Nape Nnauye akiwa kata ya kimandolu, Arusha

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,536
2,264
Katika hotuba hiyo amewataka wananchi wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura na waondokane na hofu yoyote kwa vile usalama umeimarishwa vya kutosha.

Nape amewaomba wananchi wazitumie vizuri haki zao za msingi za kupiga kura kumchagua mgombea wa CCM ambaye chama chake kilipewa majukumu ya kuongoza nchi na wananchi walio wengi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kutokana na ilani yake nzuri na inayotekelezeka ambayo mambo yaliyopo ndani ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi ni pamoja na kutatua matatizo ya wana Kimandolu kama serikali inavyofanya.

Nape aliwakumbusha wananchi kuwa kinachotekelezwa kwa sasa nchini ni ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 kupitia serikali yake na wasikubali kudanganywa na wagombea wa vyama vingine kama hao wagombea na vyama vyao watawaletea maendeleo.

Maendeleo katika kata ya Kimandolu yataletwa na CCM kupitia ilani yake na si vinginevyo.






Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ,akiwa kwenye mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea wa kiti cha udiwani cha kata ya Kimandolu,Arusha.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Kimandolu wakati wa kampeni za udiwani .

Mgombea wa kiti cha udiwani, Ndugu Edna Jonathan Sauli akisalimia wakazi wa kata ya Kimandolu wakati wa kampeni za udiwani.
 
Hao watu wamekuja kumshangaa nape au kusikiliza sera?mbona ni kama 28 tu?sana sana ni magamba yanayopewa posho....ngoja waje makamanda hapa waweke picha ya nyomi....huo ni mkutano wa familia ndani ya nyumba!!!
 
Hapo panaonyesha Nape anawasiwasi kama mtu anayetaka kufa. Anashindwa kuangalia watu na mgombea wake.

Hii inaonyesha kakata tamaa na hali inayoiona.
 
Kelele za chekechea wa kisiasa hazimzuii mtu mzima kuendelea na shughuli zake.

Wao wamebakiwa na cheap politics zinazokolezwa na spinning za kijinga na siasa zilizopitwa na wakati za kueneza sera zao wanazo zihubiri mpaka bungeni za kutaka kufahamu nani ni msagaji na nani siyo msagaji.

waacheni waendelee na siasa zao za kilaghai na maji taka.

CCM tumedhubutu, tumeweza na sasa tunatenda.

Makada tuko mikoani tunafanya kazi tuliyotumwa na wananchi kupitia kwenye sanduku la kura 2010.
 
Nape na mwigulu wanampa shida sana slaa nadhani angekuwo sijui ingekuwaje.
 
Hamna kitu cha namna hiyo Ndg,hujajua tu kusoma alama za nyakati nguvu na gharama wanazotumia ccm kukabiliana na cdm ni kubwa kiac kwamba wasingekua wamejipanga wangeishapotea ck nyingi.
 
Hivi kumbe Arusha kuna wana CCM waliobakia. Mi nilidhani akina Nape wakisema CHADEMA ni chama cha watu wa kaskazini nakajua huko hayo manguo ya laana (Ya kijani) hayavaliwi kabisa. Anyway kila la heri kwenye uchaguzi wenu huo
 
Kelele za chekechea wa kisiasa hazimzuii mtu mzima kuendelea na shughuli zake.

Wao wamebakiwa na cheap politics zinazokolezwa na spinning za kijinga na siasa zilizopitwa na wakati za kueneza sera zao wanazo zihubiri mpaka bungeni za kutaka kufahamu nani ni msagaji na nani siyo msagaji.

waacheni waendelee na siasa zao za kilaghai na maji taka.

CCM tumedhubutu, tumeweza na sasa tunatenda.

Makada tuko mikoani tunafanya kazi tuliyotumwa na wananchi kupitia kwenye sanduku la kura 2010.

Yes, naona unajitahidi sana kuandika propaganda and I believe soon utavuka kutoka "book 7" group na kupewa kazi ya ukatibu mwenezi wa kata. Anyway, Nape ameonyesha kukomaa kidogo kwa maneno yake aliyoyatumia kwenye kampeni ukilinganisha na Mwigulu ambaye kusema kweli anaiharibia sana CCM.

Tiba
 
Back
Top Bottom