameibuka na kusema kwamba kuna miladi mingi imetekelezwa ambago haikuwa kwenye ilani.

Mangula alisema anashangaa huu mjadala wa Bandari ya Bagamoyo unatokea wapi kwa kuwa mradi huo haupo. Mangula kasema hakuna haja ya watu kupotosha wananchi,” Mangula akizungumza na Gazeti la Uhuru ameeleza kwamba kilichoahidiwa ni ujenzi wa gati ya Bagamoyo.

“Ipo miradi ya maboresho ya bandari, lakini kwa upande wa Bagamoyo kilichopitishwa ni ujenzi wa gati, sio bandari,” amesema Mangula.

Baada ya kauli hiyo, Moses Nape Nnauye ikamlizimu aandike kwenye Mtandao wa kijamii kwamba sio kila miradi inayotekelezwa ipo kwenye ilani.

Nape kaandika hivi:

Najiuliza tu kimyakimya hivi,

JK alijenga UDOM bila kuwa kwenye Ilani ya CCM. JPM kajenga Bwawa la Stiglers, Ufufuaji ATCL, Kuhamia Dodoma, Daraja Kigongo/Busisi nk bila Ilani ya 2015/20. Kulikuwa na kosa!Serikali kufanya jambo la masilahi kwa nchi inafungwa na Ilani!?

Maajabu!
Nini Mtazamo wako wewe MwanaJF? Kwamba Serikali itekeleze yaliyopo kwenye ilani tu au iangalia vipaumbele vya wananchi?

Pia soma: Makamu mwenyekiti CCM, Mzee Mangula: Bagamoyo tuliahidi kujenga gati sio Bandari
 

Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
3,085
2,000
Nape atulie, hana hadhi wala sifa za kuhoji hoja za mwenyekiti wake.

Nape ameshajulikana ni mtu anaetawaliwa na njaa kuliko kitu chochote. Sasa anajaribu kujionyesha kwa samia ili angalau akumbukwe.

Nape's integrity is compromised, he has no moral authority to question or advise anything kwa sababu ameonyesha kwamba he is working for his stomach.

Makamu Mwenyekiti amesema Bagamoyo haikuahidiwa Bandari, iliahidiwa gati, shida iko wapi?
 

hydroxo

JF-Expert Member
Oct 19, 2015
1,926
2,000
Nape atulie, hana hadhi wala sifa za kuhoji hoja za mwenyekiti wake.

Nape ameshajulikana ni mtu anaetawaliwa na njaa kuliko kitu chochote. Sasa anajaribu kujionyesha kwa samia ili angalau akumbukwe.

Makamu Mwenyekiti amesema Bagamoyo haikuahidiwa Bandari, iliahidiwa gati, shida iko wapi?
Kwani chato waliahidiwa uwanja wa ndege bohari kuu ya madawa na chuo cha VETA?
 

Nkerebhuke

Senior Member
Nov 1, 2021
152
500
Hawa vijana wasioweza kulitumikia taifa mpaka wawe mawaziri hawafai, wanajiona bora zaidi ya wengine, uongozi wa serikalini usitafutwe kwa kelele nyingi za mitandaoni, uadilifu wa mtu na uchapakazi wake ndio uwe vigezo.
Kaka toa maoni kutokana na hoja ya nappe mbona tunapenda majungu sio poa. Nape katoa mawazo yake toa na wewe yakwako. Tabia ya usaka fursa ipo miaka mingi hata ingekuwa wewe
 

Heijah

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,019
2,000
Nape atulie, hana hadhi wala sifa za kuhoji hoja za mwenyekiti wake...
Na makamu mwenyekiti anapata wapi nguvu ya kumpinga mwenyekiti? Nape yuko sawa sera ni elekezi tu huwezi kuwa na sera ya miaka 5 halafu usibadilike dunia inaenda kasi sana sasa utakaa vipi na mawazo kwa miaka 5 serikali inaendeshwa kila mwaka na inaweka budget kwa mwaka.

Huyu makamu mwenyekiti ni nyoka katoka kwenye pango Mama anatakiwa kupiga rungu kichwa ndio hawa walikuwa nyuma ya ile story Mama hagombei tena kwenye gazeti la chama sasa kajitokeza.

Toka lini ukampinga mwenyekiti wako hadharani? utamaduni wa CCM haya mambo ndani ya vikao. Mwanga kawanga mchana kaonekana Mama piga rungu haraka huyo mzee mchawi.
 

Lombo

JF-Expert Member
Jan 21, 2011
5,340
2,000
Na makamu mwenyekiti anapata wapi nguvu ya kumpinga mwenyekiti? Nape yuko sawa sera ni elekezi tu huwezi kuwa na sera ya miaka 5 halafu usibadilike dunia inaenda kasi sana sasa utakaa vipi na mawazo kwa miaka...
WAchawi, Huwa hawapigani marungu ...wanahawiana!!
 

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
10,557
2,000
Salaam Wakuu,

Baada ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula kuzungumzia Bandari ya Bagamoyo kwamba haipo kwenye ilani, Mbunge wa Mtama Moses Nnauye(CCM) ameibuka na kusema kwamba kuna miladi mingi imetekelezwa ambago haikuwa kwenye ilani...
Mangula sumu aliyopewa bado inamsumbua.
 

Bendanda

JF-Expert Member
Jun 25, 2020
326
500
Mangula yupo sahihi amezungumzia ilani ya chama inavyosema, lakini na serikali pia wakati mwingine inatekeleza vitu vingine ambavyo haviko katika ilani! ila suala la bandari ya Bagamoyo linafikirisha sana!!🤷‍♂️
 

Action and Reaction

Senior Member
Oct 16, 2021
180
250
Na makamu mwenyekiti anapata wapi nguvu ya kumpinga mwenyekiti? Nape yuko sawa sera ni elekezi tu huwezi kuwa na sera ya miaka 5 halafu usibadilike dunia inaenda kasi sana sasa utakaa vipi na mawazo ...
Kweli bado hujakua, kama kweli umekua usingeandika hivi! Rabish
 

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
10,557
2,000
Na makamu mwenyekiti anapata wapi nguvu ya kumpinga mwenyekiti? Nape yuko sawa sera ni elekezi tu huwezi kuwa na sera ya miaka 5 halafu usibadilike dunia inaenda kasi sana sasa utakaa...
Mzee Mangula hawezi kuwa dira kwa miaka yote.

He is a dinasour kwa sasa.

Mama aachiwe apige kazi, na ni muda muafaka sasa kuisafisha CCM.

Wakati wa Mwalimu kulikuwa na sera ya KUNG'ATUKA, mzee Mangula anashauriwa aisome vizuri sera hiyo na aende na wakati.
 

Action and Reaction

Senior Member
Oct 16, 2021
180
250
Salaam Wakuu,

Baada ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula kuzungumzia Bandari ya Bagamoyo kwamba haipo kwenye ilani, Mbunge wa Mtama Moses Nnauye(CCM) ameibuka na kusema kwamba kuna miladi mingi imetekelezwa ambago haikuwa kwenye ilani...
😂😂Kweli ukiamua kumficha Nape unamficha vzr tu!... Yaan Nape saizi ndo anaonekana mjini, miaka mitano yuko vichochoroni daa😁😁
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom