Nape Nnauye akiongoza mkutano wa kampeni kata ya Temi

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,536
2,264
Friday, June 14, 2013

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Themi na kuwaambia wasirudie kosa la kudharauliwa kwa kuchagua watu wasiotambua thamani ya kura zao.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahakikishia wana Themi kuwa wakati huu ni wa kuirudisha heshima ya Arusha na kwa kumchagua mgombea wa CCM kutasaidia sana kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika mji huo.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimtambulisha mgombea wa kiti cha udiwani kata ya Themi, Victor G. Mkolwe, Juni, 13,2013 .

Mgombea wa kiti cha udiwani kata ya Themi, Victor G. Mkolwe akihutubia wakazi wa kata hiyo na kuwaelezea moja ya mikakati yake ya kuleta maendeleo kwa wakazi hao,ambpo pia aliwaambia yeye hatangulizi siasa bali maendeleo na anatambua wakazi wake vizuri na changamoto zao na namna ya kuwasaidia.

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Arusha, Catherine Magige akihutubia wakazi wa kata ya Themi ambapo pamoja na kuwaomba kumpigia kura mgombea wa udiwani kwa tiketi ya CCM pia aliahidi kuwasaidia wakina mama Wajane ambao walitelekezwa na ahadi za uongo za vyama upinzani.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na baadhi ya wakina mama Wajane ambao walidanganywa na vyama vya upinzani na sasa wamerejea CCM.

Wajane wa kata ya Themi wakisalimiana na mbunge wa viti maalum wa mkoa wa Arusha ,Catherine Magige.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na vijana wa Arusha mjini waliokuwa wakijiburudisha na mchezo wa karata.

Meya wa Jiji la Arusha, Ndugu Gaudence Lyimo akihutubia wakazi wa kata ya Themi na kuwataka wasifanye makosa katika uchaguzi huu.

Rehema Mohamed maarufu kama Iron Lady akihutubia wakazi wa kata ya Themi ambapo aliwataka wakazi hao kuwa makini sana na wanasiasa wasiokuwa na mipango ya maendeleo.

Kikundi cha ngoma cha Kambarage kikiburudisha wakazi wa kata ya Themi wakati wa mkutano wa kampeni za udiwani kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi.

Kijana anayefahamika kwa jina la Mboya ambaye alikuwa mstari wa mbele katika harakati za Chadema,akihutubia wakazi wa kata ya Themi wilaya ya Arusha mjini na kuwaambia wasirudie kuchagua vyama ambavyo kura yao itapotea kwa matapeli wa kimataifa.

Nico ambaye naye alikuwa mstari wa mbele kuongoza mipango michafu ya kuvuruga amani ya Arusha, amekiri kuwa chama pekee cha kisiasa Tanzania kwa sasa ni CCM na ameomba wakazi wa kata ya Themi kuungana na kumchagua diwani anayetokana na CCM ili kuleta maendeleo na si migomo.

MNEC wa wilaya ya Arusha mjini Godfrey Mwalusamba akihutubia wakazi wa kata ya Themi,ambapo aliwaambia kuna uhumu wa kufanyia kazi maendeleo yao zaidi kuliko kushabikia vitu visivyo na tija.

"Hii ni ngome ya CHADEMA". Really?.

Kelele za chekechea wa kisiasa hazimzuii mtu mzima kuendelea na shughuli zake.

Wao wamebakiwa na cheap politics zinazokolezwa na spinning za kijinga na siasa zilizopitwa na wakati za kueneza sera zao za kutaka kufahamu nani ni heterosexual, gay or lesbian.

Waacheni waendelee na siasa zao za kilaghai na maji taka ambazo wanaenda nazo mpaka bungeni.

CCM tumedhubutu, tumeweza na sasa tunatenda kama wananchi wanavyotaka kutende.
 
Ama kweli kura sio mchezo, hadi wajane wameingizwa kwenye propaganda za ccm....!!!!
 
"Hii ni ngome ya CHADEMA". Really?.

Kelele za chekechea wa kisiasa hazimzuii mtu mzima kuendelea na shughuli zake.

Wao wamebakiwa na cheap politics zinazokolezwa na spinning za kijinga na siasa zilizopitwa na wakati za kueneza sera zao za kutaka kufahamu nani ni heterosexual, gay or lesbian.

Waacheni waendelee na siasa zao za kilaghai na maji taka ambazo wanaenda nazo mpaka bungeni.

CCM tumedhubutu, tumeweza na sasa tunatenda kama wananchi wanavyotaka kutende.

Naona sasa Mmeanza kujifunza.Toka mfike Arusha hamjaongea Sera yenu ya Ukaskazini na Udini.
 
Picha uliyoleta ni Aibu tupu.Inaonekana wahudhuriaji ni Watoto na Wapita njia wanaoshangaa Vikundi vya Ngoma.Eneo lenyewe la Mkutano ni kama Barazani kwa Mtu.
 
Friday, June 14, 2013

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Themi na kuwaambia wasirudie kosa la kudharauliwa kwa kuchagua watu wasiotambua thamani ya kura zao.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahakikishia wana Themi kuwa wakati huu ni wa kuirudisha heshima ya Arusha na kwa kumchagua mgombea wa CCM kutasaidia sana kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika mji huo.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimtambulisha mgombea wa kiti cha udiwani kata ya Themi, Victor G. Mkolwe, Juni, 13,2013 .

Mgombea wa kiti cha udiwani kata ya Themi, Victor G. Mkolwe akihutubia wakazi wa kata hiyo na kuwaelezea moja ya mikakati yake ya kuleta maendeleo kwa wakazi hao,ambpo pia aliwaambia yeye hatangulizi siasa bali maendeleo na anatambua wakazi wake vizuri na changamoto zao na namna ya kuwasaidia.

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Arusha, Catherine Magige akihutubia wakazi wa kata ya Themi ambapo pamoja na kuwaomba kumpigia kura mgombea wa udiwani kwa tiketi ya CCM pia aliahidi kuwasaidia wakina mama Wajane ambao walitelekezwa na ahadi za uongo za vyama upinzani.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na baadhi ya wakina mama Wajane ambao walidanganywa na vyama vya upinzani na sasa wamerejea CCM.

Wajane wa kata ya Themi wakisalimiana na mbunge wa viti maalum wa mkoa wa Arusha ,Catherine Magige.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na vijana wa Arusha mjini waliokuwa wakijiburudisha na mchezo wa karata.

Meya wa Jiji la Arusha, Ndugu Gaudence Lyimo akihutubia wakazi wa kata ya Themi na kuwataka wasifanye makosa katika uchaguzi huu.

Rehema Mohamed maarufu kama Iron Lady akihutubia wakazi wa kata ya Themi ambapo aliwataka wakazi hao kuwa makini sana na wanasiasa wasiokuwa na mipango ya maendeleo.

Kikundi cha ngoma cha Kambarage kikiburudisha wakazi wa kata ya Themi wakati wa mkutano wa kampeni za udiwani kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi.

Kijana anayefahamika kwa jina la Mboya ambaye alikuwa mstari wa mbele katika harakati za Chadema,akihutubia wakazi wa kata ya Themi wilaya ya Arusha mjini na kuwaambia wasirudie kuchagua vyama ambavyo kura yao itapotea kwa matapeli wa kimataifa.

Nico ambaye naye alikuwa mstari wa mbele kuongoza mipango michafu ya kuvuruga amani ya Arusha, amekiri kuwa chama pekee cha kisiasa Tanzania kwa sasa ni CCM na ameomba wakazi wa kata ya Themi kuungana na kumchagua diwani anayetokana na CCM ili kuleta maendeleo na si migomo.

MNEC wa wilaya ya Arusha mjini Godfrey Mwalusamba akihutubia wakazi wa kata ya Themi,ambapo aliwaambia kuna uhumu wa kufanyia kazi maendeleo yao zaidi kuliko kushabikia vitu visivyo na tija.

Kweli CDM ni Moto kwa CCM.yaani huyu NICO Muendesha Bodaboda Soko kuu kijiwe cha kahawa ndio mnatudanganya kuwa eti ndie aliekua anatumika na CDM kuratibu Vurugu? Kwanza huyu Muendesha bodaboda tena ya kupewa anaweza kumshawishi nani.

Huyu NICO ni malaya wa SIASA anachofanya ni kutafuta Umaarufu kwa mgongo wa CDM! imekua ni kawaida kabisa kwa mtu yeyote yule anaetaka Umaarufu Kusiasa basi lazima atafute Singo ya CDM.
Embu angalieni jinsi Ccm ilivyoishiwa na kufilisika kisera,mara wawatafute wacheza karata,mara wanawake wajane mara Waliomwagiwa Tindikali basi ilimradi tu waonekane wana huruma.
Kweli usilo lijua ni sawa na Usiku wa Giza.

MUNGU NI WA HAKI.OLE WAO WALE WANAOGEUZA UKWELI KUA UWONGO,NA UWONGO KUWA UKWELI.Asema Bwana wa Majeshi!!
 
Aibu tupu kwa ccm mimi naomba niweke hii moja ya mkutano wa Nape(nepi)pale elerai jana japo nilipiga kwa mbali nikiofia kung'olewa kucha
 
Attachments

  • uploadfromtaptalk1371271844007.jpg
    uploadfromtaptalk1371271844007.jpg
    74.4 KB · Views: 132
Na pia naweka moja ya mkutano wa Mh Lema hapo hapo Elerai jana
 
Attachments

  • uploadfromtaptalk1371272087892.jpg
    uploadfromtaptalk1371272087892.jpg
    106.8 KB · Views: 142
Nashanga watu wanaponda watu waliudhuria kwenye mikutano ya ccm, hao ndio wapiga kura wenyewe, hata km wakiwa wawili, si kujaza mikutano kumbe kura hamna, hapo cdm ndio mnaweweska
 
Back
Top Bottom